Makadirio ya Kupaua Nyumba Kwa kadiri ya Fundi

Super Sub Steve

JF-Expert Member
Jul 9, 2011
17,391
10,885
Ndugu wanajamvi,nimejikusanyakusanya hatimaye kupata visenti vya kufikiria kuezeka Nyumba yangu.Fundi kanipa makadirio yafuatayo kwa materials.
Nyumba Ina ukubwa wa
Upana Ni Futi 28 Urefu Ni Futi 36 japo Kuna upande mmoja Kuna Kama futi Moja na nusu imeongezeka.
Kwa hiyo roughly 28ft upana,na 36ft Urefu.
Makadirio ya Fundi
1.Bati migongo midogo Alaf bati 90
2.Kofia 22
3.Valley 7
4.Kenchi waya 5 (Hizi nadhani Ni pakiti)
5.Misumari ya bati 25kg
6.Mbao treated 2×4×20 hapa kasema ninunue mbao 114
7.Mbao treated 2×2×20 hapa kasema ninunue 80
8.Mbao 1×10×12 fishabodi kashauri 17
9.Misumari inchi 4 kg 30 (Hapa kanishauri ninunue Bei ya jumla kg 50,itabaki mingine nitahifadhi kwa ajili ya blundering)
10.Misumari ya inchi 3 kwa ajili ya fishabodi kg 3.
11.Ufundi nimenegotiate naye mpaka tumekubaliana 1,000,000/=Tshs.
NB.
Bati Ni za upana wa 90cm.
Ndugu wadau naomba msaada wa maboresho.Wapi niongeze wapi nipunguze au nibaki hivyohivyo.Asanteni

Mrejesho baada ya kupaua
1.Bati fundi alikadiria 90 zimetumika 88 zimebaki 2

2.Kofia alikadiria 22 zimetumika kofia 17 tano zimebaki
Valley alikadiria 7 Zimetumika karibu zote

3.Mbao alikadiria 2×4×20 mbao 114 zimetumika mbao 100 zimebaki 14

4.Mbao 2×2×20 ziliagizwa 80 zimetumika 72 zimebaki 8
Misumari ya bati na kenji imebaki kiasi kidogo
NawasilishA
 
Ndugu wanajamvi,nimejikusanyakusanya hatimaye kupata visenti vya kufikiria kuezeka Nyumba yangu.Fundi kanipa makadirio yafuatayo kwa materials.
Nyumba Ina ukubwa wa
Upana Ni Futi 28 Urefu Ni Futi 36 japo Kuna upande mmoja Kuna Kama futi Moja na nusu imeongezeka.
Kwa hiyo roughly 28ft upana,na 36ft Urefu.
Makadirio ya Fundi
1.Bati migongo midogo Alaf bati 90
2.Kofia 22
3.Valley 7
4.Kenchi waya 5 (Hizi nadhani Ni pakiti)
5.Misumari ya bati 25kg
6.Mbao treated 2×4×20 hapa kasema ninunue mbao 114
7.Mbao treated 2×2×20 hapa kasema ninunue 80
8.Mbao 1×10×12 fishabodi kashauri 17
9.Misumari inchi 4 kg 30 (Hapa kanishauri ninunue Bei ya jumla kg 50,itabaki mingine nitahifadhi kwa ajili ya blundering)
10.Misumari ya inchi 3 kwa ajili ya fishabodi kg 3.
11.Ufundi nimenegotiate naye mpaka tumekubaliana 1,000,000/=Tshs.
NB.
Bati Ni za upana wa 90cm.
Ndugu wadau naomba msaada wa maboresho.Wapi niongeze wapi nipunguze au nibaki hivyohivyo.Asanteni
Fundi amekupa makadilio kulingana na alivyoliona jengo lako na mtindo wa paa uutakao (Roofing style). Fuata maelekezo ya fundi, hapa tukupongeze tu kwa hatua uliyofikia ya kuachana na nyumba za kupanga. Cha kuongeza au kupunguza ni makubaliano na fundi.
 
