Maji ya bahari ya Hindi yaibukia Mjimkongwe Zanzibar na soko kuu la Darajani

Wewe mzinjibar usiwe zuzu eti hali ya kawaida! I can assure you that is a bad signal - Indonesia, Japan and the like they never knew when it's coming. Better watch NaGeo channel and understanding how the unexpected can happen.

Si utumie Kiswahili tu kuliko kukurupuka na lugha usiyoielewa vizuri?

Sasa unataka watu wa expect the unexpected? Kwa kuwa tu wewe unatazama natgeo?
 
Sehemu ile ya darajani hadi hospitali kuu ya mnazi mmoja zamani ilikuwa ni ghuba ya bahari, ikafukiwa ( land reclamation ) kama wanavyofanya waholanzi ( baharesa pia anafanya pale mtoni marine). Mifumo ya mitaro inabidi iangaliwe upya maana masika yakichanganyika na maji kujaa huleta balaa mitaa mingi ya mji mkongwe wa Zanzibar.
 
Bamvua na mvua ni tofauti kabisa.

Hivi hizo shule mlienda kusomea ujinga? Mnasikitisha sana kuwa finyu kiasi hata bamvua hamlijuwi.

Badala ya kuuliza mpate faida, nyinyi kitu hamkijuwi mnaona nimekosea kuandika. Dah!
Hamlijuwi=hamlijui
Hamkijuwi=hamkijui
 
Hao waandishi wa itv itakuwa ni mijitu ya bara na hawakuchukuwa fursa ya kuwauliza wenyeji kuhusu hali hiyo.

Hiyo ni hali ya kawaida sana Unguja wakati wa bamvua kubwa.

Kuna wakati barabara ya forodhani Unguja huwa haipitiki msimu wa bamvua kubwa.

Upo sahihi niliishi kule miaka mingi ni hali ya kawaida sana hasa maji yakijaaa....the same thing maji ya baharini pale salender bridge huwaga yanafika hadi jagwani nyuma ya muhimbili
 
Mmechemsha kwenye bamvua utaweza kwenye hayo?

Yatamke kwa sauti mara tatu hayo maneno huku unajisikiliza. Jibu utalopata fanya siri yako.
Bi faizafoxy sote tunatambua mchango wako katika kuboresha taalum hii ya lugha ya kiswahili hususani hapa jf.
Lakini wewe si mkamilifu kwa mambo yote hivyo pale unapokosea ukubali pia kukosolewa
Huwezi kuhalalisha kosa la kifonolojia na kulipeleka kiothografia maana yako ni kuwa hata wale wanaotamka "l" badala ya "r"tuwasikilize na kuwakubali katika makosa yao ya kisarufi
 
Hao waandishi wa itv itakuwa ni mijitu ya bara na hawakuchukuwa fursa ya kuwauliza wenyeji kuhusu hali hiyo.

Hiyo ni hali ya kawaida sana Unguja wakati wa bamvua kubwa.

Kuna wakati barabara ya forodhani Unguja huwa haipitiki msimu wa bamvua kubwa.
Malizia....... na ule ukili wako inakuwa tabu kuuanika
 
Hivi visiwa taratibu vinaaza kupungua size japo baadhi ya watu wanaona kawaida Siku zijazo watashangaa kuona mwenzi mzima mji hayajarudi katika hali yake ya mwanzo.
 
Wacha kiherehere, usome uzi utapata majibu kuhusu mijitu ya bara.

Zimezama nyingi sana kabla ya Zanzibar, hiyo wala isikutishe.
Kiherehere kilichokuzidi wewe. Eti soma Uzi , uzi ndio wenye majibu ya kejeli zako. Hivi watu wa bara wakianza kuwasema watu Wa Zanzibar jamani itakuwaje Yesu wangu! hebu niishie hapa maanake sijui hata kama kuna msamiati wake! Aidha kuna waungwana kwelikweli kiasi kwamba nisingependakuwa kwaza.Wewe sijui ni mbegu ya wapi?
 
Kwa hiyo uswahili utakufisha peponi? Nauliza tu mswahili. Hivi uswahili nao umekuwa sifa si huwa nasikia humo maofisini ni tusi sasa huyu veterani yeye anajivunia duhh mamii veterani nijuze
 
Bahari munaifukia maruhubi je maji wapi uatakwenda serikali haijuwi wajibu wake na wasomi pia ovyo
 
Bamvua ni hali ya kujaa na kupwa kwa maji ya baharini, hasa kujaa sana kuzidi usawa wa sakafu ya ardhi inayoungana na bahari. Mara nyingi neno hili hutumika na watu wa pwani na wavuvi wa pwani ya bahari ya Hindi. Kwa kawaida bamvua hutokea mara mbili kwa mwezi.

Bamvua inaonekana kutokana na hali ya mwezi kuwa ama mwezi mwandamo au mwezi mpevu na karibu na siku hizi bamvua inatokea.
Kutegemeana na tabia za pwani mara nyingi bamvua haionekani sana yaani maji hujaa sentimita chache juu ya uwiano wa kawaida. Lakini kwenye mlango wa bahari kwa mfano kati ya kisiwa na bara, au katika mdomo wa mto tofauti inaweza kuongezeka hasa ikiungana na upepo mkali wa kuelekea bara.
-Taarifa hii imepatikana kwa msaada wa Wikipedia

Waambie wa Mkoani,maana wamekuja kwa mbio za Dar es Salaam na Maghorofa lakini hawana walijualo.
We unaishi Pwani hujui Bamvua?aisee,kaazi kweli
 
Back
Top Bottom