Maskini Baba Diamond, azidiwa ghafla


Abdul Juma ‘Baba D’


Erick Evarist na Gladness mallya

DAR ES SALAAM: Maskini wee! Baba wa staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Abdul Juma ‘Baba D’ anaumwa sana! Ndivyo Risasi Mchanganyiko linavyoweza kukuhabarisha baada ya mzazi huyo kuzidiwa ghafla na kukimbizwa hospitalini kutibiwa kwa msaada kutokana na kukosa fedha, twende hatua kwa hatua.

NI JUMAPILI ILIYOPITA


Tukio hilo la kusikitisha la baba mzazi wa msanii ambaye anatajwa kuwa na ukwasi wa kutosha Bongo, lilijiri Jumapili iliyopita ambapo kwa msaada wa Dk. Fadhili Emily wa Kituo cha Tiba cha Fadhaget Sanitarium kilichopo Mbezi Beach-Africana, Dar, baba Diamond alifikishwa kutoka nyumbani kwake Magomeni-Kagera hadi hospitalini hapo na kupatiwa matibabu.



….Akiwa mapokezi.


CHANZO CHAVUJISHA

Awali, Risasi Mchanganyiko lilipokea taarifa za mzee Abdul kuzidiwa nyumbani kwake lakini ikaelezwa kwamba, hakuwa na msaada wowote hadi majirani walipopata mawasiliano ya daktari huyo na kumuomba amsaidie.

“Jamani baba D (baba Diamond) yupo hoi hapa nyumbani kwake Magomeni. Miguu inamuuma, anashindwa kutembea na ukizingatia hana kipato, anashindwa pia kwenda hospitali. Na bahati mbaya kwa muda mrefu hata majirani wamekuwa wakimsaidia lakini bado hajapata tiba sahihi.”

AUNGANISHWA NA DK. FADHILI

“Leo (Jumapili) kuna jirani yake mmoja hapa ndiyo amepata wazo baada ya kusoma Gazeti la Risasi Jumamosi (ndugu na hili), amepata namba za Dk. Fadhili katika makala anazoandika gazetini kuhusu afya. Akampigia na kumuomba msaada na bahati nzuri dokta huyo ameguswa na tatizo la mzazi huyu, amemtumia nauli ya teksi ili akimbizwe hospitalini kwake, sasa hivi ndiyo wanaelekea huko,” kilisema chanzo hicho.

MAKACHERO WAUNGA TELA

Licha ya kuwa muda huo ulikuwa umeyoyoma (saa 1 usiku), makachero wetu waliingia mzigoni kuelekea moja kwa moja Mbezi kwenye hospitali hiyo na kumkuta baba D akiwa anaingia mapokezi katika kliniki hiyo.



ASAIDIWA NA WAHUDUMU

Akiwa mapokezi, makachero wetu walimshuhudia baba Diamond akisaidiwa na vijana wawili ambao ni wahudumu wa hospitali hiyo, walimkalisha kwenye kochi kisha wakaanza kumpa huduma ya dharura ambapo walimpima presha na kumuita Dk. Fadhili atazame miguu yake.

KUHUSU MIGUU

Dk. Fadhili alipofika, alimvua soksi baba huyo na kuikagua vizuri miguu hiyo kabla ya kuingia naye ndani katika chumba maalumu cha vipimo na matibabu.



VIPIMO VINGINE

Ilibainika kuwa, miongoni mwa vipimo alivyopimwa baba D ni pamoja na kile cha Quantum Magnetic Analyzer ‘QMA’ ambacho kazi yake ni kutambua magonjwa mbalimbali ndani ya mwili wa binadamu. Hata hivyo, Risasi Mchanganyiko halikufanikiwa kujua kipimo hicho kilitambua nini!

BABA DIAMOND AFUNGUKA

Baada ya kupimwa na kupatiwa dawa za kutumia, baba Diamond aliliambia gazeti hili kuwa, anamshukuru daktari huyo kwani ameweza kugundua tatizo linalomsumbua na kwamba anaamini dawa alizopewa zitamsaidia.

“Kwa kweli ni Mungu tu, hali yangu ni mbaya, miguu inanisumbua kwa zaidi ya miaka nane sasa. Inauma, imevimba na inabadilika rangi kuwa myeupe. Inakuwa kama inatoka mabakamabaka. Kiuchumi siko vizuri kabisa.”



NGOZI IMEATHIRIKA

“Dk. Fadhili amenipima, amebaini ngozi yangu imeathirika vibaya. Amenitajia tatizo langu kitaalamu na amenipa dawa za kutumia, lakini pia amenielekeza mazoezi maalum ambayo natakiwa kuyafanya,” alisema baba Diamond huku uso wake ukijaa simanzi.