Asante mkuu,itabidi nizingatie Hilo.Maana kidogo kwenye mbao nilitishika kidogo niliona Kama zimekuwa nyingi mno kwa kadiri ya makadirio yangu ya awali Lkn itabidi nizingatie ushauri wake
 
Ndugu wanajamvi,nimejikusanyakusanya hatimaye kupata visenti vya kufikiria kuezeka Nyumba yangu.Fundi kanipa makadirio yafuatayo kwa materials.
Nyumba Ina ukubwa wa
Upana Ni Futi 28 Urefu Ni Futi 36 japo Kuna upande mmoja Kuna Kama futi Moja na nusu imeongezeka.
Kwa hiyo roughly 28ft upana,na 36ft Urefu.
Makadirio ya Fundi
1.Bati migongo midogo Alaf bati 90
2.Kofia 22
3.Valley 7
4.Kenchi waya 5 (Hizi nadhani Ni pakiti)
5.Misumari ya bati 25kg
6.Mbao treated 2×4×20 hapa kasema ninunue mbao 114
7.Mbao treated 2×2×20 hapa kasema ninunue 80
8.Mbao 1×10×12 fishabodi kashauri 17
9.Misumari inchi 4 kg 30 (Hapa kanishauri ninunue Bei ya jumla kg 50,itabaki mingine nitahifadhi kwa ajili ya blundering)
10.Misumari ya inchi 3 kwa ajili ya fishabodi kg 3.
11.Ufundi nimenegotiate naye mpaka tumekubaliana 1,000,000/=Tshs.
NB.
Bati Ni za upana wa 90cm.
Ndugu wadau naomba msaada wa maboresho.Wapi niongeze wapi nipunguze au nibaki hivyohivyo.Asanteni
Bati zipo za ubora tofauti na makampuni tofauti. Jitahidi sana usinunue bati zenye ubora hafifu.Bati safi kwa Tz simba dumu/Alaf gauge 28.wengine wanajikongoja tu.
 
Ndugu wanajamvi,nimejikusanyakusanya hatimaye kupata visenti vya kufikiria kuezeka Nyumba yangu.Fundi kanipa makadirio yafuatayo kwa materials.
Nyumba Ina ukubwa wa
Upana Ni Futi 28 Urefu Ni Futi 36 japo Kuna upande mmoja Kuna Kama futi Moja na nusu imeongezeka.
Kwa hiyo roughly 28ft upana,na 36ft Urefu.
Makadirio ya Fundi
1.Bati migongo midogo Alaf bati 90
2.Kofia 22
3.Valley 7
4.Kenchi waya 5 (Hizi nadhani Ni pakiti)
5.Misumari ya bati 25kg
6.Mbao treated 2×4×20 hapa kasema ninunue mbao 114
7.Mbao treated 2×2×20 hapa kasema ninunue 80
8.Mbao 1×10×12 fishabodi kashauri 17
9.Misumari inchi 4 kg 30 (Hapa kanishauri ninunue Bei ya jumla kg 50,itabaki mingine nitahifadhi kwa ajili ya blundering)
10.Misumari ya inchi 3 kwa ajili ya fishabodi kg 3.
11.Ufundi nimenegotiate naye mpaka tumekubaliana 1,000,000/=Tshs.
NB.
Bati Ni za upana wa 90cm.
Ndugu wadau naomba msaada wa maboresho.Wapi niongeze wapi nipunguze au nibaki hivyohivyo.Asanteni
Kanunue hivyo vitu mwenyewe.
 
Siku hizi pia kuna upauaji nafuu kwa kutumia mirunda.
Unaweza kumwambia fundi akukadirie uone unafuu wake.
 
Kamwe usimtume fundi anunue vifaa. Bora usimamie mwenyewe Jumamosi na Jumapili hadi nyumba iishe kuliko kujenga kwa rimoti au wale wanaosema wanakujengea wanakukabidhi
 
Kama unapaua paa limesimama kama la kanisa hizo hesabu ni standard kabisa. Kama vp badili mfumo weka contemporary garama zitapungua kwa asilimia kama 50.
 
