Familia ya msanii wa bongo fleva Q Chilla wameamua kuingilia kati mkataba wa msanii huyo na kusema mkataba huo unamfanya aishi maisha magumu kiasi cha kushindwa kuchangia mambo yakifamilia.
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, baba mdogo wa Q Chila amesema kwamba hofu juu ya mkataba ni kwamba haukuwa na ushahidi wowote kwa upande wa Q Chilla hali inayombana na kushindwa kuendelea kimaisha na kushindwa kuwa na nyumba yake.
Amesema familia hiyo imeamua kumuandikia barua bosi wa Q Chillah ambaye ni QS Mhonda kumuomba kubadilisha sehemu mbalimbali ambazo zinambana sana kijana wao kiasi cha kumsababishia kurudi alipotoka jambo linaloweza kumvurugia maisha yake.
Ombi: wasanii jitahidini kuwa na wanasheria ili wawashauri kabla hamjasaini mikataba vinginevyo mtaishia kulalamikia watu huku makosa ni yenu. Acheni ubahili.
Source: EATV