Mbunge wa CHADEMA amtolea tamko Chid Benz

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
DAR ES SALAAM! Mbunge wa Mikumi kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Joseph Haule ‘Profesa Jay’ (pichani) amesema hali ya Mbongo Fleva, Rashid Abdallah Makwiro (31) ‘Chid Benz’ ni matokeo ya matumizi yaliyobebea ya madawa ya kulevya ‘unga’, Amani lina mchirizi wake.

Hivi karibuni, Chid Benz aliripotiwa na baadhi ya mitandao ya kijamii akionekana na hali isiyoridhisha kiasi kwamba, baadhi ya wachangiaji walisema; inauma sana!

Mwonekano wa sasa wa Chid ni wembamba wenye maswali mengi huku marafiki zake wa karibu wakidai kwamba ‘unga’ umemfanya afikie hali hiyo.

Akizungumza na gazeti hili juzi Jumanne jijini Dar baada ya kuombwa mchango wake kuhusu hali ya Chid, mbunge huyo alisema:

“Hili ni tatizo sana kwa sasa. Si kwa Chid Benz tu, bali kwa vijana wengi sana wa nchi hii ambao ni nguvu kazi ya taifa hili. Tusiwanyanyapae wale wanaoathirika na madawa bali tuwasaidie tunavyoweza ili warudi kwenye hali zao za kawaida.

“Naomba sana serikali ilichukulie suala la madawa ya kulevya kama janga kubwa sana na ilikimee kwa nguvu zote na kuweka sheria na adhabu kali ili kulinusuru taifa hili linalopoteza nguvu kazi kubwa kwa madawa ya kulevya.”

Jumatatu iliyopita, Amani lilimsaka Chid mwenyewe ili kuweza kuzungumza naye kuhusu hali yake lakini mara zote alionesha kutokuwa na utayari wa kukutana na gazeti hili hata pale gazeti lilipowatumia watu wake wa karibu, akiwemo Mwanamuziki wa Kizazi Kipya, Kalama Masoud ‘Kalapina’.

Akizungumza na Amani juzi kuhusu watu walioathirika na unga, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alisema wale ambao vipimo vinaonesha wameathirika, wajitokeze wakatibiwe kuondoa madhara mwilini, lakini serikali inaendelea kuwakamata wasambazaji wa biashara hiyo haramu.

“Serikali inafanya juu chini kuikomesha biashara hiyo. Kuhusu kuwakamata watumiaji, kunataka uhakika. Inawezekana mtu alitumia muda mrefu akaathirika, hao waende wakatibiwe tu ili kuondoka athari,” alisema Masauni…

KUMBUKUMBU ILIYOPITA
Oktoba mwaka 2014, Chid Benz alifikishwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar akikabiliwa na mashtaka matatu, likiwemo la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya Heroin yenye thamani ya Sh. 38,638, bangi ya Sh. 1, 720 na vifaa ya kuvutia dawa hizo, kijiko na kigae.

Chid Benz alisomewa mashtaka yake saa 7:50 mchana na Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Warialwande Lema aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo.
Wakili Mwanaamina alisema Chid alinaswa na mzigo huo Oktoba 24, mwaka huo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Ilala jijini Dar es Salaam.

Februari mwaka jana, Chid alipatikana na hatia ambapo Hakimu Lema alimhukumu kifungo cha miaka miwili jela au kulipa faini ya Sh. 900,000 ambapo aliweza kulipa kiasi hicho na kuwa huru.
 
Bado vita ya biashara/matumizi ya madawa ya kulevya Tanzania.....inafanyika kiunafki Sana...

Ovaaaa
 
kwenye historia ya Tanzania hakuna msanii wa muziki wa bongo aliewahi kupotea kwenye game na kurudi kwenye peak, sembuse chid wa madawa? huwa wanasema tumerudi ila cha kushangaza ndo hupotea zaidi! kama huyu chidi namshauri asije akafikiri kuwa anaweza kurudi akawa kama alivyokuwa mwanzo, akubaliane na matokeo kuwa kwenye game ndo ashapotea hivyo hata akawange! cha msingi namshauri apambane hayo madawa ayaache na aombe wadau wamchangie walau apate mtaji akalime mpunga kule Kyela, au hata matikiti maji! kilimo kinalipa, sio lazima mziki tu
 
Mi naona wangekamata watumiaji wote wawekwe ndani tuone nani aranunua
 

ULICHOSEMA NIKWELI KABISA HUJAKOSEA.