Kamwe usimtume fundi anunue vifaa. Bora usimamie mwenyewe Jumamosi na Jumapili hadi nyumba iishe kuliko kujenga kwa rimoti au wale wanaosema wanakujengea wanakukabidhi
Njia nzuri ya kujenga ni weekends ukiwepo.
 
Bora kuweka makadirio makubwa ili ujipange kazi iishe kuliko kukwamia njiani,manunuzi fanya mwenyewe
Na simamia shoo mwanzo mwisho,maana mafundi wanaibaga mbao sana, material yakibaki yatajenga hata mabanda ya uani
 
Hiyo bati ya alafu unachukua g.ngapi mkuu,mi nimeagiza gauge 30 bei ni 30000 kwa piece ya futi 10, kwenye kupaua tumia 2*3 na 2*4 badala ya 2*2 za siku hizi ni nyembamba sana, 2*6 pia zinatumika kuna fundi alinipigia hesabu ila sijui zinatumika wapi
 
Upande wa bati ongeza tano ziwe 95 na kofia ongeza 3 za ziada ili kuepuka usumbufu na gharama za kufuata nyengine kwa agent au kiwandani itakapobidi maana ALAF mitaani sehemu nyingi hawapo so itakapopungua bati moja tu itakubidi utumie gharama kuifata au uchanganye na ambazo hazina ubora kitu utakachokijutia maisha yako yote,ilinikuta hii ikabidi bati 7 nitumie 30,000/= usafiri ili zifike site.

Kwa kuanzia nunua misumari 20Kg na hizo mbao nunua kama alivyokuelekeza but ukitoa bati hakuna kingine cha kukupa hofu maana vyote mtaani vinapatikana kiurahisi so unaweza kununua pungufu ya hesabu yake.

NB:kuwa makini na fundi wako coz anaweza kukununulisha vitu akijua vitazidi ili baki aondoke nayo,njia nzuri msimamie au tafuta mtu unayemwamini asimamie taratibu zote za matumizi ya vifaa ujenzi.Kila la heri braza
 
Siku hizi pia kuna upauaji nafuu kwa kutumia mirunda.
Unaweza kumwambia fundi akukadirie uone unafuu wake.
..............Sikupingi,ila tuache kumung'unya maneno kwenye ujenzi hakuna kitu kinachoitwa “unafuu”.

Nafuu gharama,tu-assume umeezeka kwa mirunda leo baada ya miaka kadhaa paa likapata hitilafu je una uhakika utakuwa na uwezo wa kufanya maintenance ya kuridhisha wakati huo umeshakuwa na majukumu kuliko sasa?bora hapa ameshaamua kuumia acha aumie kwa ajili ya kesho ili kile cha kesho afanyie maendeleo mengine
 
Kamwe usimtume fundi anunue vifaa. Bora usimamie mwenyewe Jumamosi na Jumapili hadi nyumba iishe kuliko kujenga kwa rimoti au wale wanaosema wanakujengea wanakukabidhi
Kwenye boma Kuna sehemu nililiwa kidogo na fundi na anayenisimamia ila kwenye Kupaua nataka nikomae mwenyewe kusimamia.
 
Hiyo bati ya alafu unachukua g.ngapi mkuu,mi nimeagiza gauge 30 bei ni 30000 kwa piece ya futi 10, kwenye kupaua tumia 2*3 na 2*4 badala ya 2*2 za siku hizi ni nyembamba sana, 2*6 pia zinatumika kuna fundi alinipigia hesabu ila sijui zinatumika wapi
Kwenye bati mfuko wangu unaishia kwenye Resincot g30.Alaf Bei kwa bundle Ni 461200 lkn Agent nimeambiwa naweza pata kwa 450000 ambapo kwa piece ya ft 10 Ni Kama 28125.
Mbao ningependa nitumie hiyo 2×3 lkn mkuu nakwama mfuko so naishia hapohapo kwa 2×2.Hizo 2×6 nadhani zinatumika kwenye kulaza kwenye tofali ili juu yake zikae kenchi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom