Mapato ya Bandari kushuka, wengi sasa kupitia Mombasa

Wana JF TAFADHALINi Someni KWANZA kabla hamjatoa mautumbo yenu.Mtoa MADA hajakataa kutoa KODI ila anachotaka MAKONTENA yatoke haraka.Kitu alicho kosea ni kuandika atahamishia Mombasa.
Kama anatoa tishio.
Wataalamu wa Bandari haya mambo ya ucheleweshaji ni kweli?
 
Ni ukweli usiopingika kuwa serikali ya awamu ya 5 ikiongozwa na Rais JPM imefanikiwa kuongeza makusanyo kutoka wastani wa bilioni 900 kwaka jana na trilion 1.1.. kuanzanzia December 2015, January 2016 na sasa Feb. kwa kifupi naomba nijaribu kueleza ninachokifahamu kilichosababisha ongezeko hilo ambalo naamini siyo endelevu.
Kama tunakumbuka kabla ya August 2015 yaani July 31, 2015 kurudi nyuma kulikuwa na misamaha ya kodi tax exemption kwenye mashirika ya kimataifa, balozi mbalimbali na baadhi ya mashirika ya kidini. Utaratibu ulikuwa mashitika haya yote kupewa msamaha wa kodi katika manunuzi kwa 18% VAT na uingizaji wa bidhaa mbalimbali kutoka nje hapo kuna kodi kama Import duty, CPF, VAT, EXCESS DUTY na nk.

Baada ya July 31,2015 serikali ilifuta utaratibu wa misamaha hiyo na kuwa refund yaani mnunuzi analipa na kodi harafu anaomba kurudishiwa kodi aliyolipa. Tangu kuanza kwa sheria mpya mashirika yalianza kuomba refund December 2015 na wengi bado hawarejishewa pesa hizo. Hivyo basi serikali inaonekana kukusanya pesa nyingi tofauti na miaka ya nyuma lkn kiuhalisia ni kwamba serikali itakapo anza kurejesha hizo refund itajikuta inapungukiwa na kiasi kikubwa. kwa kipindi cha mwaka 2014/2015 serikali ilitoa misamaha ya kodi ya zaidi ya trilioni 2 sawa na wastani wa bilioni 200 kwa mwezi.

Serikali haiwezi kuacha kurejesha hizo pesa kwaani nyingi ni za wahisani mfano: Diplomatic/balozi zote, mashirika ya kimataifa yaliyo chini ya UN (UNDP, WFP, UNICEF, UNHCR, UNFPA NA NK) WORLD BANK, Mashirika yanayofadhiliwa na mashitrika makubwa OXFARM, USAID, BTC, GIZ, DANIDA, JAICA, na mengine mengi. kwa kifupi mashirika yote ambayo namba za magari ni DFP, NAMBA ZA UBALOZI NA UN hayalipi kodi hivyo yatarudishiwa. Serkalia haiwezei kuacha kurudisha hizo kodi kwa sababu kuna mikataba serikali ilifunga tangu enzi za huko nyuma. Kwa sasa sitaweka mkataba kati ya serikali na baadhi ya nchi kama Marekani. Nawakirisha.
 
Kuna kamgomo barid hapo bandari, aende akatumbue tena kunavipele vmebaki, kunavijana graduate hawana kazi huku kitaa
 
