Mawaziri wanapolalamikia fedha hazitoshi wasipuuzwe, wapo watu wanateseka

Sasa mthubutu kulalamika tuwasikie na ole wenu sauti zenu zinaswe na recorders zetu.
Na kuna wale mawaziri na viongozi wa serikali wenye IDs fake humu JF wanajifanya kuibua na kuipa changamoto serikali kupitia ID hizo feki.
Nazo tutazifuatilia kwa karibu kuanzia sasa.
 
Kama hela hazitoshi waachie nafasi zao upesi tena haraka.
Kuna mtu aliniambia kuwa Rwanda ukipewa bajeti unaulizwa unadhani kwa bajeti hii utaweza kutimiza majukumu yako? ukisema kwa bajeti hii siwezi,unaambiwa ondoka Kagame anatafuta mtu mwingine atakayeweza.
Ukisema mimi nitaweza basi bajeti ikipita unapewa bajeti unaenda kusimama mbele ya jaji wa mahakama kuu na kuapa mbele yake kuwa utatekeleza hizo kazi kwa hiyo bajeti iliyopo na kusainishwa performance contract na jaji.Ukishindwa wakati wa utekelezaji utakiona cha mtema kuni.

Sasa kama bajeti ndogo mtu anashupalia kubaki kazini kwa ajili ya nini ondoka andika barua ya kuacha.Mwambie wazi raisi kwa resources hizi siwezi tekeleza majukumu mpe kazi hii mtu mwingine.

Bajeti ikiwa ndogo rekebisha matumizi.Badala ya mkuu wa idara kuja na shangingi kazini kapande daladala.Huwezi kubaki na matumizi yale yale uliyozoea wakati pesa ni ndogo.Hivi MAGUFULI akisema anabana matumizi huko kwingine wanaelewa au hawaelewi?
wao pia wanatakiwa wabane matumizi

HAPA KAZI TU
mkuu umenichekesha sana hapo pa kuacha shangingi na kwenda kupanda daladala. kwa utawala huu wa magu hao wadekaji hakuna rangi watakayoacha kuiona. Kikwete aliwazoesha vibaya sana. acha kwanza waisome number.
 
Mtu asiyejua, akikusoma hapa ataona umeongelea kitu unachokijua, lakini akisoma anayejua ataona umepotoka. OC ni matumizi ya kawaida ya kuendeshea ofisi. Kulipia maji, umeme, stationry na matumizi mengine yasiyokuwa mishahara au maendeleo. Siyo kweli kwamba pesa za kulipia pango la nyumba ya ofisi hazikuwekwa, ziliwekwa na kupitishwa na Bunge isipokuwa hazikuletwa kama ilivyotarajiwa.

Hapa nipo manung'uniko yanapoanzia. Hajasema mishahara inalipwa kupitia OC, bali mishahara nayo huchelewa kuletwa kutoka fungu la mishahara. Kisa ni nakshi fedha hazijatolewa. Vibali vya kuajiri vinatolewa baada ya bajeti kupitishwa, wizara zinaajiri lakini mishahara ya waajiriwa waya haipo, fedha hakuna. Unatoaje kibali pasipo kuwa na fungu? Mimi nadhni bora kutuliza akili kabla ya kuwalalamikia Mawaziri wanaolalamika.

Muhimu ni kuangalia tatizo linaanzia wapi, kumlaumu mlalamikaji bila kuangalia uhalisia wa malalamiko ni kujidanganya wenyewe kwa sababu kumzuia anayelalamika hakutaondoa shida iliyopo isipokuwa ni kumsikilia kumwelewa na kutafuta suluhu ' lisemwalo lipo kama halipo laja' Magufuli kuwa Rais wa Tanzania siyo ndiyo kujua kila kitu. Hata kama ana vyombo vya kumsadia, kuwa na chombo ni jambo moja kutumia chombo ni jambo lingine si kila mwenye silaha ana shabaha
Mkuu acha uongo. Hakuna anaechelewa kupata mshahara serikalin. Kila mtu anapata on time mshahara wake. Kama hukubajet ajira mpya halafu leo unataka ku ajir kwa kutumia oc we hufai apo ulipo. Umekosa mipango na unaitukanisha serikali. Unapaswa kuwapisha wenye uwezo.
Lakini malalamiko ya Mawaziri ni kuhusu oc. Wanataka hela ikae pale ili waile wanavotaka bila kuulizwa. Hawajasema wizara hazina hela au hela zinachelewa. Wala Hawajasema mishahara haitosh. Au Hawajasema hawapewi siting allowance. Hawajasema hela wanayopata haiwatoshi. Ila wamesema hela haitoshi kwenye oc. Wao wanataka hela nyingi kwenye oc. Oc oc oc oc. Wao ni oc tu.
 
