Mawaziri Watakaolalamikia OC Ndogo!, Waache Kazi!. Ni Kauli ya Kujenga Nidhamu au Udikiteta Tuu?!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,669
119,282
Wanabodi,

Nimewahi kuzungumzia baadhi ya kauli za rais wetu Mhe. Dr. John Pombe Magufuli kuwa ni kauli za vitisho, kibabe na kidikiteta, ambapo kauli ya leo ni hii ya kuwatisha baadhi ya mawaziri na makatibu watakaosika kulalamikia fedha za ndogo za OC (other charges) zinazopelekwa kwenye wizara zao ni ndogo na hazitoshi!, amewaambia wale wotewanaoona fedha wanazopewa ni ndogo na haziwatoshi, waache kazi!, amesema kuna watu wanalalamika!, anasema ametuma 'watu' wawarekodi walalamika hao, akipata tuu ushahidi, kuwa ni kweli wanalalamika, then atawatimua kazi!.

Hili limekaaje?!. Hii sio kauli ya vitisho, kuwa watendaji hawa wakuu?!, yaani kiasi chochote watakachopewa na serikali, no matter ni kidogo kiasi gani, hawaruhusiwi kucomment chochote bali wapokee na kunyamaza kimya!.

Huku si ni kuwafunga midomo mawaziri na makatibu wakuu wao?!, kitendo cha rais kesema amewatumia 'watu' wawarekodi, ni uthibitishoa usiotia shaka kuwa freedom of "expression is at crossroad!". Hii inaitwa suppressing opinion za mawaziri, makatibu wakuu na watendaji wakuu, ambazo ndizo hatua za awali za viongozi wote madikiteta duniani, hutoa kauli za kuwafanya waogopwe!. Ukiona mwenzako ananyolewa, wewe anza kutia maji tia maji, stage ya pili haiwezi kuwa ni kwenye media?!.

Tanzania yetu hii kusema ukweli madudu yalizidi, kiasi kwamba tukafika mahali nchi yetu ilihitaji kiongozi mwenye traits za udikiteta ili mambo yaende!. Mungu kasikia kilio cha Watanzania, katupatia rais Dr. John Pombe Magufuli, ambaye ni benevolent dictator, Watanzania tupewe nini tena?!.

Paskali
 
Asante kwa taarifa ya marudio,alishasema JK kuwa ametipatia rais dikteta
 
Taifa la watu milioni 50 leo linaendeshwa na akili za mtu mmoja
na wasio ridhika hawatakiwi hata kusema tu

Ndo maana wenzetu nchi zilizoendelea walishaliona hili
hatari za kuendeshwa na mtu mmoja

wakaweka mfumo wa kuhakikisha mawazo ya mtu mmoja peke yake hayaendeshi nchi
 
Ndiyo
Hata kama ni mimi nakutimua kazi straight forward. Kwanini ulalamike.
Wanachotakiwa kufanya ni kulalamika kwa vigezo na nyenzo ya kwamba peleka mchanganuo sahihi umekusanya kiasi gani na kukiweka ktk treasury kisha toa mchanganuo unahitaji nini na kiasi gani na kwanini. Kulalamika chichini ama ku criticize bila solution hata mie nakutimua straight away.

Hao jamaa wako hapo kutoa solutions, change challenges into opportunities, sasa wanapoungana na walalamikaji, no time to hit the bush around., hit them instead.
 
...ukichukulia wazungu wameamua kubana fedha zao,halafu nyie mawaziri mnaleta mdomo pesa hazitoshi,mnadhani hizo pesa za kuwatosheleza zitatoka wapi?,hakuna namna,lazima amri itolewe,nadhani anafanya hivyo sio kwa kupenda,ila inabidi!
 
Strange, Pasco unasimamia wapi, Magufuli amefifisha akili za watu.Rudia usome halafu uone umehitimishaje. Nasema tulipofika na Umungu wa Mtukufu, tunakwenda kubaya
 
Wanatakiwa walalamike kwenye cabinet, waziri kulalamika nje ya cabinet inakuwa si halali. Budget hupita kwenye cabinet kabla haijaenda bungeni na hivyo mawaziri wote hutakiwa kuuunga mkono budget katika kile kinachoitwa collective responsibility.
 
Tatizo moja watu hawawezi kwenda na speed ya Magufuli hilo ndiyo tatizo na kasema kabisa "Msidhani hii ni trend ya awamu ya 4 kma huwezi acha kazi na wapo wasomi kibao hawana kazi watakaimu hizo nafasi! Udikteta wa Kagame ndiyo ulipowafikisha Warwanda hapo walipo na wametuacha kwa mbali sana kila nyanja! tuache kulalamika tufanye kazi
 
Mbona vile Chama Chenu chakavu kimekuwa kinaendeshwa na akili ya mtu na Mkwewe toka kianzishwe.....na sasa hivi kinaendeshwa na AKILI YA MTU MMOJA Aliyekinunua kwa PESA MINGI..... unaliona hilo!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…