Ochoa Home Decor
Member
- Jun 10, 2023
- 54
- 81
Hello habari za muda huu,
Leo maeneo mengi yamekuwa na mgogoro/mgogoro wa ardhi kwa sababu ya baadhi ya wamiliki kutokuwa na elimu nzuri ya ardhi wakati wa manunuzi pia wakati wa utunzaji na uendelezaji.
Sasa nimekuwekea baadhi tu ya mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa kununua ardhi kwaajili ya ujenzi wa nyumba yako ya makazi.
1- UHUTAJI WAKO WA ENEO,
A—— Hapa utahitajika kwanza ujue kwa sasa unajenga nyumba ya ndoto yako (dream house) au unajenga nyumba kwaajili ya kukimbia kadhia ya kodi na umeme wa kuchangishana.
Maranyingi nyumba za kwanza huwa tunajenga kwa kukimbia kadhia ya makodi na kuchoka kupanga kiujumla,
Hivyo kama dhumuni lako ni kukimbia kodi kwanza,basi hapa nakushauri kununua kiwanja kidogo sehemu yoyote ile hata kama ni miji mipya,pia sio lazima ununue kiwanja kikubwa sana.
Unaweza kununua kiwanja kidogo cha kutosha vyumba vitatu na seble na jiko dogo then ukaishi,
Baada ya muda ukanunua taratibu eneo kwaajili ya dream house yako ukajenga taratibu pia,
B ENEO KWAAJILI YA NYUMBA YA NDOTO YAKO,
Hapa lazima uzingatie ukubwa wa eneo,
Maana hii ni nyumba uliokuwa unaiota sana,
Hakikisha unapata eneo kubwa lenye kukidhi ndoto yako,
Kumbuka hii ndio nyumba ya kustafia hivyo lazima tuu itahitaji mambo mengi kama bustani,miti ya matunda na bado pia ubakishe eneo ambalo unaweza kuweka kitu kingine ukihitaji kama mabanda ya kuku,bwawa la kuogelea nk.
Hapa tunakushauri pia utafute eneo ambalo unalitamani sana kuishi.
Dream house haijengwi sehemu yoyote tu.
Hakikisha unaijenga pale unapotamani kuishi,
2—UHALALI WA ENEO
Hakikisha unathibitisha kuwa eneo hilo ni halali kwaajili ya makazi,
Kunamaeneo yametengwa kwaajili ya makazi,huduma za kijamii,nk
Sasa hakikisha unanunua eneo halali kwaajili ya makazi,
Pia umiliki wa eneo uwe ni halali(yaani anaekuuzia awe ni mmiliki halali)
Hapa uhalali wake utaupata kwa majirani zake waliomzunguka,
Baada ya kuoneshwa eneo na madalali hakikisha unarudi mwenyewe au unamuagiza mtu kwenda kuuliza majirani kuhusu mmiliki wa lile eneo,
Ukithibitisha umiliki ndio unaweza kulipia,
Kumbuka mwenyekiti au mjumbe hakuhakikishii umiliki wa eneo anachothibitisha yeye ni kuwa huyu kampa milioni kumi huyu kwaajili ya kununua eneo hili,
Saini kubwa na muhuli juu ya picha,kamaliza kazi,
Sasa eneo ni lake au la familia au kavamia tuu hiyo ni juu yako labda na watu wa ardhi kama lina hati.
NB:hakuna eneo linalokosa majirani,hakikisha unatafuta majirani kwanza hata kama ni porini vipi.
3— ENEO LIWE NA NJIA INAYOWEZA KUPITA GARI,
Hakikisha unanunua eneo lenye njia inayoweza kupita gari mpaka hapo kwenye eneo lako
Usishawishike kununua eneo badae ndio uje kununua njia kutoka kwa jirani,
Hii inaweza ikakugharimu pesa nyingi sana,
Au unaweza kupishana kidogo na jirani akagoma kabisa kukuuzia eneo hilo la njia ukaishia kujuta badae,
4— KAMA ENEO NI MAKAZI MAPYA WEKA ALAMA YA SIRI BILA YEYOTE KUJUA…
Eheee ndio nakupa hiyo chukuaa,
Maeneo ya makazi mapya maranyingi huuzwa zaidi ya maramoja,
Sasa kama unajua unanunua eneo makazi mapya na hutalitumia kwa muda huo basi ukinunua eneo usiku wake tena usiku mkubwa sana rudi na jembe afu chimba mashimo marefu kiasi kwenye pembe nne za eneo lako,chukua makopo ya plastik manne,
Weka karatasi katika kilakopo ulioiandika tarehe ulionunua eneo,mwezi bila kusahau mwaka majina yako pamoja na muuzaji na namba zake za simu.
Funga vizuri afu fukia na weka majani juu yake yani kesho mtu akija asijue kama kulichimbwa,
Angalia katikati ya eneo ni wapi napo chimba fukia kipande cha nondo,
Apo eneo lako hata likiuzwa mara 100 baada ya miaka 20 utakuwa na ushahidi wa kuanzia,
5 UKIWEZA NUNUA ENEO WAKATI WA MVUA KUBWA AMA MASIKA KABISA
Fact hii sio ya kupuuzwa kabisa,
Maeneo mengi wakati wa jua kali/kiangazi kamwe huwezi kuamini kama hiyo ni njia ya maji au hapo maji yanakaa wakati wa mvua,
Lakini shughuli utakayokutana nayo wa kati wa mvua unaweza kusema sio hapa niliponunua,
Basi hakikisha wakati wa mvua ndio unanunua eneo,
Hii itakuonesha eneo lako kama linatunza maji au kama ni njia ya maji,
Pia itakuonesha jografia ya mtaani kwako kukiwa na mvua kunakuaje?
Njia zinapitika?
Ndani utatoka?
Maana kunamaeneo kama kinyerezi kunamfinyanzi wa hatari wakati wa mvua na vilima vile inakuwa
changamoto sana,
Sasa ni bora ujue mapemaa ndio ufanye maamuzi ya kununua au laa….
Hivyo ni vitu vichache kati ya vingi vya kuzingatia unapotaka kununua eneo,