Makonda, only the truth will set you free!

IWILL

JF-Expert Member
Jun 2, 2011
346
120
Takribani wiki tano hivi story iliyoko kwenye mitandao na vyombo vyingine vya habari hapa nchini vinaendelea kutaka ufafanuzi wa hasa nini kilichopo kwenye nyuma ya pazia kuhusu elimu nzima ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam.

Vita ya dawa za kulevya ni halali japokuwa imejaa dosari za hapa na pale, lakini katika maongezi yangu ya leo ni kulielezea la umiliki wa vyeti vya Makonda na utata uliogubika katika usomaji wake mpaka kufikia hapo alipo.

Kwa mujibu wa taarifa zinazoendelea mitandaoni inatia shaka kwanini mkuu huyu wa mkoa asifike mahali asimame mbele na kuliondoa wingu hili lililotanda katika uongozi wake, hii itakuwa sahihi zaidi na mzigo anaomtwisha Rais Magufuli kumtetea kuwa hana hatia. Makonda inatakiwa ifike mahali ajitakase huo uhalifu.

Sidhani kama Rais anaweza kulifumbia macho suala la kudanganya kuhusu vyeti na kutokana na kauli ya mheshimiwa rais kusema bayana kuwa hakuna mtu yeyeto atakaye salia mtume kwa kugushi cheti.

SHERIA NI MSUMENO.
 
Binadamu tunatenda makosa makubwa sana eitha kwa bahati mbaya au makusudi. Lakini kuadhibiwa au kusamehewa siku zote huwa kunategemeana na mkosaji mwenyewe atachukua hatua gani baada ya kugundulika kosa lake.
Wapo hata watu wameua wenzao lakini mazingira ya kosa na respond ya mkosaji kujitambua ilisaidia kuachiwa huru kabisa kwani walikiri na kutubu kuwa wamekosa.
Kuna kila dalili kuwa wewe sio Paulo Makonda bali Daudi Bashite. Sio jambo baya na dhambi kubwa sana kwani wengi wamefanya katika kutafuta maisha. Na wewe hukukata tamaa pamoja na kufeli mitihani ukaamua kutafuta maisha zaidi badala ya kukata tamaa.
Sasa hilo kwa wakati huu limekuwa sio la kawaida bali kosa la jinai na wapo watumishi wengi sana tena wazuri kiutendaji pengine kuliko wewe na walibakiza muda mchache kustaafu wamepoteza kazi na mafao yao.
Wewe kama ni kweli ulifanya hivyo, acha kupambana na ukweli. Sema ukweli na kuweka wazi kuwa ulikuwa unatafuta maisha na watu watakusamehe nawe utajiweka huru.
Nimekuona ukilia pale Kanisani Kimara. Mimi nimekuelewa, hiyo hali inatutokea sana binadamu katika mapambano ya kiroho. Kuna jambo roho yako inataka useme ila nafsi yako ya kibinadamu na kiburi vinakukataza lazima ulie machozi huwezi kuhimili.
Nakuhakikishia kama ungekuwa mkweli na kazi ufanyayo ina baraka za Mungu basi hata siku moja hungeliona chozi likikudondoka zaidi ya furaha moyoni hata kama dunia nzima ikikuzomea
 
Mkuu Chakaza, mimi natofautiana na wewe kwa kumsisitizia Paul Makonda ashikilie msimamo huo huo wa kukaa kimya, asigeuke nyuma atageuka jiwe.

Jana pale kanisani alilia kwa uchungu kwa jinsi watu wabaya wanavyomsingizia. Mimi ni miongoni mwa washauri wake wa bure humu JF.
Kashfa hii ilipoibuka tuu nikamshauri ifuatavyo
Baada ya Dr.Kigwangala, Mwigulu, sasa ni zamu ya Makonda kuhusu jina, hii inaweza kuwa kweli au?

Baada ya mimi kujiridhisha tuhuma hizi ni uongo tuu na uzushi, nikamshauri anyamaze kimya na asijibu kitu.
Kumbe ni Uongo, Uzushi, Fitna, Majungu, Wivu na Kijicho Dhidi ya Mafanikio Yake!. Makonda Wapuuze! .

Paskali
 
Mkuu Chakaza,
Natofautiana
Ndugu yangu, najua wewe ni mtu wa Imani. Jaribu kwenda deep zaidi utaona kilio kile kanisani ni cha nguvu mbili zinazo vutana kiroho. Moja ina mwambia sema ukweli uwe huru na ile nyingine ya kiburi na majidai inasema achana na hilo utachomoza tuu!
Msukosuko huo moyoni lazima ulie tuu. Waulize walokole huwa wanalia nini kanisani? Au fanya research utajua. Yeye aseme kweli tuu na itamuweka huru.
 
