Mambo ya kuulizana dini na kabila hospitalini hayafai

mhogoz

JF-Expert Member
Oct 16, 2021
308
479
Kama serikali Haina dini Wala kabila Kuna haja gani ya kuulizwa taarifa kama hizi, nilienda hospitali kutibiwa na Kadi ya NHIF nikawa naulizwa mambo haya imeniuma sana kwa kuwa mimi sioni kama kabila langu na dini yangu kuwa ni vitu vya kujivunia sana naamini kama watu wote ni sawa.
 
dini muhimu ili wajulikane wapagani
 
Kuhusu kabila kuna magonjwa Fulani huwa yapo sana kwenye kabila fulani sometime huisaidia serekali kwenye kukusanya takwimu na tafiti kwanin huu ugonjwa unadominate sana kwenye kabila hili.
 
bahati mbaya umeresti in peace, halafu ndrugu na jamaa zako hawajulikani walipo, basi walau waliokuokota watatafuta watu wa kabila lako, na wa kabila lako wakishindwa kukutambua na kukuchukua kwaajili ya mazishi, basi wale wa dini yako wanaweza angalau kukuhifadhi kwa heshima kwenye nyumba yako ya milele 🐒
 
NIkiwa hospitali siku moja akaja mtu anatembea vizuri, akamaliza hatua zote ikabaki kusubiri kuingia chumba cha daktari.

Tukiwa hapo waiting area mwenzetu akabadilika ghafla ikabidi akimbizwe emergency.

Haikupita hata dk 20 mmoja ya tuliokuwa pale anasema jamaa amefariki wakati akiendelea kuwekewa oxgen.

Kilichosaidia kuna kipengele cha mtu wako wa karibu wakati wa kufungua file mapokezi.

Hizi taarifa mnaweza kuzipuuzia lkn zina msingi linapotokea tatizo.
 

Msaada wa huyo mtu wa karibu ni upi iwapo mgonjwa alifariki?

Vyovyote iwavyo mtu akishafariki ni lazima ndugu wapatikane.

Maradhi unaweza ukaficha ila siyo kifo.
 
Inakera sana hii tabia
 
Mkuu usishangae ,upepo unavoenda ndivyo tunapoenda huko otherwise jambo kubwa lifanyike!!

Tulianzia kwenye jinsia Sasa udini na ukabila ndio tunapoelekea!
 
dini muhimu ili wajulikane wapagani
Then wakishajulikana ndiyo watakuwa wameingiza kodi kiasi gani serikalini?

Ujinga tu wa kuulizana maswali ya hovyo sawa na bank wanaingiza account ya mteja dormant kisha wanamwambia njoo na kitambulisho picha zake na barua ya serikali za mitaa wakati taarifa zote aliwapa wakati anafungua acc.
 
Ni kama polisi
 
Udini na ukabila ndio silaha iliyobakia Kwa chama changu CCM kuelekea kwenye uchaguzi mkuu!

Walianza Kwa kutoa kauli tata"mwaka 2025wanawake watachagua Kwa mara ya kwanza Raise mwanamke"Baadae uungwaji mkono kupitia dini utaanza baadae ukabila unaoshabihiana na mtia nia kwamfano "wanyamwezi"ndio turufu pekee ya kuipitisha team hii ya ccm hapo 2025!coz wapo huko visiwani na mkoa wao wai tabora ni mkubwa sana kiasi kwamba wanaweza pika pilau likaiva wakati wa uapisho hapo 2025 octoba baada ya uchaguzi mkuu!!
Kifupi ni udini na ukabila na uchifu ndio kete yake!!
 
Ni masuala ya kawaida yasikutishe kwani ipo siku utakutana na mtoa huduma anayetokea nchi, mkoa, dini au kabila lako atakupa huduma bora na ya upendeleo tofauti na wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…