Sasa mthubutu kulalamika tuwasikie na ole wenu sauti zenu zinaswe na recorders zetu.
Na kuna wale mawaziri na viongozi wa serikali wenye IDs fake humu JF wanajifanya kuibua na kuipa changamoto serikali kupitia ID hizo feki.
Nazo tutazifuatilia kwa karibu kuanzia sasa.
mkuu kumbe tuko wengi humu. Huko kitengo gani? Tayari mimi nimewanasa 10 nilitumia tu siku moja Tayari nimewatuma vijana wangu Rama na Frenki
 
Sasa mthubutu kulalamika tuwasikie na ole wenu sauti zenu zinaswe na recorders zetu.
Na kuna wale mawaziri na viongozi wa serikali wenye IDs fake humu JF wanajifanya kuibua na kuipa changamoto serikali kupitia ID hizo feki.
Nazo tutazifuatilia kwa karibu kuanzia sasa.
naona unapiga bonge la kwara. du! usije ukawa miongoni mwa wale vijana 50 wa mtandao ambao Kikwete aliowataja mkumbukwe na utawala wa magu pale uwanja wa namfua singida kwenye sherehe za kuzaliwa ccm.
 
Hao wanaolalamika wamefikia hatua ya kukosa hata mahitaji muhimu, mfano fedha ya kujikimu ya mtumishi unaibanaje? Karatasi za ream unabanaje matumizi?
Nikusaidie kidogo fedha za kujikimu kama ulikua unatumia elf 20 ndio ushuke utumie elf 10,karatasi za ream unabana matumizi kwa kuandika short hand mlizoe kuandika maneno mengi na hata point hakuna,na kama maelezo ni marefu karatasi iandikwe mbele na nyuma,documents kibao za selikali utakuta ziko mbili au zaidi lakini zimeandikwa upande mmoja tu ukigeuza nyuma ni plain hayo ni matumizi mabovu ya karatasi sawa dogo!piga kazi hapa kazi tu
 
Nakumbuka Rais Mstaafu Mh. Jakaya Kikwete katika hotuba zake aliwahi kusema
".....Mh Magufuli akiwa waziri wa Ujenzi alikuja Ofisini kwangu kuniomba pesa za kuwalipa makandarasi wa ujenzi wa barabara...."

Swali: Je Mh. Rais (JK)angemfukuza Waziri wake kwa kuomba hizo pesa, au ni utaratibu wa kazi.
Si ndio wameambiwa wasiongelee corridor wamwambie
 
Nadhani hawajanyimwa kusema kwamba fedha hazitoshi! Alichogomba Magufuli, ni tabia ya kulalamika na kunung'unika ki-majungu kunakofanywa na baadhi ya mawaziri! Mahitaji uliyoyainisha yanaeleweka na yangepaswa kuakisiwa kwenye bajeti na sio OC. Na hata pale upungufu wa kweli unapojitokeza kwenye OC kuna proper channels za kuwasilisha madai na sio kulalamika!
Tatizo wengi wenu hamjui maana ya OC kwa tafsiri ya mipango/bajeti ya serikali!
Fedha za serikali hupangwa katika mafungu mawili: matumizi ya kawaida, (other charges-OC na matumizi ya maendeleo(development)

Fedha zote hizo hupitishwa na bunge katika bajeti kuu ya serikali!

OC ni fedha za mishahara ya watumishi, posho mbalimbali, gharama za kuendesha ofisi kama mafuta, umeme, maji, matengenezo ya magari, karatasi nk!
 
MLISHAAMBIWA KAMA HAMWEZI KAZI ACHENI ,WEWE BADALA YA KUHURUMIA BIBI YAKO NA NDUGU ZAKO WALIO KIJIJINI WANAOKULA MLO MMOJA KWA SIKU NA WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU UNAHURUMIA MAWAZIRI AMBAO WANAISHI MAISHA MAZURI POSHO NZURI , USAFIRI NA MISHAHARA MINONO , ACHA UNAFIKI ,ACHA RAIS ABANE MATUMIZI ILI PESA INUFAISHE WATU WA KIPATO KIDOGO ,LENGO LA RAIS NI ZURI KUGAWA RASLIMALI ZILIZOPO ILI WANUFAIKE WOTE , KWA HIYO KABLA YA KU PRESENT HOJA YAKO USIANDIKE TU KUJIFURAHISHA ANGALIA MANUFAA YAWE YA WATU MASIKINI WANAOTESEKA ,
 