Na kama ikija kubainika ya kuwa makonda ana vyeti, basi mamlaka ya uteuzi nayo inatakiwa ijitazame kwa undani, lakini pia hili linatupatia picha nyingine ya kuwa, katika zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki huenda ilikuwa ni danganya tu ili kuwaumiza watumishi wa umma, msingi unatokana na sababu ya kwamba, kama kweli zoezi zima lilikuwa haliangalii sura wala cheo cha mtu ilikuwaje huyu jamaa anayejiita bashite kusalia katika hili, mamlaka husika kwa maana ya wale wanaohalalisha vyeti(Necta) tunaomba mtusaidie kuhusu jambo hili ili umma wa watanzania ufahamu kama kweli mkuu wa mkoa ana vyeti halali au anatumia vya mtu mwingine
 
You are misleading him Mr paschal sir. Kutokana na maneno aliyoongea pale kanisani anaonyesha kuijua biblia kidogo. Dawa ya dhambi ni toba paschal. Mwambie afanye hivyo. Kwani kuna mahali imeandikwa RC ni lazima awe graduate? Mzee mzee Rashid alikuwa premier na elimu yake ndogo? Usimpoteze mwenzako. Rais Magufuli ni mkali ndiyo lakini ni mwelewa pia. It's just a question of confession paschal. Tell him to confess basi
 
Vile Vile mwambie aache kuwa na kiburi cha uzima
 
Kama anaonewa basi, Mungu atamlipia lakini best way ni yeye kutoka nje na vyeti la sivyo ajiudhuru nafasi yake.
 
Paskali amejiridhisha kuwa tuhuma ni za uongo na uzushi....
Paskali taratibu, kitaeleweka pale mmoja wa hawa watu wawili Daudi au Paulo watakapokuja kutanzua kitendawili.
Imekuwa rahisi sana wewe kumtetea RC Makonda lakini yeye amekuwa bize kupiga picha za dua na kuziweka mtandaoni.
Jana hadi machozi kamwaga tena mengi kuliko ya Steve Mengele baada ya msuto wa Mama Sepetu.
 
Pascal badala ya kumshauri Makonda njia sahihi ya kufanya unazidi kumponza.
 

Kijana wako anapimwa kwa kipimo kile kile alichokuwa anawapima wengine kwa kuwadhalilisha hadharani, kuwatuhumu bila ushahidi kwamba wanafanya biashara ya dawa za kulevya. Kwamba anapotuhumu yeye ni sahihi lakini kibao kikimgeukia inakuwa ni fitna na kusingiziwa?? Ama kweli "mkuki kwa nguruwe...."

Mshauri aombe toba kwa dhambi ya "kumshuhudia jirani uongo" ndipo atakapopata amani.....
 
Mkuu kama makonda atapita humu na kuona ulichokiandika kwa kweli ni mjivuni tu ndiye ambaye atajifanya hajakuelewa this is.....
 
Ww jidanganye kwa mkate kidogo lkn nyote ww na huyo jamaa yako ni wapumbavu anakansa ya lol lkn unamdanganya aseme amekabwa na mfupa wa samaki lkn iko siku maumivu yakizidi radhima atakwenda muhimbiri na jibu kansa imeshaharibu hivyo hakuna namna bali kusubiri lawama kwann hamkuniwahisha mapema ?hapo lawama zitakuwa kwako anyamaze?wakati maji yanambeba we mjinga kweli muulize not wa ruthu.
 
Paskali mimi nakushauri kitu kimoja tu, mshauri huyu unayemtetea alimalize hili jambo kwa kuweka wazi vyeti vyake na jina lake kamili. Kumbuka kua hakusoma shule yake yeye mwenyewe wako wengi sana walio soma naye na ndio wanaotoa taarifa hizi. Kwa sasa anapoteza mda tu, ukweli uko wazi, ni jambo la muda tu, na historia inasema hakuna hakimu mkubwa kama mda "time". Ukweli utamweka huru siku zote, akingojea hukumu ya mda ataaibika.
Watu hawana tatizo na UKUU WAKE WA MKOA, hakuna sheria inayo kataza mtu aliye pata division "0" kuwa mkuu wa mkoa.
Tatizo ni jinai ya kutumia jina na cheti cha mtu mwingine. Hivi angesema toka mwanzo kama yeye ni Daudi na alipata division "0", mkuu akamchagua hivyo hivyo kutokana na uchapakazi wake hakuna mtu hata mmoja angepiga kelele, na isengelimhusu mtu yeyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…