Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

Yaani Makonda ni kiherehere kweli...sijui ni msukuma gani wa hivyo. Pamoja na kumsimanga mzee wa watu, lakini bado anajipeleka kwenye msiba? Halafu hiyo familia nayo ndiyo wanajipendekeza ili serikali isiendelee na uchunguzi wa ufisadi wa marehemu ama? Maana sielewi ni kwanini walimruhusu Makonda kufika na hadi kupewa muda wa kuongea!!
kwani makonda ni msukuma? Bas napata picha kwa nini anajihamin na iyo nafas kupewa
 
hili gazeti lina taarifa za umbea sana, sasa hii nayo ni habari ya kuweka front page ili ipeleke ujumbe gani kwa jamii?
YEYE MAKONDA ALIPOENDA PALE MSIBANI ALIFUATA NINI KAMA SIO KWENDA KUWAONGEZEA UCHUNGU WAFIWA? MAMBO MENGINE YANAHITAJI KUTUMIA AKILI KIDOGO TU.
 
hili gazeti lina taarifa za umbea sana, sasa hii nayo ni habari ya kuweka front page ili ipeleke ujumbe gani kwa jamii?
Yaani wewe mpaka sasa hujajua ni ujumbe gani uliopelekwa kwa jamii kwa hili sakata la makonda na marehemu Kabwe?! utakuwa mvivu wa kufikiri.. tafsri moja ndogo tu nikupe, hakuna aijuae kesho, Makonda angejua hili asingefanya alilofanya.
 
hili gazeti lina taarifa za umbea sana, sasa hii nayo ni habari ya kuweka front page ili ipeleke ujumbe gani kwa jamii?
ujumbe unaokwenda kwenye jamii ni kwamba bwana makondakta aache UNAFIKI. mtu amesababisha kifo cha mpendwa wao halafu anaenda kuwapo mikono ya kinafiki ili iweje?
 
TATIZO LA BWANA MAKONDAKTA NI KUJIFANYA MJUAJI NA MTOTO WA MJINI...SASA AMEKUTANA NA MTOTO WA MJINI KULIKO YEYE. MAKONDA AMECHANGIA KIFO CHA KABWE KWA ASILIMIA KUBWA.
Jamani tuache kuwatisha viongozi wetu wanapochukua hatua stahiki dhidi ya wahujumu uchumi. Tujifunze tu yakuwa dhuluma ni mbaya sana. Sio kuwa wachochezi.
 
ni majonzi tu aliyonayo kwa baba yake kipenzi...nadhani aliishiwa nguvu ya kunyanyua mkono.
 
Jaman mambo mengine sio ya kupost humu, kwanza unapoandika vile ni dhahiri kuwa umefurahishwa na kitendo cha huyo binti, pia mi sioni kosa la makonda kusema makosa na ubadhilifu wa kabwe uliopelekea mpaka kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi, pia ieleweke kuwa kazi ya kutumikia umma huhitaji mhusika awe na uadilifu kwa umma.
Kabwe amefanya kazi kama mkurugenzi kwa mkoa wa mwanza, mbeya na dar lakini udhaifu mkubwa ulionekana ukiambatana na ubadhilifu, kusimamishwa kazi kusiwe sababu ya kumuona kuwa alikuwa mwema mno kiasi cha kumuona makonda kama kihelehele kwani naamini aliyafanya yote hayo kwa faida ya wanadaresalaam wote hata watanzania kwa ujumla.
Kila kifo kina sababu zake, kama inasemekana tayari alikuwa mgonjwa, je haikupaswa kumsimamisha kazi kisa mgonjwa kwa kuhofia atafariki? Tuacheni unafiki wa kuwa vigeugeu wasioeleweka, baadhi mlilalamika kuwa marehemu alikuwa tatzo leo tena lawama kwa makonda?
R.I.P KABWE
 
Back
Top Bottom