Hivi kwanini matapeli wengi jijini dsm wanapenda kujifanya wametoka maeneo ya Mufindi, makambako na Iringa huko. Na kujinasibu ni wamiliki wa mashamba ya miti au malori ya kubeba mbao na mizigo toka huko kuleta mizigo bandarini. Nimepata mkasa wa kuataka kuibiwa gari ila wamechukua wallet na simu baada ya kuzunguka nao wakidai wanataka nunua gari yangu niliyokuwa nauza. Na wapo na ushirikiano sana. Baada ya kuwacheki kwenye Gps walionekana wapo kinondoni.