MLISHAAMBIWA KAMA HAMWEZI KAZI ACHENI ,WEWE BADALA YA KUHURUMIA BIBI YAKO NA NDUGU ZAKO WALIO KIJIJINI WANAOKULA MLO MMOJA KWA SIKU NA WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU UNAHURUMIA MAWAZIRI AMBAO WANAISHI MAISHA MAZURI POSHO NZURI , USAFIRI NA MISHAHARA MINONO , ACHA UNAFIKI ,ACHA RAIS ABANE MATUMIZI ILI PESA INUFAISHE WATU WA KIPATO KIDOGO ,LENGO LA RAIS NI ZURI KUGAWA RASLIMALI ZILIZOPO ILI WANUFAIKE WOTE , KWA HIYO KABLA YA KU PRESENT HOJA YAKO USIANDIKE TU KUJIFURAHISHA ANGALIA MANUFAA YAWE YA WATU MASIKINI WANAOTESEKA ,
 
Kwa uzoefu wangu mdogo nilionao katika fani ya uhasibu katika halmashauri pesa zote ni sehemu ya budget ila dev fund sio OC, road fund sio OC, PE pia sio OC, humo kwenye dev fund kuna matumizi yote km stationary, mafuta, perdiem, extraduty nk pia road fund pia vitu hivyo vipo na OC pia vipo ndo maana wengine wanalilia isiwepo hiyo OC matumizi yake yote yapo sehemu nyingine ila ukiangalia kwa jicho la 3 OC ipo kwa upigaji zaidi maana ndo inayoliliwa zaidi
 
MLISHAAMBIWA KAMA HAMWEZI KAZI ACHENI ,WEWE BADALA YA KUHURUMIA BIBI YAKO NA NDUGU ZAKO WALIO KIJIJINI WANAOKULA MLO MMOJA KWA SIKU NA WANAISHI CHINI YA DOLA MOJA KWA SIKU UNAHURUMIA MAWAZIRI AMBAO WANAISHI MAISHA MAZURI POSHO NZURI , USAFIRI NA MISHAHARA MINONO , ACHA UNAFIKI ,ACHA RAIS ABANE MATUMIZI ILI PESA INUFAISHE WATU WA KIPATO KIDOGO ,LENGO LA RAIS NI ZURI KUGAWA RASLIMALI ZILIZOPO ILI WANUFAIKE WOTE , KWA HIYO KABLA YA KU PRESENT HOJA YAKO USIANDIKE TU KUJIFURAHISHA ANGALIA MANUFAA YAWE YA WATU MASIKINI WANAOTESEKA ,
hao mawaziti kama wanaona oc haitoshi waache kazi nyambaf zao
 
Inawezekana una asili ya ubishi kama siyo mbishi basi unajikomba hutaki kusema ukweli. Watu wenye asili kama ya kwako ni wale wanaomwambia mfalme amevaa na anapenda huku wakijua kuwa mfaulme yu uchi wa mnyama. Kubishana na mtu kama wewe ni kujijingisha nami sipendi kuwa mjinga. Tatizo la kuchelewa mishahara ya watumishi waajiriwa lipo. Usiwe kama mama ANNA Kilango aliyesema watumishi hewa hawapo na kesho yake ikadhihirika kuwa wapo. Wakamtumbua jipu. Tusibishane tatizo la kucheleweshwa kwa mishahara kwa atumishi wapya lipo.
OC inaingiaje kwenye mishahara? Hawa watumishi wapya kabla hawajaingia kwenye Payroll hulipwa posho za kujikimu wakati wakisubiri kuingia kwenye payroll. Ukizingatia kuwa wanakua kwenye mazingira mapya ya kazi mbali na kwao. OC isipokuwepo maana yake wanashindwa kujikimu hata kwa mahitaji madogo madogo, wanadhalilika. Penginepo mwezetu umeshiba kifisadi na ndiyo maana huoni shida ya wenzako-'Mwenye shibe hamjui mwenye njaa' na mzigo wa mwenzio ni kanda la sufu. Mambo kama haya ni ndoto kwako kuyajua au pengine unashiriki kuyasababisha hivyo unatumia fursa hii kujihami[QIUOTE="Nguvu ya Ajabu, post: 15869311, member: 280619"]Mkuu acha uongo. Hakuna anaechelewa kupata mshahara serikalin. Kila mtu anapata on time mshahara wake. Kama hukubajet ajira mpya halafu leo unataka ku ajir kwa kutumia oc we hufai apo ulipo. Umekosa mipango na unaitukanisha serikali. Unapaswa kuwapisha wenye uwezo.
Lakini malalamiko ya Mawaziri ni kuhusu oc. Wanataka hela ikae pale ili waile wanavotaka bila kuulizwa. Hawajasema wizara hazina hela au hela zinachelewa. Wala Hawajasema mishahara haitosh. Au Hawajasema hawapewi siting allowance. Hawajasema hela wanayopata haiwatoshi. Ila wamesema hela haitoshi kwenye oc. Wao wanataka hela nyingi kwenye oc. Oc oc oc oc. Wao ni oc tu.[/QUOTE]
 
