Makonda: Ujenzi wa Dar es Salaam ya viwanda umeanza rasmi

*RC MAKONDA: UJENZI WA DAR ES SALAAM YA VIWANDA UMEANZA RASMI*

Ama kwa hakika kila mmoja wetu anaifahamu dira na dhamira ya serikali ya awamu ya *tano ya Dr. John Pombe Magufuli ya kuifuta historia yetu ya aibu ya muda mrefu ya kuwa na taifa la wachuuzi kwa kuligeuza kuwa taifa la wazalishaji kupitia kuchochea uanzishwaji wa viwanda vya kutosha chini ya mwamvuli wa sera ya Tanzania ya viwanda.*

Ni kwasababu hiyo tu, sisi watendaji wake aliotuamini na kutupatia dhamana, hatuna budi kuendelea kuwaza zaidi, kutenda zaidi na kushirikisha washirika wengi zaidi ili kwa pamoja tuikamilishe ndoto hii ya Rais wetu mpendwa.

Kuelekea kutimiza azma hii *tayari ninapozungumza nimekamilisha maongezi na mshirika wetu wa maendeleo Azimio Housing Estate kampuni ambayo imekubali kutupatia eneo lililopo Kigamboni lenye ukubwa wa ekari 1500 la thamani ya zaidi ya bilioni 121 na milioni 470 litakalotumika kama eneo maalumu nitakaloligawa kwa wajasiriamali zaidi ya 3,000 kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vya idadi hiyohiyo.* Pamoja na mambo mengineyo mpango huu *unakusudia kuwasaidia wamiliki wa viwanda vidogo kupata maeneo yao ya kufanyia kazi ili kuwapunguzia gharama za kukodi maeneo, kuwaepusha na usumbufu wa kukaa maeneo yasiyo rasmi pamoja na kuwapatia uhakika wa kuwa na anuani (address) za kudumu.*

Kimsingi chini ya utaratibu huu *kila mmiliki wa kiwanda kidogo tutampatia Sqm 2,000 hivyo eneo hilo litabeba viwanda vidogo zaidi ya 3,000 ambavyo vitatengeneza ajira za moja kwa moja zisizopungua 15,000 zitakazoambatana na ajira zisizo za moja kwa moja zipatazo 43,000.*

Kwa namna ya kipekee niendelee kuwashukuru Azimio Housing Estate ambao *wameendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano ambayo Mpaka sasa imedhihirisha ni kwa kiasi gani uongozi wake unafanya kila jambo kwa kuzingatia maslahi mapana ya wananchi wake.*

Na mfano wa hili ni mdogo tu, badala ya kuhangaika kuomba ekari zote 1500 kwa ajili ya wamiliki hawa wa viwanda vidogo wanaopambana kubadili historia za vipato vyao usiku na Mchana ningeweza kujiombea hata ekari 10 tu kwa ajili yangu na mke wangu nikatulia.

Itoshe tu kusema kwamba, *maamuzi ya kutanguliza maslahi ya wananchi ndio yameufanya mkoa wangu Mpaka sasa kuendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya zaidi ya bilioni 160 ambazo nimezipata kwa wadau wa maendeleo waliotuchangia na kufanikisha utekelezaji wa miradi hiyo inayojumuisha ujenzi wa wodi tatu kubwa na za kisasa zenye ghorofa tatu tatu, theatre kubwa za upasuaji, hospitali kubwa ya Chanika ya zaidi ya bilioni 8 za kitanzania, Makao Makuu ya kisasa ya Bakwata ambayo yapo katika hatua za mwisho, madarasa, barabara, mahakama 20 za mwanzo na Vituo 20 vya polisi.*

Na kwa ushahidi wa haya machache niliyoyataja ibaki tu kuwa ushahidi ya kwamba, *utajiri wa Makonda ni wa watu kwa Maendeleo ya watu kwani Dar es Salaam tuitakayo ipo mikononi mwa wanadar es salaam wenyewe*.
 
washirika wa maendeleo ? Mbona Mkuu anatabia ya kuwa karibu na watu na makampuni tata ambayo tayari yamechokwa kwa tuhuma mbali mbali....
AZIMIO HOUSING ESTATE Ni kampuni ambayo tayari ina kashfa kubwa huko NSSF kwenye nradi wa Dege kule Kigamboni. Wamefanya ufisadi mkubwa kwenye mradi ambao hakuna mpaka sasa hakuna nyumba waloziuza .
mmiliki wa Azimio Housing ni Baghdad. huyu jamaa alishafungwa jela enzi za Mwinyi kwa kufanya utapeli wa viwanja kila mahali Dar kwa kushirikiana na Ardhi. Alifungwa 5 years jela..leo katoka ndio mshirika wa maendeleo.
Pia huyu huyu Baghadad alitaka kuichukua uwanja wa Mnazi Mmoja kujenga maduka lakini wazalendo wa Dra es salaam wakayavunja mabati na program ile ikafutwa.
inaelekea Makonda haijui Dar ingawa anataka kutufukuza na ndala ...hawajaui hata watu wa kuleta maendeleo ..anadaka watu wenye kashafa kama njia ya kuwasaidia kutakatisha fedha chafu...
hapana inatosha ukitaka kuwapa viwanja naona umekosa ubunifu.
manispaa lilinunueni eneo la gerezani muwalipe fidia wenye nyumba pale na mujenge majengo makubwa ya ujasiri mali ..mfano wa Jua kali kule kenya...wale wa gerezani watapata mahali salama na wengine nao watapata sehemu ya viwanda ambayo tayari ina huduma muhimu na wateja.

Ardhi ya Kugaiwa na matapeli ni njia ya kuwasaidia kuwatoa kwenye tuhuma...hatutaki...unafanya kwa GSM na sasa kwa Baghdad..kunani ?

Tunashukurusana Lukuvi kutusikiza..kuna watuwenye kashfa ndio wanawafanya wema ...
Afadhali kiliochawenhi kimesikilizwa..
 
Kwanzia makonda atuitage ma graduate wote mwaka flani akatuambia twende leaders pale, mara kufika tunakuta akina le mutuz ndio wanaongea eti wanatupa ushauri. Mara tukaambiwa tupeleke CV kwa mkuu wa wilaya. Wallahi hakuna kilichofanyika mpaka leo..

Yaani sina hamu na makonda. Hata simsikilizagi tena akiongea. Hata nikimsikia anaongea kwenye redio na nipo kwenye daladala huwa naweka earphones maskioni.

Ni hayo tu wadau
asante lukuvi

ingawa wengi hawakukuelewa
 
Kumbe ardhi yenyewe kacheza keusi na kekundu?Ahahaha Makonda kaenda pokea ardhi ya serikali
 
Daudi Bashite mzee wa kukurupuka. Yaani mpaka aibu wallahi.

Hivi huyu jamaa huwa anawaona waliomtangulia kiwa walikuwa wajinga na Malofa?? Yaani yeye eti anataka kuacha legacy bwahahaha. Legacy my foot.

Atulie officn afanye kazi kama wenzake walivyofanya kazi kimya kimya na atulize mshono maisha yaendelee.. nyambaff
 
Back
Top Bottom