Mama kaniletea mke kutoka kijijini bila ridhaa yangu, nifanyeje?

baptiste

Member
Aug 17, 2015
92
157
Wadau,

Mwishoni mwa Mwezi Disemba mama alikuja hapa Dar na mgeni, walifikia kwangu, mgeni mwenyewe ni binti wa kama miaka 20 hivi, nilishangaa maana mama akija Dar hufikia kwa mkubwa wangu, kaka, mimi huenda kumuona huko.

Cha kushangaza safari hii, mama akafikia kwangu pamoja na huyo mgeni wake, nilipomuuliza kuhusu huyo binti mama akadai wana mambo yao yaliyowaleta, after some days mama akaaga anaenda kuwasalimia familia ya kaka yangu atakaa siku kadhaa, ila atamuacha binti hapa kwangu kwa siku tatu nne.

Nilipoachwa nae binti, roho ya shetani ikatamalaki, nikamrubuni yule binti hatimaye tukashiriki ile dhambi pamoja bila kujua ni mtego eti kumbe mama kamuacha kama mke wangu, nikamuhamishia chumbani kwangu ili nimfaidi sana pindi mama akija kumchukua niwe mwepesi.

Kuja kustuka ni wiki mbili zimeisha tangu binti kuhamia room kwangu na tangu mama aende kwa kaka Kimara, mimi naishi Kigamboni, kukawa na kila dalili girlfriend wangu atakuja siku moja kumkuta binti hapa halafu iwe shida, nikaona nipige simu kwa kaka kuuliza mama anakuja kumchukua huyu binti lini, kaka alishangaa mno, akasema mbona mama alishaondoka wiki nzima nyuma kurudi kijijini na kwamba huyo binti ni mke wako amekuletea na wewe umekubali na amewaacha kwa furaha, nikachanganyikiwa
kumbe ndio maana simu ya mama haikupatikana kwa wiki 2.

Wana JF nimechanganyikiwa, sasa jana nimempata mama hewani ananiambia huyu ndio mke wangu, ana tabia nzuri, kuwa ni mtoto wa flani wanamjua tangu kuzaliwa, kwamba hata baba karidhia na ndie aliyewasafirisha, kwamba wamenivumilia muda mrefu nipo nipo tu hivyo waniletee mke.

Naombeni msaada

Sijui siku Florence akija hapa itakuaje na mimi bado nampenda

Help please
 
Last edited by a moderator:
 
Nikushauri, Mwambie umepata semina unaondoka kidogo, hemea vitu vitamu sokoni,
Onesha mapenz ya dhati kwa siku tatu bila kupanic

Kisha umpe safari ya dharura kuelekea kijijin ukimuahidi next week ukitika safari unaenda kuandaa mipango ya harusi, mnunulie na simu.

Akiondoka hama na nyumba, mchezo kwishney, utamuandikia msg huwezi kuoa kwa sasa.

Just kidding.
 
Naombeni msaada

Sijui siku Florence akija hapa itakuaje na mm bado nampenda

Help pls

Dah! sasa wewe, unaona kabisaa mama kakuacha na mtoto wa kike peke yenu. Wakati kama kaweza kukaa baye hapo si shida akaenda naye kwa kaka. Hushtuki tu?
Swali moja kwanza, ulimkuta bikra?
 
Dah! sasa wewe, unaona kabisaa mama kakuacha na mtoto wa kike peke yenu. Wakati kama kaweza kukaa baye hapo si shida akaenda naye kwa kaka. Hushtuki tu?
Swali moja kwanza, ulimkuta bikra?
Siku hizi bikra ni story tu... Ye ameshaoa hivyo.. Aweke plans mpya 2016 inoge.
 
Haaaaaaa!!! baptiste wewe utakuwa wa kule kwetu, kwani hata mimi nilikoswa koswa kwa mbinu hiyo mara mbili, mara ya tatu mama akanyoosha mikono akasema amekubaliana na mimi kuwa atamkubali mwanamke yeyote kutoka popote nitakayechagua mimi!!! na ndivyo ilivyokuwa!!. Pole.
 
kaletewa binti kaandaliwa kabisa yupo kwenye danger kitu kisha nasa asubirie matokeo ya mchezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…