Ur words are fake as ur id§§
Acha ujinga,Kama hujui kitu kaa kimya. Mleta mada kasema ukweli mtupu, na Hiyo ndo hali halisi kwenye halmashauri zote nchini, achilia mbali wizara mbalimbali na taasisi zingine za umma. OC ya mwaka huu mwisho imeletwa mwezi January , sasa unatarajia ufanisi gani hapo!!!!!?? Huwezi kuendesha ofisi bila fedha, halmashauri pia zinasomesha watumishi leo hii serikali imebania oc kwa maelekezo kutoka juu, sasa hao watumishi walioko vyuoni watasomaje? Haya kuna watumishi waliostaaf wanastahili kurudishwa makwao utawalipa nn?? Mafuta ya magari utatoa wapi? Karatasi, wino, files utanunua na nn? Na mengi tu, wagonjwa utawasafirishaje kwenda hospitali za rufaa???? Kwahiyo malalamiko haya yanayohusu oc ni ya ukweli kabisa na hali ni mbaya sana, tena mwaka wa fedha ujao ndo itakuwa balaa kabisa.
 
Watu wanaolalamika maana yake wanaogopa kusema, mzee apunguze ukali aisee khaaaa
Tatizo siyo hilo, siyo ukali. Wewe kama ni mfanya kazi wa serikali unajua kabisa watu wana 10% ktk kila kitu, ila mawaziri hawajui. Hivyo unakuta foto copy moja ni 1000 badala ya 200 au 50, na mafuta unakuta mkuu wa wilaya au mkuu wa mkoa au waziri anaenda kula bata anataka hela ya mafuta itoke OC, au unakuta OC ipo haina kazi watu wanatafuta kitu ili iishe badala ya kuisevu. Yaani serikalini kuna ujinga mwingi, acheni kutetea. Hicho kidogo wanachotumiwa kinatosha. Mfano nenda halmashauri zetu uone watu wanavyogawana OC na mapato ya kodi, wengine wanaamua hata kuwadhulumu wafanya biashara. Muombee Mh. Magufuli atumbue majipu tu.
 
Jsmani kama hatujui mambo tusijadili hivi unaposema waweke budget badala ya ON unatakakutuambia nini
 
Watu wanaolalamika maana yake wanaogopa kusema, mzee apunguze ukali aisee khaaaa
KIONGOZI UMESOMA MPAKA UDOKTA HUJUI KUTATUA KUSOLVE MATATIZO SASA ULISOMA NINI YAANI HATA KUBUNI TU VYANZO VYA MAPATO HUTAKI UNATAKA KILA KITU UPEWE BORA WATOKE TU.
 
....Ikumbukwe fedha hizi za OC ndio hutumika kulipa stahiki za wakurugenzi, fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya, kulipa umeme, maji, kununua mafuta ya kuendeshea ofisi, kununua shajala na posho za mawaziri wanapokuwa safarini...

Miaka yote wizara hazijui wanatumia kiasi gani kwenye umeme? Kwa nini wasichukue matumizi ya mwaka wa fedha uliopita na kuongeza asilimia fulani ili kiwango hicho kiingie kwenye budget badala ya OC?

Wizara hazina mipango ya ajira au wanakurupuka tu kila wakati? Kwa nini wasijue mwakani wataajiri watu wangapi na hela ikaingia kwenye budget?

Wizara kwa miaka yote bado hawajui wanatumia kiasi gani kwenye mafuta na matengenezo ya magari ili waingize kwenye budget?

Hayo matumizi yapo kila mwaka na hayaji kama ajali. Ujanja wa kuweka OC kubwa upo miaka mingi na ni chaka la kukwapulia pesa tu.

Huo ndiyo ujumbe JPM anajaribu kufikisha kwenye wizara na idara za serikali!
Hv unaelewa tofauti ya bajeti na oc?
 
Back
Top Bottom