MAWASILIANO ni sekta mUHIMU ambayo imewezesha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli kuwasiliana na wananchi wake, kufikisha huduma na kurahisisha utoaji wa taarifa, kuwezesha makusanyo ya mapato ikiwa ni pamoja na sekta binafsi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, kupunguza gharama za uendeshaji, imefungua fursa mpya za ajira, imeboresha namna ya kuwasiliana pamoja na kuleta huduma mtambuka zijulikanazo kama huduma mtandao.
Huduma hizi ni pamoja na intaneti, Serikali mtandao, mawasiliano ya kijamii (social media), biashara mtandao, fedha mtandao na nyinginezo. Uwepo wa huduma hizi ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi kwani umeboresha maisha ya watanzania na kukuza uchumi wa nchi.
Serikali imewekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya TEHAMA ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, Kituo cha Data cha Taifa ambapo Serikali imetenga nafasi ya asilimia 25 (25%)za kuhifadhi data za taasisi za Serikali na asilimia 75 (75%) za kuhifadhi data za sekta binafsi; na kutoa ruzuku katika ujenzi wa miundombinu ya mawasiliano vijijini ambapo jumla ya shilingi bilioni 93 zimetumika kujenga minara na kufikisha mawasiliano kwenye kata 530 ambazo hazikuwa na mawasiliano. Miundo mbinu hii inahakikisha kuwa wananchi wanapata huduma za mawasiliano kwa gharama wanayomudu na kukuza uchumi pasipo ubaguzi.
Aidha, baada ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kuunganishwa kwenye maeneo mengi nchini, matumizi ya intaneti yameongezeka kutoka watumiaji 19,862,525 mwezi Desemba, 2016 hadi kufikia watumiaji 22,995,109 mwezi Desemba, 2017. Pia, Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano umekuza uhusiano na nchi jirani kwa kuwa umeunganishwa mipakani na nchi za jirani za Uganda, Kenya, Rwanda, Malawi, Zambia, Burundi na Msumbiji na zinaziwezesha nchi hizo kuwasiliana na mataifa mengine ulimwenguni kupitia Mkongo huo kwa Kusafirisha data na taarifa kwa wakati na kwa uhakika.
Uwepo wa miundombinu ya TEHAMA nchini ikiwemo Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano, imeiwezesha Serikali kupitia taasisi zake mbali mbali kutengeneza na kutumia mifumo ya kielektroniki ambayo imeiwezesha Serikali kukusanya kodi na tozo mbalimbali kwa wakati na imeziba mianya ya rushwa na upotevu wa mapato. Kupitia miradi ya miundombinu inayotekelezwa na Sekta hii, jumla ya taasisi 149 ambazo ni Halmashauri (LGAs) 77; na Wizara, taasisi na Wakala (MDAs) 72 zimeunganishwa na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano hivyo zinapata huduma ya mawasiliano ambayo inawawezesha kurahisisha kazi, kufanya kazi kwa ufanisi, kwa wakati, kupunguza urasimu na gharama za usafiri na kuwawezesha wananchi kuwasiliana na Serikali yao.
Pia, mifumo ya mawasiliano imetumika kuhakiki wafanyakazi hewa na hivyo kusaidia Serikali kuelekeza mapato yaliyopatikana kwenye matumizi stahiki ili kuleta maendeleo kwa wananchi na taifa kwa ujumla. Vile vile, wananchi wanatumia huduma za mawasiliano kwa kutuma na kupokea pesa, kulipia ankara, kupata huduma za mtandao kama vile afya, elimu, biashara na masuala ya kijamii. Uwepo wa huduma hizi umewawezesha wananchi kutumia muda wao katika shughuli za uzalishaji na hivyo kutekeleza kwa vitendo kauli ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU.
SEKTA YA MAWASILIANO NA UTEKELEZAJI WA AHADI ZA CCM
Ahadi ya Chama Cha Mapinduzi ni kuhakikisha wananchi nchini kote wanapata mawasiliano ya uhakika ifikapo mwaka 2020. Azma hii inatelekezwa na Wizara ya UjenZi ,uchukuzi na Mawasiliano kupitia uongozi mahiri wa Waziri mwenye dhamana, Mhe. Mhandisi Isack wa Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Atashasta Nditiye, Katibu Mkuu, Mhandisi Dkt. Maria Sasabo na Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Jim Yonazi kwa kuhakikisha kuwa Serikali inafuatilia na kusimamia matumizi salama ya mitandao nchini na kutoa ruzuku ili mawasiliano yafike vijijini na maeneo yasiyo na mvuto wa kibiashara.
