Maisha ni safari kadri unavyosimama sana ndivyo unavyojiongezea kuchelewa kufika

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Feb 4, 2024
304
807
UKIANZA KUFANYA MAMBO KUKIMBIZANA NA UMRI JUA KUNA KITUO SIO CHAKO ULISIMAMA SANA

Akitokea mtu anakwambia alimaliza shule ya msingi na miaka 20 jambo la haraka ambalo kama usipomuuliza basi utajiuliza ni hili "KIPI KILIMCHELEWESHA?

MAISHA NI SAFARI KADRI UNAVYOSIMAMA SANA NDIVYO UNAVYOJIONGEZEA KUCHELEWA KUFIKA.

Huwezi kukwepa kusimama njiani kwa sababu kuna muda utasimamishwa na uhalisia wa maisha ila kibaya zaidi ni kujisimamisha mwenyewe kituo kimoja kwa muda mrefu ilihali bado una safari ndefu mbele.

SEHEMU ULIYOSIMAMA SANA NDIO LEO HII INAFANYA WATU WAKUONE UMECHELEWA

Ukianza biashara baada ya kustaafu watakwambia ulikuwa wapi kipindi upo kazini?

Wanakuona umechelewa kwa kanuni hii UMRI WAKO+ NAFASI ULIYOKUWA NAYO NA MAFANIKIO ULIYONAYO SASA.


Sio vibaya kuangalia umri wako na kisha jikimbushe kuwa kuna vituo hutakiwi kusimama sana kwani bado una safari kubwa.

Mwanasayansi Saul kalivubha
Instagram@fikia ndoto zako
 
Bora anaesimama atachelewa kufika, kuliko anaekimbia na anapo kimbilia apajui, akipotea anapotea haswaa
 
Ni kweli kabisa mwalimu suala la mafanikio ni fumbo ila waonaje mtu mwenye miaka 70 akiwa bize kutaka kuanza biashara?
Inawezekana,who knows!? Ukute Mungu akampa miaka 90 ya kuishi duniani,utasema amechelewa?yupo mwingine akihangaika biashara akiwa na 24 akafa na 30 nae utasemaje?,kila mtu ana muda wake hapa duniani.
 
Back
Top Bottom