Msomi Livelu

Member
Jun 21, 2024
24
30
Watanzania tulio wengi tunataka maendeleo ya viwanda ktk nchi yetu. Wakati huo huo tunailalamikia bidhaa kupanda bei.

Mimi sikutegemea malalamiko ya bidhaa kupanda Bei kwa muda huu ambapo tunahangaika kufufua viwanda.

Kwa mtazamo wangu kwa hatua hii ya awali ya kuendeleza sekta ya viwanda, gharama ya uzalishaji itakuwa kubwa na uzalishaji utakuwa mdogo wakati mahitaji ni makubwa, hivyo bei lazima iwe kubwa. Lakini pia ukubwa wa faida kwa sector ya viwanda itachochea viwanda vingi zaidi na kusisimua uzalishaji, hivyo kuwa na faida ya bei kushuka na ajira kuzaliwa.

Lakini Kama tunataka bidhaa ziwe Bei poa basi serikali kwa mtazamo wangu inatakiwa iwaache huru waagizaji wa bidhaa na sio kuchagua muuza vocha au asie muuza vocha alimradi tu mwenye uwezo basi na alete, hapo Bei itapoa, Ila tusitegemee kukuwa kwa viwanda vya ndani hapo.
Watanzania hatujui muda gani tulie, hatuna subira.

Hakuna nchi iliyoendelea bila kupitia maumivu Fulani, Tena makubwa. Tunataka miradi mikubwa ila hatutaki Kodi na hatutaki serikali ikope. Na muda huo huo tunataka shilngi iwe juu ya dolar. Daaa ! Hii ni confusion kubwa.

Ila tatizo nililoliona Mimi ni watu wengi tunatazama kila Jambo Kama fursa ya kisiasa.

Watu wa vyama mbadala wanailazimisha serikali kufanya maamuzi based on political advantage.

Ujumbe kwa serikali, kwenye Safari ya maendeleo vilio vitakuwa vingi, lazima tujifunze kuishi na vilio hivyo Ila visitufanye kurudi nyumba, vitusaidie tu kuona namna ya kusonga mbele.

Angalia Agricultural revolution in Europe, Industrialization in Europe. Maendeleo ya China na nchi zote tuzoziona zimepiga hatua, kumekuwa na kelele nyingi na even Vita Kali baina ya makundi yenye mitazamo tofauti.

Kwenye uchumi huwezi kumnufaisha kila mtu. Unapomnufaisha Juma lazima John aumie, na kinyume chake ni hivyo hivyo.
 
Sasa si uishauri pia serikali kutengeneza mazingira bora na rafiki kwa wazalishaji wa ndani ili uzalishaji usitumie gharama kubwa!!

Mfano kupunguza/kuondoa kodi na tozo mbalimbali kwa wazalishaji, kupunguza bei ya umeme, nk!
 
Sasa si uishauri pia serikali kutengeneza mazingira bora na rafiki kwa wazalishaji wa ndani ili uzalishaji usitumie gharama kubwa!!

Mfano kupunguza/kuondoa kodi na tozo mbalimbali kwa wazalishaji, kupunguza bei ya umeme, nk!
Kuna wakati kwenye kipindi Cha Jakaya alifanya hivyo kwenye kiwanda Cha kuzalisha cement Dangote, cement ikafika 8000. Baadae wakaja watu na kulaumu kuwa Dangote halipi Kodi. Ikawekwa Kodi kubwa na cement ikapanda Bei. Na hao hao wakalalamika cement kupanda bei. Sasa kipi ni kipi?
 
Kama zipi.
yaani kwa mfano mimi nipo hapa tarime mkate wa kenya ni 1000
nijilazimishe ninunue wa tz kwa 1500 why
cement from kenya 14000, niachane nayo ninunue ya tanga cement 22,000
si ndo unavyotaka hivo?
sukari ya kenya 2500, niachane nayo ninunue ya tz 3500
 
Back
Top Bottom