Makonda achuniwa na mtoto wa Kabwe msibani

kyalankota

JF-Expert Member
Jul 27, 2014
2,594
1,460


Anna Kabwe, binti wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe amegoma kumpa mkondo Paul Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Tukio hilo la aina yake lilimfika Makonda aliposhiriki shughuli ya kuaga mwili wa Kabwe katika Viwanja vya Karimjee alipokuwa akitoa mkono wa pole kwa familia ya Kabwe.

Wakati Makonda akimpa mkono, Anna aliendelea kuchezea simu yake huku akipuuza mkono wa kiongozi huyo. Anna alifanya hivyo akiwa amekaa huku ndugu zake wengine wakiwa wamesimama wakati wakipokea mkono huo wa pole.

Kitendo hicho kimetafsirika kwamba, Anna alikumbuka tukio lililofanywa Aprili 19 mwaka huu wakati wa uzinduzi wa Daraja la Kigamboni ambapo Makonda alimtuhumu marehemu Kabwe (baba yake) kwamba amehusika na kusaini mikataba iliyoikosesha mapato serikali.

Kabwe alifariki tarehe 19 Mei mwaka huu kutokana na tatizo la ini. Mauli yalimkuta akiwa katika Hospitali ya Mama Ngoma jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Ameacha mjane na watoto watano; wanne wa kiume na mmoja wa kike.
 
Binti wa aliyekuwa mkurugenzi wa jijj la dar es salaam marehemu Kabwe amchunia RC Makonda.

Hata mim siyo kumchunia bali hata kwetu asingekanyaga. Naweza sema hata kama Kabwe alikuwa anaumwa but kifo chake kimesababishwa/kimeharakishwa na changamoto za kibinadamu alizozipata baada ya Makonda kusababisha atumbuliwe.

RIP KABWE.
 

Attachments

  • IMG-20160525-WA0034.jpg
    67.6 KB · Views: 153
Anajua fika kwenda kwake pale anawaongezea wafiwa maumivu

Kiherehere cha nini kujipeleka...si angeenda mkuu wa wilaya

Huu ni ukosefu wa Ubinadamu

Lile lilikuwa suala la kifamilia....Alitakiwa tu kutumia common sense
 
Ni ujinga tu wa huyu makonda

Anajua fika kwenda kwake pale anawaongezea wafiwa maumivu

Kiherehere cha nini kujipeleka...si angeenda mkuu wa wilaya

Huu ni ukosefu wa Ubinadamu

Lile lilikuwa suala la kifamilia....Alitakiwa tu kutumia common sense
kwani marehemu aliwahi kufanya ubinadamu? nikumbushe...alikosea angejiunga CHADEMA mgemsafisha fasta.
 
Yaani Makonda ni kiherehere kweli...sijui ni msukuma gani wa hivyo. Pamoja na kumsimanga mzee wa watu, lakini bado anajipeleka kwenye msiba? Halafu hiyo familia nayo ndiyo wanajipendekeza ili serikali isiendelee na uchunguzi wa ufisadi wa marehemu ama? Maana sielewi ni kwanini walimruhusu Makonda kufika na hadi kupewa muda wa kuongea!!
 
Haya mambo ya Suarez na Patrice Evra yapo mpaka kwenye misiba...Tulizoea kuona kwenye mpira ligi z Ulaya
Ndio maana mambo ya kuajiliwa ni kama "Utumwa",Mzee Kabwe "alitumbuliwa" na Makonda mtoto wake kabisa wa kumzaa
Maana mwaka 1982 wakati Mzee Kabwe anaanza Chuo Kikuu akisomea Sheria,Bwana Mdogo Makonda alikuwa hajazaliwa kabisa,nafikiri hii ya Kabwe ni moja kati ya kumbukumbu "mbaya" ya Makonda ktk utumishi wake na maisha yake ya kiroho.Makonda ni "kijana" wa yule Pastor Ndegi wa Kawe.Kwa ulimwengu wa Roho,hii kitu ina nafasi yake,kama tu "dhamira ya kiroho" ya Makonda bado i hai.
 
kwani marehemu aliwahi kufanya ubinadamu? nikumbushe...alikosea angejiunga chadema mgemsafisha fasta.
sijaongelea issue ya marehemu alikuwaje...however he was...yule ana familia yake ambayo wote wanamthamini kama mzazi na ndugu yao...however he was

Msibani ni sehemu familia inapata fursa ya kumwomboleza ndugu yao

Sasa limtu linajibeba tu linaenda kama vile pale pia ni shughuli ya serikali...Upuuzi na kutotumia common sense
 
bado mahakama ya mafisadi ikianza atafunguliwa mashitaka na familia itafilisiwa haiwezekani familia yako ikaishi kama ipo peponi kwa mali za wizi tena kudhulumu wanyonge.
 
Yawezekana alikuwa na majonzi kupita kiasi
hata akashindwa kutoa mkono kwa mheshimiwa
si sahihi kufikiri kwamba alifanya makusudi.

msiba unahitaji uvumlivu kwa waliowahi kufiwa wataniunga mkono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…