Holy Trinity
Member
- Oct 10, 2023
- 21
- 29
Mbona walishaanza kitambo! Ndio maana hujatangaziwa shule kumi Bora, wanafunzi 10 Bora nk, shule inawekewa grade yake mchezo inaishia hapoWakuu kwema?
Hii naileta kama hoja binafsi, tafadhali wadau emu jambo hili tulitafakari kwa umakini.
Matokeo ya darasa la saba, huwa katika mtindo huu: mfano:
Richard Zembwe Kiswahili-A, Maarifa-A, Hisabati-A, Uraia-B, English...
Pia shule hupewa daraja la jumla kulingana na matokeo. Madaraja hayo ni A-E, ambapo A ndio daraja bora, na E ni daraja hafifu.
Kwa ujumla, jambo hilo ni jema, lakini sasa limechukuliwa kama biashara kwa shule binafsi na hivyo, shule hizo (si zote) zimekuwa zikifanya kila mbinu ili mradi kupata daraja A
Wazazi (wengi) wanachukulia kama shule zenye daraja A ndio bora zaidi katika ufundishaji na ujifunzaji.
Jambo hili linafahamika na shule zote, na ndio maana wako tayari kufanya lolote maadamu wapate daraja A, ili waweze kupata (wateja) watoto wengi zaidi.
Sasa, ili kufanikisha daraja A linapatikana, shule inaweza ikatumia mbinu mbalimbali, mojawapo ni:-
kumaliza topics mapema.
Kulingana na muongozo, syllabus inabidi ikamilike mwezi wa nane.
Lakini, shule inaweza ikalazimisha syllabus ikamilike mwezi wa tatu. Ili wanafunzi wapate muda mwingi zaidi wa kufanya revisions na kujiandaa na mitihani.
Shule hufanikisha hilo kwa kuongeza vipindi vingi zaidi vya ziada.
Matokeo yake mtoto anakuwa overloaded, na hivyo hapati nafasi ya kujifunza na ku reflect yale aliyofundishwa.
Mwanzo mwisho mtoto anafundishwa tu, vipindi vinakuwa bandika bandua, mwanafunzi hapati muda wa kujifunza na kutumia akili yake kutatua changamoto kwenye jamii yake.
Lengo linakuwa ni mitihani tu, na akishafaulu mitihani basi, tuna assume mwanafunzi ana akili... Hii si sawa!
USHAURI KWA SERIKALI
Badilisheni namna ya kutangaza matokeo, kwa kuondoa mianya yote ya ushindani.
Badala ya kuonyesha Gredi, sasa muwe mnaonyesha kama mwanafunzi kafaulu (pass) au kafeli (fail) tu.
Mfano: Richard Zembwe: Kiswahili-pass, English-Pass, Hisabati-Pass, Uraia-fail, Average- pass
Pia sisitizeni shule kufuata muda uliowekwa wa kumaliza sylabus. Nakumbuka kuna kipindi ilianzishwa hii, but wadau wakaikataa.
Chondechonde serikali, fuatilieni hili swala, kwani wanafunzi wetu wanakuwa spoon feeding na matokeo yake huko mbeleni wanashindwa kutatua changamoto za maisha na hivyo kuishia kwenye umasikini wa fikra.
USHAURI KWA WAZAZI
Wazazi tafadhalini sana, achaneni na kudhani kwamba mwanao akipata A darasani ndio ana akili. Akili inapimwa kwa namna nyingi, mojawapo ni kutatua changamoto zitukumbazo.
Pia hata siku moja mzazi, usidhani mwanao hana akili kisa hajapata A,B au C
Yawezekana ni kweli darasani haendi vizuri, lakini haina maana hana akili... Jaribu kutafuta kipaji chake(kitu anachokiweza) na wekeza huko zaidi.
Ukimpeleka shule X kisa wanafunzi wanatoka na daraja A, atapata kweli hilo daraja A, lakini kwa fimbo nyingi, kukariri, kuibia majibu na hata kupewa majibu
USHAURI KWA SHULE BINAFSI
Ni kweli hiyo ni biashara na inapaswa kuonyesha ushindani ili kupata (wateja) wanafunzi wengi zaidi
Sasa, shindani kwenye mambo mengine, mfano huduma bora, miundombinu safi, mazingira bora ya kujisomea na extra carriculums.
Pia shindaneni kwa products mnazozitoa, mfano wanafunzi wahitimu waweze kuonyesha creativities na innovations za kutosha.
Hapo mtakuwa mmelisaidia sana taifa
MWISHO
Naomba mniwie radhi kwa andiko lefu na lenye makosa mengi sana ya kiuandishi. Lakini natumai nimeeleweka