Dk. Fadhili akimpa mushauri Baba Diamond.


AMWAGA SHUKRANI

Baba Diamond alipoulizwa kama alimueleza mwanaye Diamond kuhusu suala hilo wakati alipozidiwa, alisema hakuona na haoni sababu ya kumwambia kwani analijua na hapendi kuendeleza malumbano na mwanaye lakini anamshukuru Dk. Fadhili kwa kujitolea kumsaidia bila malipo yoyote.



“Sipendi kuendeleza malumbano, ninachokiangalia kwa sasa ni miguu yangu. Nitamshukuru Mungu zaidi nitakapopona kabisa maana nimeshahangaika nayo sana. Kipekee, kutoka moyoni nimshukuru Dk. Fadhili kwa kusikia kilio changu na kunisaidia bure.

“Sikutegemea, mtu unaumwa, anakwambia anakutumia fedha ya teksi uende hospitalini kwake akakutibu bure. Ni upendo wa hali ya juu na Mungu amzidishie, pale alipotoa apabariki na apate zaidi,” alisema baba Diamond.

Diamond

DIAMOND ANASEMAJE?

Gazeti hili lilifanya jitihada za kutaka kumsikia Diamond anazungumziaje suala hilo la ugonjwa hadi kufikia mzazi wake kusaidiwa na mtu baki, simu yake haikuwa hewani lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maandishi kupitia Mtandao wa WhatsApp ulioonesha ameusoma, bado hakujibu chochote.



TUMEFIKAJE HAPA?

Baba Diamond amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo wa miguu ambapo awali, mzazi huyo alisema anasumbuliwa na kansa ya ngozi lakini hata hivyo, mwanaye Diamond amekuwa mzito kumsaidia kutokana na kile kinachodaiwa kuwa ni mwanaume huyo kumtelekeza mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ yeye akiwa mdogo.

MAJIBU YA DK. FADHILI

Juzi Jumatatu, Risasi Mchanganyiko lilimpigia simu daktari huyo na kumuuliza kuhusu tatizo la baba Dimaond na namna alivyolishughulikia, ambapo alijibu:

“Ha! Jamani, ugonjwa wa mtu ni siri kati yake na daktari, labda kama ataona sawa aseme yeye mwenyewe.”

chanzo.Maskini Baba Diamond, Azidiwa ghafla!
Kikubwa ni kujifunza kusamehe mzee alikosa yamepita wanatakiwa kuangalia maisha mpya nataka kujua akifa huyo mzee kwenye msiba ataenda au ? Naisi diamond utoto pia unamsumbua au niseme ulimbukeni afande sele alikanwa na mama yke lkn alisamehe.
 
Tangozo lenu zuri sn kwa kapatia kuitangaza iyo muganga y jadi.alifikilia kumlipa D kumtangaza n garama kubwa sn.bora nitumie tax tu
 
Kikubwa ni kujifunza kusamehe mzee alikosa yamepita wanatakiwa kuangalia maisha mpya nataka kujua akifa huyo mzee kwenye msiba ataenda au ? Naisi diamond utoto pia unamsumbua au niseme ulimbukeni afande sele alikanwa na mama yke lkn alisamehe.
Bila Shaka utakuwa unabebwa na upepo wa watu na hufuatilii vitu, kwani kuna mahali Diamond alishasema hajamsamehe baba yake?? Fuatilieni vitu sio kuropoka..alishasema amemsamehe yote yaliyopita ila kila mtu aendelee na maisha yake, mlitaka amjengee mjumba na gari ndio mseme kamsamehe?? How sure are you kwamba anaumwa kweli na sio anaigiza ili ale mema ya Diamond??? Ana watoto kibao tu akiwemo na yule dogo aliyekuwa anatafuta kiki kwa kuiga nyimbo za kaka yake, yupo Queen Darleen na wengine kwanini wasimsaidie badala yake ugonjwa wake Diamond tu ndio amsaidie?? Angekuwa na mtoto mmoja tu sawa lakini watoto kibao uje kufa na mmoja?? Ugonjwa wake umekuwa jini kwamba Diamond akimsaidia ndio utatoka??? Fikiria kabla ya kuandika vitu, ukiona Diamond kakaa kimya ujue anajua anachokifanya maybe ashajua mdingi anaigiza na pia huyo mdingi zezeta maana anatumiwa saaana na waandishi wa habari na inawezekana analipwa ili kuuza magazeti kwa habari za Diamond tu...bullshit wazee kama hao wanasahau wana watoto wengine wao wanashupaza shingo zao kwa mmoja tu...akafie mbali
 
