Mama Maria Nyerere Atimiza Miaka 93. Rais Samia amtakia afya njema,furaha na amani.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Jul 28, 2022
25,428
18,865
Ndugu zangu Watanzania,

Mama yetu na bibi yetu mama Maria Nyerere aliyekuwa mke wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius kambarage Nyerere ametimiza miaka 93.

Katika kutimiza huko miaka hiyo Rais wetu mpendwa kipenzi cha watanzania mama wa shoka, chuma cha Reli, shujaa wa Afrika, jasiri muongoza njia,simba wa nyika, komandoo wa vita na nuru ya wanyonge mh Dr Mama Samia Suluhu Hasssan amemtakia afya njema,furaha na amani katika kusherehekea kumbukumbu hiyo muhimu kabisa katika maisha yake.

Ni neema ya kipekee kabisa aliyoipata mama yetu Na bibi yetu mama Maria Nyerere.kufikisha miaka hiyo ni kwa neema tu ya Mungu na siyo kwa ujanja au uweza wa mwanadamu.mama yetu na bibi yetu katika umri huo ameona mengi na kupitia mengi.

Alikuwepo wakati wa vita ya pili ya Dunia,alikuwepo wakati Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere akipigania Taifa letu liwe huru nakujitawala lenyewe,alikuwepo wakati tunapata uhuru,alikuwepo wakati wa vita ya kagera,alikuwepo wakati Rais wa Marekani John F Kennedy anapigwa Risasi na kuuwawa angali akiwa madarakani,alikuwepo wakati wa harakati za akina Dr Martin Luther King junior,alikuwepo wakati wa ubaguzi wa rangi Afrika kusini.

alikuwepo wakati wa Tanzania inasaidia ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika,alikuwepo wakati hayati baba wa Taifa anatoroshwa kutoka ikulu baada ya baadhi ya wanajeshi kuasi,alikuwepo wakati JW inaundwa na kuanzishwa ,alikuwepo wakati hayati Nelson Mandela anafungwa gerezani na wakati anatoka na wakati anakuwa Rais wa Afrika ya kusini ,alikuwepo wakati wa Elnino ya miaka ya 90.

Alikuwepo wakati mfumo wa vyama vingi vinaanza hapa nchini,alikuwepo wakati wa wabunge wa G55,alikuwepo wakati wakati Franklin Roselvet wa Marekani mpaka Sasa wakati wa Joe Biden.alikuwepo wakati wa Barack Hussein Obama kuwa Rais wa kwanza mwenye asili ya Afrika kuingia whitehouse kama Rais wa Marekani.

alikuwepo wakati azimio la Arusha linaanzishwa.alikuwepo wakati meli ya Mv Bukoba inazama,alikuwepo wakati wa maisha ya ujamaa,alikuwepo wakati wa ukame mkali,alikuwepo wakati kikosi cha makomando wa islael wakiongozwa na kaka yake Benjamini Netanyau walipoingia kikomandoo Uganda na kukomboa mateka wa ki islael.alikuwepo wakati matukio yote yanafanyika ndani ya karne moja.

alikuwepo wakati mabomu ya nyuklia yakishushwa katika miji ya Nagasaki na Hiroshima huko japani .alikuwepo wakati jumuiya ya Afrika mashariki inaundwa ,inavunjika na inaundwa tena.alikuwepo wakati nchi zote za Afrika mashariki zinapata uhuru ,alikuwepo wakati wa mzee Mwinyi, Hayati mzee Mkapa,mzee Kikwete,Hayati Dr Magufuli na sasa yupo hai na mwenye afya njema wakati wa uongozi wa Mh Dr Mama Samia Suluhu Hasssa jasiri muongoza njia.

Kwa hiyo mama Maria Nyerere anauwezo wa kukusimulia mengi sana katika umri wake huo wa karibu karne moja.ana mengi kifuani pake ya kukueleza na kutueleza Watanzania mpaka mioyo yetu na miili yetu ikasisimuka. Ni maktaba ya kitabu cha historia,ni darasa tosha ambapo ukimsikiliza mwanzo mpaka mwisho bila shaka unaweza usishike vitabu vya historia vya darasani kwa kuwa unakuwa tayari unaelewa kila kitu.

Alikuwepo na kushuhudia Tanzania kwa mara ya kwanza katika Historia ikipata na kuapisha Rais wa kwanza Mwanamke Rais jasiri , shupavu,imara,mzalendo na madhubuti kwelikweli Mh Dkt Mama Samia Suluhu Hasssan pamoja na kushuhudia Tanzania Ikitoa Rais wa kwanza mwanamke kutoka barani Afrika kuongoza IPU yaani umoja wa mabunge Duniani Mh Dkt Tulia Acksoni mwansasu.

Kazi iendelee mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel mwashambwa, Kijana mzalendo na mpenda nchi yangu.

0742-676627.
 
Vipi mke wa kwanza wa ndoa ya kimila wa Julius kambarage mugendi nyerere Bhoke watiha hafai kupewa zaidi ya sifa hizo???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…