Mbunge Nancy Nyalusi Awapiga Jeki UWT Iringa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,581
1,189
MHE. NANCY NYALUSI ACHANGIA MILIONI 6 UJENZI WA NYUMBA YA KATIBU UWT, ATOA KADI 1500 KWA WANACHAMA WAPYA WA CCM

MBUNGE wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Mhe. Nancy Nyalusi amenunua Kadi za uanachama 1,500 kwa ajili ya wanachama wapya wa Jumuiya ya Wanawake CCM (UWT) Wilaya ya Kilolo, Mufindi na Iringa Mjini

Mhe. Nancy Nyalusi amechangia Saruji Mifuko 300 yenye thamani ya Shilingi Milioni 6 ili kusaidia juhudi za ujenzi wa nyumba ya Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) Iringa Mjini, Kilolo na Mufindi huku kila Wilaya ikipata Mifuko 100 ya Saruji (Milioni 2)

Mhe. Nyalusi amefanya hayo mnamo tarehe 5 Julai, 2023 akiwa ziarani Wilaya ya wakati wa Kikao cha Kikanuni cha Baraza la Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilayani humo.

Aidha, Mhe. Nancy Nyalusi amewakumbusha wanachama wa jumuiya ya UWT kutambua juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya 6 katika kuboresha Maisha ya wananchi kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo na kueneza mazuri hayo yanayofanywa na Serikali.
WhatsApp Image 2023-07-06 at 08.28.03.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-06 at 08.28.04.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-06 at 08.28.50.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-06 at 08.28.50(1).jpeg
 
Back
Top Bottom