Hali ya mawasiliano vijijini inaendelea kuwa nzuri ambapo asilimia 94 ya wananchi wote wanapata huduma za mawasiliano na mitandao ya simu za mkononi imefikia asilimia 95 kwenye vijiji vyote nchini. Hatua hii imeongeza upatikanaji wa taarifa kwa wakati, pasipo ubaguzi kuendana na mahali mtu anapoishi na kuchangia katika kuhamasisha wananchi kuendelea kuishi vijijini kwa kuwa mawasiliano yanawapa fursa ya kujiajiri na kupata huduma mbali mbali.
Serikali iliyo madarakani ilipewa jukumu la kufufua mashirika yaliyobinafishwa ili yaweze kufufuka, kujiendesha kwa faida na kutoa gawio kwa Serikali. Kwa upande wa Sekta ya Mawasiliano, Serikali imenunua hisa za TTCL asilimia 35 zilizokuwa zinamilikiwa na Bharti Airtel ambapo kuanzia mwezi Julai mwaka 2016 Serikali inamilikiasilimia 100 ya hisa zote za TTCL.
Aidha, Serikali kwa kushirikiana na wadau na kupitia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imeridhia na kutunga sheria Na. 12 ya mwaka 2017 ambayo imefuta Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) na kuanzisha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) kwa lengo la kuwa na Shirika imara la Mawasiliano lenye kuhimili ushindani na kutengeneza faida.
UENDESHAJI NA USHIRIKIANO NA WADAU WA SEKTA YA MAWASILIANO
Katika kuhakikisha kuwa mafanikio yanapatikana katika Sekta ya Mawasiliao, Wizara inafanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa taasisi za Serikali na sekta binafsi. Kwa upande wa taasisi za Serikali, utendaji ni mzuri unaozingatia miongozo ya Serikali ya kubana matumizi yasiyo na tija, kufanya kazi kwa weledi na ubunifu. Hii imewezesha Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL Corporation) kutoa gawio la Tsh. bilioni 1.5 katika kipindi kifupi cha utendaji kazi wake tangu Shirika lilipoanzishwa rasmi na kusogeza huduma za simu za mkononi katika mikoa yote nchini. Aidha, TTCL imeanzisha huduma za malipo kwa mtandao yajulikanayo kwa jina la T-PESA ambayo kwa muda mrefu ilikuwa ikisubiriwa na wananchi wenye mtandao wa TTCL huo ambapo simu za TTCL zinaingiliana na simu za mitandao mingine nchini. Anachohitaji mwananchi ni kupata laini ya TTCL na kuiweka kwenye simu aliyonayo tayari kwa kupata na kutumia huduma bora za TTCL zilizo na gharama nafuu ukilinganisha na mitandao mingine. Wa nanchi tujivunie na kutumia huduma zinazotolewa na Shirika letu la Mawasiliano Tanzania kama wanavyojitambulisha kwa kauli mbiu ya RUDI NYUMBANI KUMENOGA.
Katika kipindi cha mwaka 2017/18, Mdhibiti wa Sekta ya Mawasiliano nchini, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imeitoa gawio la zaidi ya sh. bilioni 81 na kuwa miongoni mwa mashirika yaliyotunikiwa cheti na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuvuka kiwango kilichokuwa kimelengwa. Shirika la Posta Tanzania lilitoa gawio la milioni 250 na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ulitoa gawio la shilingi bilioni moja. “Ninajivunia utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais kwa mashirika haya kufanya kazi kwa ufanisi na kuchangia katika kuboresha huduma nyingine za wananchi kwa kutoa gawio,” amesema Mhandisi Kamwelwe.
Aidha, makampuni binafsi ya mawasiliano yameendelea kuwekeza na kutoa huduma zenye viwango bora kwa wananchi. Mathalani, Kampuni ya Simu ya Vodacom imesajili hisa
katika Soko la Sisa la Dar Es Salaam na kuwezesha wananchi kushiriki katika kuwekeza na kutimiza kauli ya Serikali ya kuwa uchumi wa nchi utaboreshwa kwa ushirikiano baina ya sekta binafsi na Serikali. Vodacom pia imefanikiwa kupata masafa katika bandi ya 700MHz ambazo zitatumika kusambaza huduma ya intaneti ya kasi (broadband) kutoka kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano kupitia simu za mkononi na kufikia wananchi nchi nzima.
