Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,580
- 1,189
MHE. NORAH WAZIRI MZERU - AMEIULIZA SERIKALI MASWALI UWEKEZAJI, VIWANDA NA BIASHARA, BUNGENI-DODOMA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Morogoro Mhe. Norah Waziri Mzeru amemuuliza swali Waziri wa Viwanda Bungeni, Dodoma leo tarehe 14 Aprili, 2023
Je, ni lini Serikali itawasaidia wawekezaji wa kiwanda cha Mazava a Winds Group mkoani Morogoro kupata eneo kubwa la uwekezaji Ili waweze kupanua zaidi eneo la uzalishaji wa Jezi kwani ni kiwanda ambacho kimeajiri Vijana wakitanzania zaidi ya 2800 na Madai yao makubwa ni kuzaliza zaidi jezi ili waweze Kuuza ndani na nje ya Tanzania kwani kutokana na eneo la uzalishaji kuwa dogo wanalazimika kuzalisha jezi ambazo hazikidhi mahitaji ya nje ya nchi na ndani ya nchi ?
Swali lilipata majibu ya Serikali kwa niaba ya Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, kwa niaba ya waziri Mhe. Dkt. Ashatu K. Kijaji; Kupitia Mhe. Exaud Kigahe(Mb)
Swali la Nyongeza;
Je, Serikali haioni sasa kuna umuhimu mkubwa wa kutenga maeneo ambayo hayana migogoro ya ardhi ili kuruhusu wawekezaji wawekeze kwenye maeneo hayo kwani kuwepo kwa viwanda kama Mazava a Winds Group Kunaongeza ajira kwa Vijana kwa Kiasi Kikubwa Zaidi Nchini kwani watanzania wetu ndio wanaajiriwa kwenye Viwanda hivi?." - Mhe. Norah Waziri Mzeru
Vilevile, Swali hili lilipewa majibu ya Serikali Kupitia Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angellah Mabura ya kwamba Serikali imeagiza Mikoa na Halmashauri nchini Kutenga Maeneo ya uwekezaji na kuhakikisha maeneo hayo hayana migogoro ili kuepuka migogoro ya Ardhi katika maeneo ya Uwekezaji
MaswaliNaMajibuBungeni.