Makonda amjibu Lukuvi adai ataendelea na kuendeleza zile ekari 1,500

MAKONDA AMUONESHA JEURI LUKUVI.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda amemuonesha jeuri waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleao ya Makazi William Lukuvi kuhusiana na eneo la hekari 1,500 alilopewa hivi karibuni kwa kusema ofisi yake inaendelea kujipanga ili kuliendeleza eneo hilo

Hivi karibuni Mkurugenzi wa Hazimio Housing Estate ya Jijini Dar es salaam Mohamed Iqbar alimkabidhi Makonda eneo hilo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo vidogo vya biashara

Baada ya taarifa hizo Waziri Lukuvi alijitokeza na kusema Makonda alidanganywa juu ya eneo hilo na kuwa linamilikiwa na serikali na sio mali ya mfanyabiashara huyo

Mbali na kosa la kudanganya serikali, Lukuvi pia alisema atamchukulia hatua mfanyabiashara huyo kwa kumiliki Ardhi kinyume cha sheria

Mbali na kauli hizo za Waziri Lukuvi Makonda hakuonesha hali yeyote ya kujali wakati akifungua mkutano wa kamati ya Ushauri wa Mkoa (RCC) Jijini Dar es salaam Makonda alisema changamoto za ukosefu wa maeneo kwa wafanybiashara na wajasiriamali zitaondoka kwa kuwa wataalamu wa ofisi yake wanajipanga kuendeleza eneo hilo

Makaonda alisema baada ya kukamika kwa utaratibu wa upimaji eneo hilo litatengwa katika makundi matano ambapo wajasiriamali wa Wilaya zote za Jijini hapa wenye nia za kuwekeza watakabidhiwa maeneo hayo kwa utaratibu utakao pangwa.

Fahari news
Hapa umechanganya madawa kwa kiherehere! Nadhani Lukuvi hakusema kuwa hili eneo halitatumiwa kwa viwanda. Yeye alizungumzia umiliki. Na akasema kuna sehemu ya wananchi ya eneo la viwanda!
 
Sasa Mh Lukuvi amesema ni eneo la Serikali na Mh Makonda amesema ataendelea na program hapo shida iko wapi wakati wote ni Serikali Kuu tena moja.

Tusitafute tu maneno ya kusema ionekane kama kuna shida ktk uongozi.
 
Serikali ya wahuni ndivyo ilivyo ubabe ubabe tu nani atamzuia homeboy wa nanihii kufanya atakalo!? Serikali inaenda kama gari bovu halina sukani. Serikali imepoteza mwelekeo haijui itendalo ni madudu tu mwanzo mwisho.
ila sometimes ni nzuri sana kuwa homeboy aisee. akiwa mkuu wa kaya na wewe unakuwa mkuu wa kaya, na akidondoka mnadondoka wote. mtu anao uwezo hata kubishana na mawaziri, ana bahati sana aisee.
 
Laundering .........ninachojua,anayehusika na ardhi na maendeleo yake kwanza ni halmashauri husika za jiji,hakuna sheria inayomtambua mkuu wa mkoa katika masuala ya ardhi,ndio maana huwezi kusikia ofisi ya mkuu wa mkoa/wilaya inagawa Viwanja.

Huyu anajipa kazi ya kugawa Viwanja kwa ajili ya viwanda,

Na muhusika mwenye eneo lukuvi alisema "hawezi kumruhusu kutakatisha uchafu wake"

Kama ndivyo,pengine tungeujua uchafu huo na huyo mwenye "uchafu" kwa nini anasema mkuu wa mkoa ndiye alimuomba hilo eneo

Mkuu wa mkoa alijuaje hilo eneo ni la mohamed Akbar? Alimuomba baada ya kufanya vikao na halmashauri na wananchi? Je alihusisha wizara ya ardhi? Anajua hana mamlaka ya kugawa Viwanja? Kama hana mamlaka kwa nini amekomalia kugawa maeneo ya viwanda?
 
Makonda hana tofauti na makondakta wa daladala.. Makondakta wengi ni wabishi.. Elimu hawana.. Wavuta bangi na wanywa viroba kweli
ila usipokuwa na elimu unaweza kuwa mbishi sana, hata ukieleweshwa huwezi kuelewa. ila siku utakapokuja kuanguka, hadi wadudu watakucheka.
 
Haka kajamaa kapuuzi sana
Kanapewa jeuri na bwana mkubwa hata kwenye mambo ya ovyoovyo

Bashite tumechoka sinema zako weka vyeti acha maneno
 
Mfanyaniashara Ikbal amejibu kuwa eneo ni lake, kideo akiongea na mapaparazi


 
Makonda ana nguvu kuliko Lukuvi,yeye ni namba 4 baada ya waziri mkuu.
Mawaziri mnatakiwa mumuheshimu Makonda lasivyo mtatumbuliwa.
 
Serikali ya wahuni ndivyo ilivyo ubabe ubabe tu nani atamzuia homeboy wa nanihii kufanya atakalo!? Serikali inaenda kama gari bovu halina sukani. Serikali imepoteza mwelekeo haijui itendalo ni madudu tu mwanzo mwisho.
Kwa namna hii tusitegemee matokeo chanya ktk awamu hii kwe uchumi.

Ubabe unauporomosha uchumi

Ubabe unaiyumbisha serikali na one day itaanguka

Uchumi mbovu, mapato yamepungua,, hii yote kwa sababu ya ubabe

Tukutane 2020
 
huyu jamaa kweli alipata Division 0, hivi anabishana na waziri mwenye dhamana ya kusimamia ardhi. Magu tumbua hili jipu libakudhalilisha
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Waendelee kuvurugana hivyo hivyo mpaka kufika 2020, ila Makonda anajiamini jamani natamani kujua hiyo nguvu anaipata wapi

Unatamani au unajua,Acha kujipngopea.Sizonje inammaana humjui?Ndio yeye!
 
kijana inabidi akumbuku ya kuwa mkubwa ni mkubwa tu
ila naona anajiweka zaidi katika wakati mgumu kwa kiburi chake hivyo asipojiangalia atapotea haraka sana kwenye
ulimwengu wa siasa


jifunze kutoka kwa wakubwa zako bwana mako
 
Aliendeleze tu kwa manufaa ya wamachinga wa Dar, lakini asisahau kuweka hadharani vyeti vyake na aainishe majina yake aliyoandikisha kuanzia primary, Sekondari mpaka sasa! Hilo asitusahaulishe! Utata wa vyeti vyake hauwezi kuisha hivi hivi tu! Kwa nafasi yake hana namna ya kulikwepa hilo lazima aweke kumbukumbu sawa!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom