Makonda: Wananchi masikini msikimbilie mahakamani, kuna rushwa! Watumieni viongozi wa Serikali kutatua shida zenu

lord atkin

JF-Expert Member
Sep 30, 2018
202
697
Makonda: Mungu amenipa mlango dhidi ya aliyenidhulumu nyumba

Katibu wa itikadi na uenezi wa chama cha Mapinduzi Paul Makonda amefunguka jinsi alivyodhulumiwa nyumba na mtu mwenye pesa. Paul Makonda amesema alipodhulumiwa nyumba wajanja walimshauri aende mahakamani ila akakataa maana anajua mahakamani hakuna haki kwa masikini. Makonda aliamua kumuomba Mungu na sasa Mungu amempa mlango.

Hivyo Makonda ameshauri wananchi masikini wasikimbilie mahakamani kwani Kuna rushwa badala yake wawatumie viongozi wa serikali kutatua shida zao.

Itakumbukwa kuwa mwaka 2022 iliripotiwa katika vyombo mbalimbali vya habari uwepo wa mgogoro wa umiliki wa nyumba iliyopo regent estate Mikocheni, Jijini Dar Es Salaam Kati ya Paul Makonda na GSM.

Chanzo; Global online
 
Kama ameyaongea hayo bhasi ni

Message sent kwa "aliemdhulumu" nyumba

Message delivered kwa muhimili wa mahakama

Message delivered kwa waliomcheka na kumdhihaki kuwa "hajawasahau"


Kiufupi wamekufa ndege wengi kwa jiwe moja 😁😁

Haya nasubiri kushuhudia wafu wakizikana
 
Back
Top Bottom