CHANGAMOTO ZINAZOIGUSA SEKTA YA MAWASILIANO
Changamoto kubwa inayoambatana na kuongezeka kwa fursa zilizotajwa hapo juu zilizopo kwenye Sekta ya Mawasiliano, ni mabadiliko ya kasi ya technolojia na hivyo kusababisha uhitaji wa kufanya marekebisho ya sera, sheria, uwekezaji na kutoa kwa umma mara kwa mara.
Katika kukabiliana na changamoto hiyo, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawailiano kwa kushirikiana na wadau, imefanya mapitio ya Sera ya TEHAMA ya mwaka 2003 na kuboreshwa, hivyo kuwa na Sera mpya ya TEHAMA ya mwaka 2016, kutunga kanuni 20 za sheria ya Mawasiliano ya kielektroniki ambazo zimefanyiwa rejea mwaka 2018 na kuwa na Usalama wa Taifa wa Mtandao uliondaliwa mwaka 2018 na kuwa tayari kwa utekelezaji. Pamoja na uwepo wa mazingira wezeshi ya sheria, bado kunatakiwa kuwa na utambuzi wa uhakika wa watumiaji wa huduma mbali mbali na maeneo waliyopo. Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inafanya kazi kwa karibu changamoto hiyo kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha maeneo ya makazi yanapewa utambulisho kwa kuandika majina ya barabara na mitaa na kuandika namba za kila nyumba.
Katika kipindi cha miaka mitatu, Halmashauri 12 zimeshirikishwa na tayari mfumo wa anuani za makazi unatumika kufikisha barua mlangoni katika sehemu kubwa ya Jiji la Dar es Salaam, Arusha na Dodoma. Pamoja na kuboresha utambulisho, miundombinu hii itawezesha ukuaji wa viwanda kwa kutambua mahitaji ya soko na bidhaa zinazozalishwa na mahali zinapopatikana malighafi. Ni vema wananchi kushirikiana na Serikali katika kuweka miundombinu ya anuani, yaani kusimika majina ya mitaa na namba za nyumba, kwa kuwa haki ya kutambuliwa ni haki ya msingi na itawezesha kuboresha mipango ya huduma za kijamii na kiuchumi.
Aidha, juhudi zinafanyika ili kuboresha usajili wa watumiaji huduma za mawasiliano kwa kutumia vitambulisho vyenye kuainisha vinasaba (biometric) ili kuhakiki mtumiaji. Sambamba na utambuzi, tunahimiza matumizi stahiki ya nywila (password). Wananchi makumbushwa kutumia nywila tofauti kwa vifaa vya mawasiliano kama vile simu na laini ili kujihakikishia usalama wa mawasiliano yako. Aidha, iwapo si kwa ajili ya dharura, wananchi wazingatie kutoweka wazi au kumpa nywila mtu mwingine. Inapotokea unahitajika kutoa nywila kwa ajili ya matumizi ya dharura, mara baada ya matumizi yenye idhini, ukumbuke kubadilisha nywila ili iendelee kuwa siri yako mwenyewe tu. Hili ni jambo la msingi na muhimu katika kuhakikisha usalama wa mitandao.
WITO WA SERIKALI KWA WANANCHI KATIKA KUTUMIA MAWASILIANO
Wizara ya Ujenzi, uchukuzi na Mawasiiano inawapongeza wananchi kwa kutumia vizuri mawasiliano kwa matumizi endelevu. Hivi karibuni Serikali ilitoa tamko kuhakikisha kuwa watoa huduma za utangazaji nchini wanazingatia matakwa ya sheria na kutekeleza majukumu yao ya kuhabarisha wananchi kuendana na matakwa ya leseni walizopewa na sio vinginevyo. Hivyo, niwatake wananchi watumie vyombo ambavyo vimepewa jukumu la kuwahudumia kwa kuendelea kupata habari, taarifa na matangazo kupitia ving’amuzi husika vya star times, Ting, Dijitek na Continental. Pia, wananchi muendelee kutumia vizuri huduma za mawasiliano kwa faida na manufaa badala ya kumomonyoa maadili, mila na desturi za taifa letu na kusababisha uvunjivu wa amani. Mawasiliano yatumike kwa maendeleo ya taifa letu
Iwapo kuna maoni kutoka kwa mwananchi yeyote ya kuchangia katika kuboresha sekta ya Mawasiliano na Taifa kwa ujumla, wananchi mpo huru kuwasilisha maoni au malalamiko husika Wizarani, kwenye taasisi zinazohusika na mawasiliano zilizo chini ya Wizara au kwa watoa huduma kwani tupo kwa ajili ya kuwahudumia wananchi na Kuboresha maisha ya wananchi kwa kutumia Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) .