Sijajua kinachokushangaza ni nini wakati kila mtu anajua CCM inatumia mbinu za upinzani wakati wa kuomba kura hadi sasa wakati wa utekelezaji. Waliiba sera ya CUF miaka ya nyuma kufuta kodi ya kichwa ilihali walishatuaminisha kabla kuwa wale wote wanaoleta sera za kufuta kodi hawajui wasemalo.
CCM waliiba sera ya upinzani kufuta ada za shule. Mwaka 2010 sera hii ilihubirwa sana na Dr Slaa na CCM ya Magufuli wakatuaminisha kuwa haiwezekani elimu iwe bure, leo wote wenye akili mnaona CCM hao hao wameahidi kufuta ada hadi form 4. Yaani miaka 5 iliyopita walisema haiwezekani elimu iwe bure, leo wanasema inawezekana.
Sera ya kubana matumizi ni wimbo wa miaka yote wa Chadema, kuanzia kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali, kufuta safari zisizo za maana kwa viongozi, kufuta vyeo visivyo na tija au vinavyoshabihiana n.k. Magufuli anafanya haya haya.
Kinachozungumzwa kuhusu mabadiliko ndio hiki hiki kinachofanywa sasa hivi, Magufuli anajaribu kuhuisha utendaji dhaifu wa serkalini na taasisi zake, kuleta uwajibikaji na kupambana na rushwa. Rushwa hii imekuzwa na mfumo CCM na Chadema walisema wataondoa mfumo mbovu uliopo ili kuleta mfumo bora zaidi
Kwa ujumla nadhani wewe huzijui vzr sera za Chadema, unasilikiliza maneno ya kwenye vikao vya kahawa na maskani ndio unataka kuaminisha watu hizo ndio sera za Chadema