HUKO MOMBASA KWENYEWE WANATIMUANA KWA KUMUIGA MAGUFULI!! WAMEANZA KUTUMBUA MAJIPU YAO, PIA SISI KAMA TANZANIA HATUIGI MOMBASA! ILA KWA HAO WANAOCHELEWESHA NI MUDA TU, WATAENDA KULIMA VITUNGUU MAANA VITUNGUU UNASUBIRI MIEZI, KUTOA MIZIGI INATAKA HARAKA.....
Huaga tunaelewa tofauti sana; nimemsoma mleta uzi sijaona mahali popote alipomlaumu Magufuli; hivi unadhani Magufuli anapenda ucheleweshaji wa mizigo ya wateja pale Bandarini? Kwa mfanya biashara yoyote kwake time is money, Magufuli pia anaonekana anapambana na huo mfumo wa kijinga uliokuwepo miaka na miaka! Msome tena mleta UZI uone kama ana mpinga mhe rais. Lakini pia unaweza kunipa mfano wowote wa Kenya kuunga mkono mageuzi ya Magufuli pale Bandarini? Nitakua wa mwisho kuliamini hilo, watamuunga mkono kwenye mambo mengine but sio Bandarini vinginevyo we wa Kenya huawafahamu vizuri.
 
Mkuu Leo ni siku ya kazi nenda bandarini kuna watu wanatoa mizigo yao waulize ina muda gani tangu ifike halafu uje na mlejesho hapa. Lakini hiyo ya kuambiwa na jamaa si ya kuamini na kupuuza post ya huyu jamaa!

Sikuambiwa bali nimeona. Na mimi kulikuwa na mzigo wangu kwenye hilo Container. Mpaka January 13 mwaka huu container lilikuwa bado halijatoa China.
 
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.

Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?

Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.

Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.

USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.
Banadam hana jema,, anapenda kila upendeleo wa jambo zuri liwe upande wake tu!!
 
mkuu napata shida sana na baadhi ya watu humu JF kwani wameweka ushabiki mbele hata kama mtu anazungumzia jambo la msingi lakini wao wanajitia upofu kwamba hawaoni hilo,mfano mtoa mada kazungumza kitu tofauti na ukwepaji kodi lakini watu kwa kutokujua wanadhani mtu yeyote akilalamikia bandari basi yeye ni mkwepa kodi kitu ambacho sio,mfanya biashara unapomkwamishia mzigo wake bandarini kwa mda mrefu kuna charge ambazo zinaongezeka kama storage,customs rent na demurrage,ili mfanyabiashara aje afidie hizi garama inabidi apandishe bei kufidia hizi garama! alafu wale ambao leo wanashabikia ndo kesho wataathirika na mfumuko wa bei na ndo watakuwa wa kwanza kulalamika.KODI IKUSANYWE KISAWA SAWA NA PIA SPIDI YA KUTOA MIZIGO IONGEZWE.tuacheni ushabiki usio na maana
Ndo tatizo lilipo hilo ambalo linachangiwa sana na wengine kujifanya kujua wakati hawajui! Ukimsoma mtoa mada na kama unafahamu mambo yanavyoenda, huwezi kusita kukubaliana na hoja zake nami nilianza kuliona mapema sana hili!

Nilishawahi kufanya kazi kwenye taasisi moja ya kifedha. Enzi zile suala la kubadili pesa za kigeni ilikuwa ni full of bureaucracy! Mtu atajaza ma-form utafikiri anaomba hati ya uzima wa milele! Wateja wakashituka, wakaamua wawe wanaenda kwenye bureau de change za Waasia ambako unakuta ameshahudumia wateja 5 nyie mna mmoja yule yule na protokali zenu za traditional banking procedure! Binafsi nilikuwa nikiona mteja wa foreign currency anakuja nilikuwa najificha kuona aibu na ile milolongo isiyo na maana yoyote (it's true story hii)! Thanks God baadae tukapata CFO Mkenya akaondoa upumbavu upumbavu wote usio na tija ambao ulikuwa ni kikwazo cha biashara... the guy was my role model. Sasa hapa watu wanadhani vipaumbele vya mfanyabiashara na serikali havifanani na hawataki kufahamu kwamba pasipo na biashara hakuna mapato ya serikali.
 
