Mapya kuhusu watumishi wa umma kwenda kusoma kwa ajili ya kupanda madaraja na vyeo

Mdakuzi mkuu

JF-Expert Member
Dec 27, 2016
212
719
Habari wanaJF!

Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mh Anjellah Jasmine Mbelwa Kairuki, P.O.Box 34368 Dsm alisema kwamba, ili watumishi wa umma wapande vyeo na madaraja, ni lazima kwanza wapitie mafunzo maalumu ya kiuongozi katika Vyuo vya Utumishi wa Umma; Mbeya, Singida, Uhazili -Tabora, Tanga, Magogoni na Mtwara.

Ikumbukwe kwamba, madaraja na mishahara havijapanda kwa watumishi wa umma ili kujirithisha na zoezi la uhakiki wa watumishi hewa ambao mpaka sasa wanakadiriwa kuwa 19,000.

Maswali ya kujiuliza kuhusu hao watumishi wa umma ambao wanatakiwa kupitia hayo mafunzo maalum:

1. Gharama za kusoma mafunzo hayo ni shilingi ngapi na zinagharamikiwa na nani?

2. Muda wa mafunzo hayo ni miaka mingapi na majukumu ya kiofisi yatakuwa yakifanywa na nani pindi watu wapo masomoni?

3. Mitaala ya kufundishia imeandaliwa na nani, lini na kwa tafiti/research ipi?

4. Muhula wa masomo kwa awamu ya kwanza unaanza lini na utaanza kwa kuchukua watu wangapi, wa ngazi ipi na wa taasisi zipi za serikali?

5. Mtumishi atakayefeli mafunzo hayo atarudia mafunzo au kudisco?Na hela ambazo atakuwa amezitumia je?

6. Watumishi wa umma wenye miaka 2,3,4 wastaafu, nao wanaenda kula shule?

Swala la uhamisho kwa watumishi wa umma bado tu? Mke wangu amehamishiwa Dodoma, mm nipo Mtwara Halmashauri, mateso matupu ndoa yangu inavunjika.

Asanteni kwa kunisikiliza
 
k
 
Maswali ya msingi, ilifaa wayatolee majibu. Utashangaa hawana hayo majibu, siamini hawa watu siku hizi, mtu anadiscuss na mke wake usiku kesho anakuja kutangaza.
 
Reactions: SDG
Kusoma ni jambo zuri na obvious anayesomesha ndio gharama ziko juu yake. Wasiwasi wangu ni kuwa hii imetolewa makusudi ili kuwanyima watu uhuru wa kupanda vyeo na kuongezwa mishahara. Tunaambiwa kuwa watumishi wa umma Tanzania nzima wako zaidi ya 500,000 ambao ukigawanya kwa 3 ina maana kuwa watumishi 150,000 watakuwa wanaenda mafunzoni kila mwaka kwa gharama za serikali. Ngoja tuone bajeti ya mwaka huu itakuwaje lakini utumishi wa umma chini ya Magufuli ni mateso. Hataki kulipa stahili za watumishi kwa sababu ya jeuri na kiburi
 
Tunaongozwa na hisia za watu sasa, badala ya taratibu za kiutumishi.
 
Kuna "mtu" atabatilisha hili tamko.

Pole sana kwa ndoa yako kuwa kwenye hatihati kufikia kikomo
 
Reactions: SDG
Haya nayo ni mambo yanayohitaji mijadala ya kitaifa, ila kwa unyumbu wetu tumeegemea kwa Bashite tu!
Naona kama hizi ni regulations za utumishi ambazo zinahitaji Taasisi maalum kama Bunge au mjadala mpana wa wadau na sio kichwa kimoja tu cha Kairuki!
Mnakumbuka kipindi walichobadili mitaala ya shule na kufanya uozo kabisa na waliendelea kuwatesa watoto wetu kila waziri akibadilika alikuwa anakuja na yake, na mwishowe wakatufikisha pabaya!
Sasa huyu dada naye anatupeleka uelekeo huo mbovu!
 
Sababu nyingine ya kuwanyima watumishi wa umma stahiki zao.!
 
Hawezi maana kuna mikataba inayoonesha upandaji was madaraja. Labda wavunje mikataba wajaze mipya kwa makubaliano baina ya mwajiri na mwajiriwa
 
Reactions: SDG
TUCTA Hawana habari wapo wanagegeda pesa wanazokata kwenye mishahara ya watumishi
 
Elimu bure awamu ya pili huenda ikawajumuisha mpaka watumishi wanaopanda vyeo. Keep watching
 
Maswali ya msingi, ilifaa wayatolee majibu. Utashangaa hawana hayo majibu, siamini hawa watu siku hizi, mtu anadiscuss na mke wake usiku kesho anakuja kutangaza.
Yapo ya msingi zaidi kuliko haya. Kwa mfano, kama Mimi Ni mtaalam WA molecular biology na immunology na kazi zangu za kila siku zinahusu maswala ya PCR, sequencing, cloning, immunohistochemistry, immunodiagnostics na mengine kwenye eneo hilo. Na kama nimekuwa nikipanda madaraja huko huko kulingana na scheme of service ya pale nilipo, huko Chuo cha utumishi natakiwa kwenda kusoma kozi gani? Ikumbukwe kuwa Mimi ni mtaalam tu, sI kiongozi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…