Mcheza Pooltable, Abdallah Hussein(Dullah) aelekea Uganda kwenye Mashindano ya wazi "PAU Pool Grand Open"

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,713
13,463

MCHEZAJI wa Pooltable anayeshikilia kiwango cha namba moja Tanzania, Abdallah Hussein(Dullah) leo mapema ameondoka kuelekea Uganda kwenye Mashindano ya wazi "PAU Pool Grand Open" yaliyoandaliwa na Chama cha Pool nchini Uganda(PAU).

Mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki hii May 28 - 29, 2020 katika Ukumbi wa SEETA Kampala Uganda kwa kushilikisha Wachezaji nguli(Maarufu) Afrika ambao tayari wameshathibitisha kushiriki.

Wachezaji waliothibitisha kushiriki ni kutoka, Afrika Kusini, Zambia, Kenya, Tanzania na wenyeji Uganda.

Abdallah Hussein(Dullah) ametamba kwenda kufanya vizuri kwenye mashindano hayo baada kushiriki mashindano ya Afrika Mashariki hivi karibuni yaliyofanyika Nchini Kenya nakupata uzoefu wa kutosha.

Alisema Dullah, 'Nina ndoto za mbali sana za kuitangaza Nchi yangu ya Tanzania kupitia mchezo wangu wa Pool, naomba sana Wafadhili wangu, ndugu zangu, marafiki zangu na Watanzania kwa ujumla mniombee' alimaza Dullah huku akiingia kwenye Bus likielekea Kampala Uganda.
 
Alirudi???
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…