ILA UKWELI HUO INGEKUWA WEWE NDO UNAPEWA INAUMA SANA, NADHANI WASANII/VIJANA WENGINE WANA LA KUJIFUNZA HAPA

MJINI NOMA, KAMA MBUGANI WAZAIFU HUFANYWA KITOEO KWA MAJAYANTI
 
ULICHOSEMA NIKWELI KABISA HUJAKOSEA.

ILA UKWELI HUO INGEKUWA WEWE NDO UNAPEWA INAUMA SANA, NADHANI WASANII/VIJANA WENGINE WANA LA KUJIFUNZA HAPA

MJINI NOMA, KAMA MBUGANI WAZAIFU HUFANYWA KITOEO KWA MAJAYANTI
Na siku zote ukweli unauma!
 
Vijana waishie kwenye bange haya maunga wawaachie kina 50 centi labda Kama wameamua kujiua. Napendekeza mtu akishikwa faini iwekali na ijizidishe kadri inavyoenda kwa hao waliomwuzia. Akikataa kuwataja adhabu iongezeke zaidi.
Hiyo lakitisa aliyotozwa ni kituko kwa nchi iliyoamua kupambana na madawa! Au walihisi wanamsaidia supastaa...
. Tuwe siriaz! Kesi ya kukutwa na kobe haifai kuwa kubwa kuliko kesi ya madawa haramu
 
MADAWA NI KUJITAKIA. hili wala si la kusingizia mtu au kitu. ni sawa na leo hii iwe kuna ugonjwa unaotokana na kunywa soda. then kesho na keshokutwa eti tukuonee huruma kwa kuwa unaumwa ugonjwa unaotokana na kunywa soda. huo ni upumbavu wako. kwa nini usiache kunywa soda? soda si kitu cha lazima, tena kina gharama. tuache kuwaonea huruma mama,dada,ndugu zetu wanaokufa kwa magonjwa ya kuhara kwa sababu wanalazimika kunywa maji machafu tuje kuhangaika na mtu anayetumia madawa ya kulevya tena huwa wanajiona wao ndo wajanja,wamarekani na wana enda na utandawazi kuliko sisi wengine.

waachwe tu ili wengine nao wajifunze. adhabu alipewa ndogo sana faini ya 900,000 au miaka miwili jela? huu is uhuni tu wa huyo hakimu. hawa watu wanatakiwa wafungwe kifungo kikubwa na kama ni faini iwe kubwa. madawa ya kulevya ni janga la kujitakia hata shetani tusimsingizie hili.
 
Kila anaetumia haya madawa huishia kifo cha mateso na aibu, ajabu ni kwamba wasanii wanafukuzana kuyatumia na wote wanaotumia wana akili timamu hii inanishangaza sana, Aisha madinda R.I.P ulikuwa mkali sana.
 
Unga mtamu. Kuuanza kuna udora wake na kuuacha kuna tabu yake. Nawafahamu watu wengi waliopotea kwa cocaine na heroine. SAD!
 
".....kama .... na sikinde, mimi ndo nilimshawishi mamako ili uimbe....." Prof jay

"......get of my shoulder ngoma inavuka boda, waoga check mnalewa mpk soda....."
 
Unajua suala la dawa za kulevya lina chukuliwa kama siasa, inatakiwa sheria iende mbali zaidi ya hapa ilipo kiasi kwamba anayepatikana akivuta au akitumia dawa za kulevya isivyo halali nae aadhibiwe. Yawezekana hilo ombwe limewekwa makusudi ili kuendeleza utumiaji wa dawa za kulevya. Kwani kwa hivi sasa hata mtu akikutwa analewa au kutmia dawa za kulevya isivyo halali inaonekana ni kitu cha kawaida ila kukiwa na sheria inayofika mpaka kwa mtumiaji sidhani kama watu watajitokeza hadharani ili tuwahurumie.
 
kuna ngudu pub ya mama yake ataenda kuhudumu pale
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…