Carnivora
JF-Expert Member
- Jan 26, 2018
- 3,650
- 6,012
Habari za muda huu wanabodi,
Bila kuchelewa naomba niende kwenye mada moja kwa moja.
Hapa nchini Tanzania tunayo Mamlaka ya Usafirishaji nchi kavu iliyoundwa miaka ya karibuni kuratibu na kusimamia usafirishaji kwa nchi kavu. Mamlaka hii ndiyo yenye jukumu la kupanga na kusimamia gharama za usafiri pia kulingana na hali ya soko kwa wakati husika. Mada yangu itajikita kwenye usafiri wa daladala.
Kwa miaka mingi sana gharama za safiri wa daladala maeneo mengi ya nchi yetu imekuwa ni shilingi 400 kutoka kituo kimoja hadi kingine. Hii inasemekana wanachaji wastani wa shilingi 30 kwa kila kilometa moja ya usafiri. Mfano ukitoka Buzuruga (jijini Mwanza) mpaka Nyakato National utalipa shilingi 400. Bei imekuwa ikiongezeka kulingana na umbali husika, kwa mfano kutoka Mbagala rangi 3 mpaka Ubungo mawasiliano ni sh 600. Vivo hivyo kutoka Kariakoo mpaka Tegeta Nyuki.
Concern yangu mimi iko wapi? Ama logic ya uzi huu ni nini? Basi twende pamoja.
Kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ni dhahiri kwamba sote twafahamu namna hali ya usafiri inavyokuwa ngumu nyakati za asubuhi na jioni ambapo watu huenda na kurudi kwenye shughuli zao za kila siku. Ukipita vituo vingi vya usafiri wa umma unakuta watu wengi wamesimama kwa shauku kubwa-macho yote yameelekezwa kule mabasi yanapotokea kwa muda huo kutazama ni gari gani yaja ili mtu ajipange namna ya kuliwahi ili awahi huko anakokwenda. Inakuwa mbilinge mbilinge sana na purukushani kubwa.
Lakini katika baadhi ya maeneo kwa uzoefu wangu wa kuishi Dar es Salaam, unakuta kuna watu wenye gari zao binafsi wamepark pembeni na kuna wanaoitia abiria waende kwenye magari hayo wapande kwa nauli ya juu kidogo. Mfano unakuta mtu anaita abiria toka Kimara mpaka Posta kwa nauli ya shilingi elfu 2. Na watu huchangamkia na kuzipanda. Na hapa ndipo hasa penye msingi wa uzi huu. Kufanya hivyo kwanza ni makosa kisheria za usafirishaji. Lakini watu wanasaidika. Nasikia siku hizi pale station wanakamata magari hayo na ukikamatwa unasafirisha watu namna hiyo fine yake inafikia laki 3. Kulikua na bajaji tokea Mbezi mpaka maeneo ya Manzese zikiwasadia sana wakazi wa Kimara na Mbezi nazo zimepigwa stop hivi karibuni.
Kibiashara, ama kiuchumi kuna kitu kinaitwa EFFECTIVE DEMAND kwa lugha ya malkia. Mimi naomba nitafsiri hicho kitu kama UHITAJI KAMILI, nafahamu kwamba si tafsiri sahihi, lakini kwa matumizi ya uzi huu naomba muipokee tafsiri hiyo na itumike hivyo. Effective demand ama uhitaji kamili unatokea tu pale ambapo kuna (i) WILLINGNESS TO BUY (ii) ABILITY TO BUY yaani uhitaji kamili unatokea pale ambapo mtu yuko radhi/tayari kununua kitu na ana uwezo wa kununua. Maana yaweza tokea una uwezo wa kununua kitu lakini hauko tayari kununua kitu hicho kwa wakati huo....hiyo sio effective demand. Ni kama kuoa tu, lazima mtu awe tayari na uwezo awe nao kulingana na mahitaji yake. Kikikosekana kimojawapo, hakuna hitajio kamili. Sasa basi, uzoefu unaonesha kwamba wapo watu na ni wengi tu, wenye uwezo na utayari wa kulipa nauli zaidi ya shilingi elfu 1 kwa safari zao hizo bila wasi wasi. Effective demand ipo.
Naishauri mamlaka ya usafiri iangalie namna ambavyo itaruhusu mabasi ya business class, ambayo abiria wataingia na kukaa bila purukushani na kulipa nauli ya juu wafike safari zao.
Mimi naamini kuna watu wengi wanatamani kuacha magari yao asubuhi na jioni watumie usafiri mbadala lakini wanashindwa kufanya hivyo kwa sababu hali ya daladala zetu katika miji mingi ya hapa nchini hairidhishi. Fikiria mtu anafanya kazi katika moja ya ofisi za pale Golden Jubilee Towers ama ile Ohio Street kiujumla.
Ametoka nyumbani amevalia vizuri anaenda kugombania daladala kwa purukushani mpaka shati lake alilopambana nalo kulinyoosha anafika nalo limejikunja kunja. Si heshima hata kidogo.
Serikali inapambana kujenga madaraja ya juu ili kupungiza adha ya foleni, lakini sidhani kama watendaji wamewahi kufikiria kuwa-encourage watu waache kutumia gari zao binafsi kwa kuwawekea usafiri wa aina hii na tupunguze foleni. Ni nafuu sana kutumia elfu 4 kwenda na kurudi kazini Posta kutokea Kimara kuliko kuweka mafuta kwenye IST.
Naamini inawezekana kuwa na daladala za hivyo, zilizo safi na hazina purukushani, na hakuna mtu kusimama. Leo hii ukiwa na mgeni toka nchi za nje unashindwa kupanda naye usafiri wa umma sababu ya hali ya daladala zetu. Ndio, we lifikirie lile Eicher la Masaki-Gongolamboto likiwa linapita pale Karume saa 12 za jioni.
Mi naamini inawezekana. Kabla hatujaangalia changamoto katika kutekeleza mpango huu. Tuamini kwanza inawezekana.
Karibuni.