1. kukua uchumi kwenye makaratasi na si kwenye mifuko ya wafanyakazi.
2. waajiri kuwanyima wafanyakazi uhuru wa kujiunga na vyama vya wafanyakazi.
3.watumishi wa umma kuishia kulipwa posho tu na si mishahara.
4.TUCTA imeendelea kufanya tathimini ya gharama zamaisha na kukuta kuwa mwaka 2009 mfanyakazi alipaswa kulipwa kima cha chini cha Tsh 315000/= lakini kima hicho hakikufanyiwa kazi na waajiri na serikali.
5. Tunaimani serikali hii yako Magufuli utatuongezea mishahara kwakua mapato sasa ya serikali yameendelea kuongezeka siku hadi siku.
6.Tunaomba mifuko ya jamii ipunguzwe na kuwe na mifuko miwili tu yaani mfuko wa sekta binafsi na sekta ya umma.
7. kuwepo na mabadiliko ya kiutawala kwenye mifuko ya jamii kama ilivyofanyaka kwenye mfuko wa NSSF ambako kumeleta ahueni kwenye mfuko huo.
8. Tunaomba kodi ya serikali ya pay as you earn ipunguzwe na iwe ya tarakimu moja, kwakua washauri waliokuwa wanaishauri serikali zilizopita hawakuwa na ubunifu wowote kiasi kwamba walizipotosha serikali zilizopita kushindwa kupunguza kodi ya mishahara.
9. Wafanyakazi kufanya kazi bila mikataba hasa kwenye mashirika ya umma kama Tanesco,
Mwana JF wewe umeguswa na lalamiko gani na nini ushauri wako kwa serikali hii ya hapa kazi tu?