Kingmairo
JF-Expert Member
- Apr 7, 2012
- 4,936
- 3,542
Unapoint lakini umeandika kama hujui siasa halisi zilivyo. Hizo outcome hazitafikiwa na upinzani chini ya mazingira yaliyopo. Nguvu kubwa wanatakiwa watumie kupigania "equal playing ground." Kwasasa hivi battle ni upinzani against (ccm+serikali+polisi+tume ya uchaguzi+jeshi). Haitakuja tokea wakachukua nchi kwa mazingira haya.Watu wengi tuna kawaida ya kujisifu kwa kuangalia matokeo na kusema nimejitahidi sana, nimeweza kufika mahali ambapo sikufika mwaka jana etc.
Ifike mahali tuyaweke malengo yetu wazi, mfano tunataka kuwa na bunge 50% 50% uchaguzi wa 2020, au tunataka kushinda uchaguzi wa rais, na ikifikia tusifanikiwe iangaliwe tatizo ni nini ili kama kuna kuwajibishana ifanyike hivyo.
Ila kwa jinsi tunavyoenda utashangaa kila mwaka sisi ni chama kikuu cha upinzani na bado tutakuwa tunapongezana. Tuweke malengo, watu wawe responsible kwa malengo yaliyowekwa kabla na si kuanza kusifiana baada ya matokeo ambayo hatuna uhakika kama ndo lilikuwa lengo letu au zuga.