Mbowe atoa kauli juu ya kauli ya Rais Magufuli

Majambazi yanyang'anywe bunduki 'haraka haraka'

Magari yatakayo kamatwa kwenye barabara ya mwendo kasi yatolewe matairi

wanasheria watakao watetea wahalifu waswekwe rumande.

Kauli hz ni hatari, hv tunasubiri nn kupaza sauti? Tumuunge mkono mhe Mbowe kukemea kauli hz.
 
Katika hili nampongeza Freeman Mbowe ameongea ukweli.
Kumruhusu Rais kuendelea kutoa matamko ambayo ni kinyume cha sheria ni jambo la hatari sana katika kujenga utawala bora na utawala wa kidemokrasia"!
Huyo Tapeli Mbowe hukumbuki matamko yake aliyowahi kuyatoa na kisha kuwageuzeni midoli!?
1.Wezi wa kuku wanachomwa moto Wakati mwizi Lowasa anazunguka na fomu za urais.
2.Kumpokea Lowasa chadema, "Over my dead body", Sasa sijui siku hizi tumwite marehemu or?
Na mengine mengi ya ajabuajabu!
 
Huyo Tapeli Mbowe hukumbuki matamko yake aliyowahi kuyatoa na kisha kuwageuzeni midoli!?
1.Wezi wa kuku wanachomwa moto Wakati mwizi Lowasa anazunguka na fomu za urais.
2.Kumpokea Lowasa chadema, "Over my dead body", Sasa sijui siku hizi tumwite marehemu or?
Na mengine mengi ya ajabuajabu!
Mwambieni raisi anatakiwa kuheshimu katiba ambayo aliapa nayo hii nchi inaongozwa kwa kufuata katiba siyo matamko yake.
 
Wale wa BIG RESULT NOW yaan BRN

Haon jinsi katiba inavyohujumiwa na kuvunjwa.

Uhuru wa habari.......chali

Uhuru wa mikusanyiko hususan vyama vya siasa.....chali

Bunge la jamhuli linapanga bajeti feki.....inayotumika ni ile ya magogoni

Vyombo vya habari....vimepigwa kufuri

Mahakama nikufunga wapinzani.....ccm wanakatiba yao

nknknk
 
Mbowe hana muda wa kuondoa ufisadi,dhuruma na maovu ktk jamii maana yeye mwenyewe si msafi,mmoja wa wakwepa kodi wakubwa kwa kisingizio cha masuala ya kisiasa, Mbowe angekuwa mtii ktk katiba basi asingefanya utapeli ktk katiba ya chadema kwa kuondoa kwa makusudi vipengele ndani ya katiba iliyopitishwa na wanachama na kujipa uenyekiti wa kudumu wa chama,chadema ni kichaka cha waovu hawatuelezi lolote watanzania kwa sasa maana tulishawabaini ghiriba zao za kutaka tuwape ridhaa ya nchi ili watuibie na kutuacha masikini wa kutupwa..!!
 
Mambo mengine tukiweka siasa pembeni tutaiongoza nchi yetu ktk njia iliyo njema!!

1)Rais kusimama hadharani tena siku ya Sheria Tz,kwa macho makavu akiwaangalia majaji na kuwaambia kuwa kuna kesi za madai ya serikali,ambapo serikali ikishinda inaenda kupata karibu trilioni 07.
Akawasisitiza majaji wazihukumu hizi kesi harakaharaka maana ni toka mwaka 2005.Na katika hizo pesa zitakazopatikana,basi zitatumika kuimarisha maslahi ya Idara ya Mahakama.

2)Rais kama kiongozi wa muhimili mwingine,usiopaswa kuingilia muhimili wa Mahakama,anashangaa kwanini kuna Majaji ambao toka wameanza kuhukumu kesi ambazo serikali inashitakiwa,katika hukumu ya kesi hizo,serikali haijawahi kushinda.Rais anauliza hadharani...."Kweli hawa majaji kila siku ktk kesi wanazohumu serikali inashindwa?"

