Mbunge Saashisha Mafuwe aishauri Wizara ya Ujenzi Iwe na Mkakati wa Kudhibiti Barabara Zijengwe kwa Kiwango Kinachostahili Ili Kupunguza Matengenezo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189

MBUNGE SAASHISHA MAFUWE Aishauri Wizara ya Ujenzi Iwe na Mkakati wa Kudhibiti Barabara Zijengwe kwa Kiwango Kinachostahili Ili Kupunguza Matengenezo ya Mara kwa Mara

"Jumapili ya tarehe 26 Mei, 2024 nilikuwa na mkutano wa hadhara katika Kata ya Weruweru na wananchi wakaniambia Mhe. Mbunge kwa kazi kubwa alizofanya Mheshimiwa Rais kila ukisimama hata kama ni kuuliza swali anza kwanza kumshukuru Rais, na mimi namshukuru Mheshimiwa Rais kwa miradi mingi aliyofanya nchini na miradi kedekede katika Jimbo la Hai ambayo kihistoria haijawahi kutokea" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai

"Waziri wa Ujenzi ulitusaidia fedha tukajenga daraja la Msomari lililokuwa linasumbua sana lakini naomba mfanye utafiti chanzo cha maji yanatokea wapi kwasababu mafuriko yaliyokuja yalivuka daraja"

"Nakushukuru Waziri wa Ujenzi kwa fedha ulizotuletea tunajenga daraja la Makoa na kazi inaendelea vizuri. Mmeleta fedha Mkandarasi ameshapatikana kwaajili ya ujenzi wa daraja la Kikafu kwa Barabara ya Kalali - Uswaa. Naomba daraja la zamani lisivunjwe ila liendelee kuwepo"

"Naomba Barabara ya Kwa Sadala - Kware (KM 15) imeshafanyiwa Visibility Study, ni ya muhimu sana maana inaleta chakula soko la Kwa Sadala na kutoka Kwa Sadala - Longoi (KM 17). Barabara ya Machame - Kiaria na Barabara ya Bomang'ombe hazina taa, tunaomba tuwekewe taa za Barabarani"

"Barabara ya Bomang'ombe - Chekimaji - TPC, TARURA wametuwekea KM 3 lakini hii Barabara ina hadhi ya kimkoa, kaeni na TANROAD ili Barabara ikengwe kwa kiwango cha lami"

"Tuna madeni tunawadai ya fidia, Barabara ya Mashinetuz - Kiaria tangu mwaka 2017 wananchi waliwekewa alama X lakini hawajalipwa au kuambiwa waendelee kuitumia Barabara. Tunaomba tujue moja, Barabara tuendelee kutumia au mtatulipa fidia maana watu wamebaki hawaelewi kinachoendelea. Na pia daraja la Kikafu"

"Tulipitisha kwenye kikao cha RCC kupandisha hadhi Barabara za vijiji kwenda TARURA na Barabara za TARURA kwenda TANROAD. Naomba Waziri wa Ujenzi ukihitimisha hotuba yako hapa tupate majibu"

"Mfuko wa Barabara umeweza kukarabati Barabara kwa asilimia 40.8 tu lakini mkakati mlioweka ili mfuko uwe na nguvu ni kubadirisha Sheria, mimi sioni kama mkakati huu utatufikisha mahali"

"Kwanini tunatengeneza sana Barabara? Mmefanya matengenezo ya Barabara KM 34,383.67 n Barabara maalum KM 3600+. Kwanini matengenezo ni mengi? Jibu ni rahisi, Barabara zinajengwa chini ya kiwango (Below Standard) ndiyo maana kuna matengenezo mengi sana na fedha za matengenezo ni nyingi sana"

"Mkakati uwe ni kudhibiti, Barabara zitengenezwe kwa kiwango kinachotakiwa ili zidumu muda mrefu. Barabara zijengwe kwa kiwango kinachostahili ili kupunguza gharama za matengenezo" - Mhe. Saashisha Mafuwe, Mbunge wa Jimbo la Hai

"Nauliza, kwanini TBA tunawapa ruzuku ya Serikali wakati wanafanya kazi kama Wakandarasi wengine. Kama TBA anapewa ruzuku basi na Wakandarasi watanzania mnaotaka kuwainua wajengeeni uwezo, wapeni ruzuku kwa kuwapa vifaa kwa bei nafuu ili wawe na uwezo wa kufanya kazi"
 
Katika taifa ambalo njia zake zinajengwa chini ya kiwango ni Tanganyika. Na wala viongozi hawajali kabisaa. Njia MPYA baada ya miezi 9 haifai full mashimo tu!!





KAZI ni kipimo cha UTU
 
Back
Top Bottom