Mbunge Cherehani Akabidhi Mabati 120 Jumuiya ya Wazazi Kahama

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
2,584
1,189
Mbunge wa Jimbo la Ushetu Mhe. Emmanuel Cherehani amekabidhi Mabati 120 (geji 30 msauzi) katika nyumba ya Mtumishi wa Jumuiya ya Wazazi wilaya ya Kahama kama alivyoahidi hapo nyuma.​

Akizungumza wakati wa kukadhiwa mabati hayo Mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi CCM Taifa Fadhili Maganya amempongeza Mbunge huyo kwa kuwa mstari wa mbelel kuchangia Maendeleo ya Chama huku akiwaomba wadau na Viongozi kuwa na moyo wa kujitolea shughuli mbalimbali za kimaendeleo ndani na nje ya Chama.

Aidha, Maganya amesema wao kama Jumuiya ya Wazazi watatoa mbao zote zitakazohitajika kuezeka nyumba hiyo.

Awali akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa mradi huo Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM mkoa wa Shinyanga, Bi. Regina Ndulu amesema mpaka kufikia hatua hiyo ya upauaji wameungwa mkono na watu mbalimbali Wakiwemo Mbunge wa Jimbo la Msalala Mhe. Idd Kassim ambaye alichangia tofali 1,000 na Mbunge wa Kahama Mjini Mhe.Jumanne Kishimba tofali 500.

Utakumbuka Mwezi Julai 16, 2023 Mbunge Cherehani aliahidi kutoa mabati ya kuezeka nyumba hiyo kupitia kikao cha Jumuiya ya Wazazi Wilayani humo.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.41.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.41.jpeg
    36.1 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.40.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.40.jpeg
    42.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.41(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.41(1).jpeg
    56.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.42.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.42.jpeg
    38 KB · Views: 1
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.42(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.42(1).jpeg
    32.3 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.43.jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.43.jpeg
    35.5 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.43(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-02-29 at 00.12.43(1).jpeg
    39 KB · Views: 2
Wao wafanye ila wasisahau kutatua huduma muhimu kwa wananchi ndo tulichowatuma!.
 
Back
Top Bottom