3)Rais ambaye kisiasa ni mwanachama wa chama cha siasa na pia mwenyekiti wa chama dola,anasema hadharani kuwa Tanganyika Law Soceity imekuwa kama chama cha siasa,sababu inakosoa sana serikali.Mwenyekiti huyu wa chama dola anasema kwa sasa amepata "taarifa za siri" kuwa wagombea wa TLS sio wafuasi wa chama chake,bali ni wa chama kingine cha siasa,hivyo kaahidi...Uongozi huo mpya wa TLS ukiingia madarakani,hata akipelekewa majina ili awachague wawe majaji au viongozi ktk serikali basi hawachagua ng'oooooo!!

4)Hii ina maana kubwa sana ktk utawala wa Sheria!Unapokuwa mbele ya Majaji na Mawakili,na unapigiaa chapuo kuwa mawakili wanaotetea wahalifu wenye kesi dhidi ya serikali nao wafungwe

5)Unapokuwa Raisa,halafu unasema akikamatwa mtu na ushahidi hakuna haja ya kufuata "procedures" ni mtu kufungwa tu...Hili ni tatizo

Rais naye ni binadamu,siyo malaika...Tuache akosolewe ili ajue alipokosea
 
Tatizo la mbowe ni mhalifu sugu,kodi halipi yaani ni kama vile siyo mtanzania mwenzetu,ni mbinafsi hatari!!!so hatetei mtu ila anajitetea mwenyewe anakwepa kodi mpaka jimboni kwake.Mbowe kiboko.
 
Watanzania tunawoga sio aman mnadanganywa

Usalama akimuua RAIA (konda daladala)
Ni vita ndan kwa ndani

Spendagi ujinga.
 
Wakati mwingine michango ya humu :( inatupa picha kubwa sana ya namna elimu yetu inavyotutayarisha kama mazuzu tusioweza kuhoji. Wakubwa wakisema jambo hata wanataaluma husika wanahangaika kulitetea hata kama ni la kijinga.
 
1) ...
JIBU: Magufuli ameshavunja sheria nyingi tu hata ya vyama vya siasa ameivunja kwa kukataza shughuli za kisiasa hasa mikutano ya hadhara wakti ni jambo la haki kwa vyama vyote hapa tanzania kwa mujibu wa sheria hiyo.

JIBU 2:... anachotaka mbowe ni viongozi wote lets say raia wote waheshim matakwa ya katiba bila kujali post yako maana hakuna aliye juu ya sheria

2) JIBU...ssa kma mtu kaua out of self defense atatetewa wapi?? Eti hapo katiba itafuatwa??

3) JIBU:
KATIBA NA SHERIA ZILIZOPO ZIFUATWE NA WOTE NA ZISIMAMIWE KIUFANISI ZAIDI

4) JIBU:
TAMKO LIPI LA MBOWE LIMEVUNJA KATIBA YA NCHI??
Mbowe ni kiongozi wa chama cha siasa ambacho sio kila mtanzania ni mwanachama wake so haina impact kwa taifa kma taifa kwa ujumla wake...
Pia mbowe ni mjumbe tu sasa kwanni usijibu hoja zake unamlenga mtoa hoja?? Character assasinatiom hazisaidii mkuu jibu hoja sio mtu alieileta hoja

zitto junior: hakika majibu yako hayo ndiyo yanampa uhalali wa Rais Magufuli kutoa matamko hayo mnayodai yanavunja Katiba.

Katiba inampa Rais madaraka ya kuisimamia. Na vifungu vingi katika Katiba vinampa madaraka kulinda haki na maslahi ya wengi.

Mimi si mwanasheria ila upeo nilionao naheshimu Katiba ya JMT, km Ibara ya 35 inahusu 'Utekelezaji wa shughuli za Serikali Sheria ya 1984 Na. 15 ib.9, kifungu kidogo (1 na 2).
"(1) Shughuli zote za utendaji za Jamhuri ya Muungano zitatekelezwa na watumishi wa Serikali kwa niaba ya Rais".
"(2) Amri na maagizo mengine yanayotolewa kwa madhumuni ya ibara hii yatathibitishwa kwa namna itakavyoelezwa katika kanuni zilizowekwa na Rais, kwa kuzingatia masharti ya Katiba hii".

Wewe na wenye mawazo kama yako, mnadai 'amri na maagizo' anayotoa Rais kikatiba ni matamko! Du, mnataka nchi isitawalike!
 
Leo 4/2/17 Gazeti la Mwananchi lenye habari yenye kichwa "Kauli ya JPM yaibua mjadala mzito".

