Nilikua naomba maoni, ushauri na mawazo kuhusu hii biashara ya laundry ( kufua nguo ). Nafikiria kufungua katika moja ya maeneo kama Sinza, Masaki, Mbezi beach, Kinondoni. Vipi changamoto zake na faIda zake?
Nilikua naomba maoni, ushauri na mawazo kuhusu hii biashara ya laundry ( kufua nguo ). Nafikiria kufungua katika moja ya maeneo kama Sinza, Masaki, Mbezi beach, Kinondoni. Vipi changamoto zake na faIda zake?
Laundry ni biashara kama zilivyo biashara zingine tu, in nzuri sana lakini ina changamoto zake.
Uzuri wake
1. Ni biashara ya mwaka, haina msimu na wala haitegemei sana misimu ya mvua ama kiangazi
2. Ni biashara ambayo faida yake ni ndogo lakini ya uhakika
3. ukipata eneo lenye mzunguko mkubwa wa watu wenye kipato cha kati inaweza kuwa nzuri zaidi
Ubaya wake
1. Inakuhtaji uwe na machine za ziada ili uwe na quick replacement kwa inayoharibika (kila zikipiga kazi bila ya services ndio zinavyozidi kuharibika
2. Uwe na source ya upatikanaji wa maji ya uhakika
3. Chemical ambazo zinatumika kuondoa madoa na taka taka huwa zinaathiri baadhi ya materials nguo (jiandae na lawama)
4. Wakati mwengine mzigo unakuwa mkubwa wateja wanachelewa kupata nguo zao kwa muda muafaka. Wanakimbia
5. Baadhi ya machine za kufulia kwa mfano PAROS zinatumia umeme mwingi sana, ujiandae kwa hilo.
Ki ujumla si biashara mbaya na kama utapata tenda ya kwenye taasisi ambazo wafanyakazi wake wanapeleka nguo zako laundry hutojutia