Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,744
- 239,393
Kuna video zimerushwa mitandaoni zikionyesha mashabiki wa Yanga wakimtukuza Mama Samia kwa nderemo , nyimbo na vifijo , kiasi cha kuwashangaza hata wenyeji wao , Yaani kama vichaa wamelipuka mitaani wakimshangilia mama Samia ambaye hakuna anayemfahamu huko S.Africa , ukiacha viongozi wachache wa nchi hiyo .
Uchunguzi unaonyesha kwamba hayo ndio masharti waliyopewa na serikali baada ya kupewa usafiri wa bure , walielekezwa wakampambe mama kwamba anaupiga mwingi , Bali kinachoshangaza ni hiki iweje Samia akasifiwe ugenini ? Taarifa zingine zinadokeza kwamba hata hao mashabiki walioenda hawajulikani walipatikanaje , wako wanaodai huenda ni wanaccm wa Tawi au kata fulani wamepelekwa kimkakati ili kumtukuza mama , haidhaniwi kama ni mashabiki halisi wa Yanga , kwamba Wanayanga walipaswa kuiombea na kuitukuza timu yao badala ya mtu binafsi ambaye hajawahi kupiga hata danadana mbili .
Hakika Bure yaweza kuwa ghali na ikakudhalilisheni huku unajiona , kwa hali hii timu hii ikifungwa nani atasononeka ?