Maoni yangu kuhusu hukumu ya Ester Bulaya na Halima Mdee

kasenene

JF-Expert Member
Jun 6, 2008
1,632
2,413
Katika mjadala unaondelea sasa hivi nimejifunza mambo machache yafuatayo

(1). Kwanza sikujua kabisa kwamba Spika nae yupo katika list ya wachangiajia..amechangia baada ya Kubenea kama Dk3. wakati kwenye Listi ya wachangiaji hakuwemo..
(ii). Spika yeye ndo mshitaki pili yeye ndio anae simamia hukumu.
(iii). Spika anawanyima upinzani nafasi ya 'Taarifa' ila CCM wamepewa kwa visingizio tofauti..
(iv). Kila anapomaliza kuongea mbunge wa Upinzani.Spika anatoa ufafanuzi na kutoa muelekeo wa hukumu kwa 'kuponda' michango ya wapinzani. Hii inadhihirisha kuwa yeye hakustahili kukalia kiti hicho..
(v). Wanawake kumbe wamekuwa wachangiaji wengi kuliko wanaume kwa upande wa kuwaombea wanawake wenzao wahukumiwe..tofauti na pale zinapokuja hoja za maendeleo...kweli nimeamini wanawake.....
(V).. Wachangiaji wanawake..wanapendekeza adhabu kali saana kuliko wanaume...pili hawataki wenzao warudi mpaka Januari....hivi wanawake mnanini?..
(vi).Spika anazidi kuchemka kwa kuwa 'Subjective'...na amekuwa mchangiaji aliyechukua mda mrefu kuliko wachangiaji wengine woote.
(v).Kwa hakika Bunge hili linastahili Spika na sio kada...

 
Niliwahi kusema humu kuliko tuwe na bunge la aina hii ambalo ni kama mhuri wa serikali ni bora tubaki na mihimili miwili..

Hawa ni watu waliojirundika sehemu moja ili kutafuna pesa za walipa kodi bila sababu za msingi!
 
Wawasamehe dada zetu
 
Hao wanabebana mwanzo Mwisho huwezi kuwatenganisha
by the time wanarudi inawezekana wasimkute 'mwenyekiti wa mjengo' kutokana na ugonjwa hatari na maarufu unaomsumbua...manake dose ndo zimefikia mwishoni...nimeamini zile dawa zinapandaga kichwani..
 
Hakuna marefu yasiyo na ncha. Wananchi tunaelewa na tumejua nani yupo sahihi nani kaonewa.
Cc Maserati
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…