Bila Shaka utakuwa unabebwa na upepo wa watu na hufuatilii vitu, kwani kuna mahali Diamond alishasema hajamsamehe baba yake?? Fuatilieni vitu sio kuropoka..alishasema amemsamehe yote yaliyopita ila kila mtu aendelee na maisha yake, mlitaka amjengee mjumba na gari ndio mseme kamsamehe?? How sure are you kwamba anaumwa kweli na sio anaigiza ili ale mema ya Diamond??? Ana watoto kibao tu akiwemo na yule dogo aliyekuwa anatafuta kiki kwa kuiga nyimbo za kaka yake, yupo Queen Darleen na wengine kwanini wasimsaidie badala yake ugonjwa wake Diamond tu ndio amsaidie?? Angekuwa na mtoto mmoja tu sawa lakini watoto kibao uje kufa na mmoja?? Ugonjwa wake umekuwa jini kwamba Diamond akimsaidia ndio utatoka??? Fikiria kabla ya kuandika vitu, ukiona Diamond kakaa kimya ujue anajua anachokifanya maybe ashajua mdingi anaigiza na pia huyo mdingi zezeta maana anatumiwa saaana na waandishi wa habari na inawezekana analipwa ili kuuza magazeti kwa habari za Diamond tu...bullshit wazee kama hao wanasahau wana watoto wengine wao wanashupaza shingo zao kwa mmoja tu...akafie mbali
Unajua nn maana kusamehe mtu aendi hta kumjulia hali yke ndio kusamehe uko kifupi yule mtoto ni limbukeni tu ana muda sio yupo busy ila nina hakika akifa yule mzee atajifanya kulia sna ujumbe kibao ujinga yule mzazi ugomvi wa Baba na mama ww sio wako
 
Nakumbuka huyu Mzee alishawahi muomba msamaha kijana wake halafu mtoto anashindwa kukubali msamaha wa baba yake. Yeye Dai anamkosea mangapi Muumba wake?

Tatizo nalo lipo kwa Mama yake, anaona alishaachana na huyo Mzaz mwenzake na ana maisha mengine so anaona Dai atamtunza mke mwingine wa huyo mzee. Uswahili umemjaa huyo mama
 
Una uhakika gani kama haendi Una ushahidi??? Mambo ya familia za watu yaache kama yalivyo...Yule mzee amefua hivyo anatafuta kimchafua mtu ili asaidiwe...huna ushahidi iwapo anaumwa kweli, huna ushahidi kama hawasiliani naye hivyo huwezi kumsemea..ndio Maana nikasema ukiona amekaa kimya ujue anajua anachokifanya.. kama Una kumbukumbu nzuri basi utakumbuka tukio la yule dogo wa Kamwambie alivyosema Diamond katumia uchawi kutoka na yote kwakuwa hakuwa akimsaidia lakini Diamond hakuwa na muda wa kujibu..watu wakaongea saaana kama wanavyoongea Sasa hivi hakujibu kitu anajua anachokifanya hivyo hutakiwi kuwa msemaji wa upande wowote ndugu...
 
Huyu nae sasa hadi picha za kupozi, anatafuta kiki ya nini tena??!!! labda ndio kufutia machozi anayoyajua yeye....mmmh kazidi anataka kuwa celeb haswa...

Alipewa pia salamu za siku ya akina Baba na mwanae Baba Tiffah aka mume wa Zari.
 
Kweli kabisa, ugomvi wa baba na mama haukuhusu mtoto! Ninachokiona ni kuwa Diamond kubebeshwa mbegu ya chuki na mama yake ili amchukie baba yake na ndivyo ilivyo kwa wanawake wengi wasio na elimu na washamba! Baba atabaki kuwa baba regardless ni makosa mangapi aliofanya nyuma, ukishakuwa mwanaume mtu mzima you have to learn to understand things but sioni Diamond akifanya hilo ilihali baba yake alishaonyesha kujuta kwa makosa yake. Huwezi kumsamehe mtu na bado ukaendelea kuwa na kinyongo nae...Haiwezekani!!!
 
Halafu hapo hospital kweli jamani? Mmh, mbona kama Bongo Movie, hizi kamba sasa.
 
Inawezekana babake ana tatizo kwenye miguu yake lakini hana sababu ya kuyumiwa na wenye magazeti na mmiliki wa zahanati kutangaza biashara zao au kutaka kumdhalilisha Diamond - haya ni masuala ya kifamilia wao inaeahusu nini, kwani huyo baba ana mtoto mmoja tu, regardless ya tatizo alilo nalo mambo anayo yafanya skidhirikiana na wanahabari sio mazuri hata kidogo if anything yatamkasirisha Diamond mpaka baba wa watu atajikuta anakosa msaada kutoka kwa Diamond kutokana na kutaka kulazimisha mambo, abashauriwa vibaya na wapambe.
 
Back
Top Bottom