Naomba muelewe, hata me ni mtanzania napenda nchi yangu ikusanye kodi ili tuendelee, kwaani huko nyuma waliokuwa wanapata hiyo tax exemption walikuwa wafanyabiashara wakubwa, sisi wadogo ndiyo tulikuwa tunalipa kodi halali, ninachotaka kushauri serikali ni kwamba ucheleweshaji mizigo umeongezeka tofauti na siku za nyuma, hapa niongee km mtaalam kidogo (logistician) ili serikali ikusanye mapato kwa wingi ni lazima ihamasishe mzunguko wa biashara-fostering supply chain. ndiyo maana ktk nchi za wenzetu kuna kitu kinaitwa JIT-JUST-IN-TIME ikiwa na maana kuwa kuhamasisha zero storage. let say, mfanyabiashara anaelipa kodi 20m kwa kila delivery akifanya mizunguko mingi ndivyo serikali inatakiwa kukusanya kodi.

Sina maana serikali itoe misamaha ya kodi lakini isimamie uharaka wa utoaji wa mizigo. baadhi mnaweza kuona km kawaida kumbe ni sabotage ya baadhi ya watendaji ambao mitandao yao imekatwa hivyo kujenga mazingira ya rushwa ili wakufanyie haraka km ilivyokuwa miaka 5 iliyopita. Pia kutaka kuwa disappint wafanyabishara wahame bandari ili serikali ya JPM ikose mapato na baada eionekane kuwa na ilifanya makosa kuwatimua baadhi ya watu mhimu.
unaandika kizalendo lakini vijana wengi kula kulala wanakurupuka tu .
 
Shida ya hili jukwaa sasa limegeuka uwanja wa matuc, hakuna thinkers, mtu anaeleza issue ya maana hakuna anayejaribu kuangalia mantiki ya aliyeleta Uzi ila ni kutokana tu. Basi iwekwe wazi watu waandike mambo gani yanayokubalika humu ili asitukanwe.
Watu wengi wameisha anza kuona uko mchezo mwingine mchafu umeanza kufanywa na waliofukuzwa hapo bandarini na mleta mada kaielezea vizuri, majibu ni matusi!!!
 
Jipu limetumbuliwa,teh,teh,teh.
Wahenga walisema kila jambo jema halikosi kasoro, baada ya mheshimiwa Rais na Serikali yake kutumbua majipu akianzia bandari, sasa maisha ni magumu kwa wafanya biashara, wafanyakazi wa bandari na TRA wanachelewesha mizigo kisa ukaguzi mzigo kwa mzigo, kifurushi kwa kifurushi hasa kwenye lose cargo. Biashara yetu imekwama bandari kwa miezi miwili sasa, meli ilifika tangu kati kati ya December 2015, lakini mpaka leo February hakuna hata Dalili, hata kulipa haiwezekani japo document zipo sawa.

Mimi kama mfanya biashara nafikiri kurudi kupitisha mizigo yangu bandari ya Mombasa, kwa sababu miezi miwili mzigo uko bandarilini, jumlisha mwezi mmoja wa kuusafirisha kutoka HONG KONG. Nani anaweza kufanya biashara miezi 4 unasubiri mzigo?

Ina maana kwa mwaka mfanya biashara asafiri mara 4 tu, kwa sababu ukilete mzigo kuutoa ni kuanzia miezi 2-4. Nchi itapoteza mapato makubwa muda si mrefu kwa either wafanyabiashara wengi kupitisha mizigo Mombasa au kwa mkufanya mizunguko midogo ya biashara.

Kwa sasa kila mfanyabiashara anatakiwa kuweka detail za mzigo, mfano km ni nguo uandike rangi, jina la muuzaji, na mambo mengine mengi, hivyo bandarini kila kipande kinakaguliwa km ni sawa na document, hivyo kuchelewesha mzigo kutoka.

USHAURI:
Serikali isimamie vizuri bandari ili kupunguza ukiritimba kwa sababu itapoteza wateja wengi, kama mteja amekamirisha kila kitu hakuna sababu ya kuzuia mzigo wake, alipe kodi aendelee na biashara ili arudi tena kuchukua mzigo.
 
Back
Top Bottom