Habari yenyewe ni kauli ya Rais kuhusu watu wanaowatetea wahalifu na kwamba Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeingiliwa kisiasa.

Wanasheria wanaoingiza siasa kwenye chama hicho wanataka kigeuzwe kuwa na mtazamo wa kisiasa ili kiweze kupambana na Serikali, kwa kisingizio cha ati kulinda Katiba ya JMT. Kuna wanasheria wanaongoza jambo hilo na wanaandaa kufanya mapinduzi katika uongozi wa Chama.

Hayo nawaachia wanachama wenyewe wa TLS, maana Rais amelibainisha hilo na hakusita kulikemea na kutoa maagizo lichunguzwe.

Lakini, mada yangu ni kuhusu neno la Mh Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, M/kiti wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani, mtetezi mkuu wa mabadiliko, yakilenga kuondoa ufisadi, dhuruma na maovu katika jamii!!!!

Mh Mbowe amenukuliwa katika hilo Gazeti kuwa kasema "Kumruhusu Rais kuendelea kutoa matamko ambayo ni kinyume cha sheria ni jambo la hatari sana katika kujenga utawala bora na utawala wa kidemokrasia"!

Maswali yafuatayo nayaelekeza kwake Mh Mbowe (naamini anasoma ya JF) na wapambe wake:
1) Hivi ni kweli Rais Magufuli anatoa matamko na hayo matamko ni kinyume cha sheria?
i) Ni sheria zipi zinavunjwa?
ii) Ni demokrasia gani Mh Mbowe abaizungumzia? Naamini si inayowapa wachache kuamua hatima ya haki katika jamii!!!

2) Rais kama Kiongozi na Amri Jeshi Mkuu, anapaswa kutoa matamko gani, wakati wanaopaswa kulinda, kutetea na kutoa haki, hawafanyi hivyo ipasavyo? Arejee kisa cha mjane alitejitokeza kwenye huo mkutano.

3) Mh Mbowe, ni njia na jinsi gani ya kushughulikia maovu, pamoja na kwamba kuna vyombo na taasisi zenye dhamana hiyo?

4) Mh Mbowe, je, unakumbuka matamko ambayo umekwisha kuyatoa yenye kukanganya na kufitinisha jamii?


HAKUNA MTU MWOVU KAMA MNAFIKI NA HASA AKIWA KIONGOZI WA NGAZI KAMA MH MBOWE.

Hongera Rais Magufuli kwa ujasiri wa kuwakemea hadharani watu wanaojifanya wako juu ya sheria. Kauli zako siyo zinalinda haki za wanyonge, ambazo zinachezewa na vyombo vilivyopo kikatiba, pia zinawapa changamoto wahusika katika vyombo hivyo.

Tatizo umejikita kwenye kumuandama Mbowe badala ya kuhoji juu ya hoja...Na ndio maana hujaweka hata nusu ya hizo kauli ambazo Mbowe amezingumzia coz ulikuwa na lengo la kuonesha ubaya wa Mbowe Tu, Ili sisi tumjadili Mbowe..??? This is foolishness.

Sasa sisi tutajadili nini kama hizo kauli hujaziweka??
 
Tatizo umejikita kwenye kumuandama Mbowe badala ya kuhoji juu ya hoja...Na ndio maana hujaweka hata nusu ya hizo kauli ambazo Mbowe amezingumzia coz ulikuwa na lengo la kuonesha ubaya wa Mbowe Tu, Ili sisi tumjadili Mbowe..??? This is foolishness.

Sasa sisi tutajadili nini kama hizo kauli hujaziweka??
Kama hukunielewa nisamehe.
 
"...some People will always be comfortable to be ruled anyhow, not because they like it but they have given away the sense of humanity..."

Nelson Mandela
Haya maneno yamfikie mleta mada popote pale alipo ndani au nje ya mipaka ya Tanzania.
 
Jamii forums imegeuka sehemu ya watu kuja kudhihirisha ujinga wao!

Mtu na akili zake timamu kabisa hata kama hakusoma sheria eti anashindwa kuona ni kwa kiasi gani kauli za rais zilivyo na ukakasi katika nchi inayofuata misingi ya kisheria!
 
Back
Top Bottom