Mastaa wa Bongo fleva wenye vipaji ila hawana nyota ya kukubalika kwenye tasnia ya muziki

Eddy Tarimo

Member
Nov 27, 2016
27
38
BEN PAUL: Bernad Paul ndilo jina alilopewa na wazazi wake. Huyu ni mwanamuziki mkali wa Bongo Fleva na nyimbo nyingi anazoimba na uimbaji wake ni mzuri lakini imekuwa ni vigumu kutoboa kimataifa pia kwa Bongo tuzo nazo zimekuwa zikimpitia mbali. Ben Pol ametamba na ngoma kali kama jikubali, unanichora, Sophia na nyingine nyingi.

BARNABA: Barnaba Elias ni mwanamuziki mzuri unaweza kusema anamshinda hata Diamond kiuwezo kwani amefanya kazi kadhaa zikakubalika. Kwanza ni mtunzi wa nyimbo mbalimbali za wasanii wenzake na za kwake mwenyewe. Pili anajua kuimba na tatu anajua kutumia vyombo vya muziki tofauti na wanamuziki wengi ambao wanajua kuimba tu. Barnaba amefanya vizuri kwa nyimbo zake kama Suna, Siri aliofanya na Vannesa Mdee, Wahalade ambayo ilipendwa sana na mashabiki wengi na nyingine nyingi ambapo ameshindwa kufika levo za Diamond wakati anastahili hata kumpita.

BELLE9: Wimbo wa Masogange ndiyo uliomtambulisha kwenye anga la muziki. Abednego Damian ‘Belle 9’ aliutendea haki wimbo huo na nyingine alizowahi kuimba kama shauri zao, listen na nyinginezo lakini ameshindwa kutoboa kimataifa kama walivyo akina Ali Kiba na Diamond wakati ni mwanamuziki mzuri.

RICH MAVOCO: Richard Martin ni jamaa aliyebamba na nyimbo kama pacha wangu, labda niseme, roho yangu na moyo. Ana kipaji lakini amejikuta akififia kadiri siku zinavyosonga mbele. Mwanamuziki huyu hajawahi kufanya kolabo na msanii wa nje ya Bongo na amewahi kusema kwamba hana mpango wa kufanya kazi na wasanii wa kimataifa kwa sababu anaamini atatoka mwenyewe.

MO MUSICMOSHi KATEMI a.k.a Mo Music ni mwanamuziki wa Bongo Fleva ambaye amefanya ngoma kali kama Basi nenda, Simama na Nitazoea. Kiukweli jamaa anajua kuimba na kila anapotoa wimbo unabamba na kuwashika vilivyo mashabiki wake. Mo Music nyota yake imeshindwa kung’aa labda kutokana na kwamba hajaingia moja kwa moja kwenye muziki au la kwani alikuwa masomoni huku akiimba.

Mtaje ambae unahisi anakipaji na nimemsahau apo.
.
 
Nuru Elly.. Alifanya vizuri na nyimbo yake kama umeondoka baba.. Lakini hana nyota kimuziki na jina lake kutajwa masikioni mwa watu ni nadra sana
Ismael Kipira... Niliwah kusikia ana undugu na banana zoro ... Kafanya nyimbo nyingi na nzuri kama gauni la kijani.. Ombi langu na hata kuimba katika band ya Mjomba na baadae B band lakin n vigumu jina lake kutajwa/kusikika midomoni mwa mashabiki wa muziki
Grace Matata.. Daah nadhani kila mmoja alitman kumjua zaidi baada ya "free soul" na wimbo lakini sasa ana wimbo mpya wa lakini haujapata airtime ya kutosha
Steve rRnB.. Sitaki kumuongelea sana ila wengi mnajua anafanya nini
Rama D.. Sina la kuongelea kwake maana mnajua kazi zake
Ngoja niwakumbuke wengine
 
Kuna hii Ngoma tamu saana ila huwezi kuisikia ikipata airtime


Jamaa anajua..Kwa mbele ni km John Legend.
 
Me huwa naangalia masupa star jinsi wanavyoweza kuwa masupa star ni ishu simple tu kujitofautisha na wengine au kuwa/kufanya kitu cha ziada mfano labda mpira messi au ronaldo huwa wanatumia nguvu inayozidi kawaidi ili kujitofautisha na wengine kama uliwahi kuhudhuria sherehe za uhuru kuna afande mmoja alipata umaarufu pale uwanjani kwa jinsi alivyokuwa anapiga kwata ukiangalia wote wamevaa sare kwa kila kitu wamefanana na wanachofanya ni sawa lakin yule mtu alikuwa ni kivutio yote kwa sababu ya upekee ukiangalia diamond huwa utofauti wake upo kwenye vibwagizo,manjonjo manjonjo,nakishi na hata staili za kucheza zinakuwa na utofauti wa pekee lengo ni kutafuta utofauti kuimba tu haitoshi tutapenda mziki wako lakini utakuwa ni muimbaji kama waimbaji wengine tu huna jipya kama una jipya litakufanya ung'ae zaidi ndo usupa star uko hapo na ili uwe na mafanikio unabidi ujitangaze tafuta soko mbali uko wengi wameridhika pale walipofika bila kujua wangekuwa mbali zaidi kupitia mziki ambao tayar wametengeneza
 
Wapo wengi mkuu yaani Kiba na Diamond hawana uwezo wa live performance lakini wape hao vijana uliowataja na uliowasahau wanakupigia live show vizuri.

Mi imani yangu ni kwamba wenye nyota za fasta pia hu-expire fasta. Sitegemei wenye vipaji kutoka barabarani mapema ila hao wengine wape muda.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…