Mahakama yatupa ombi la CHADEMA dhidi Polisi Kuzuia Mikutano ya Kisiasa

Kansigo

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,670
2,156
Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza imetupilia mbali ombi la Chadema la kuruhusiwa kufungua kesi dhidi ya amri ya Jeshi la Polisi la kupiga marufuku maandamano na mikutano ya kisiasa kutokana na maombi hayo kutokidhi matakwa ya kisheria.

Uamuzi huo umetolea muda mfupi uliopita na Jaji Mohamed Gwae baada ya kukubaliana na pingamizi lililowekwa na mawakili wa utetezi, Robert Kidando na Obadia Kajungu waliodai waleta maombi hawakutumia kanuni sahihi kuwasilisha ombi hilo.
 
Utasikia majaji wanatumika na ccm. CHADEMA yetu tunaipenda lakini kwa sasa inaendeshwa kiharakati, it's no more longer original as it used to be. Kazi yake sasa ni kutafuta tu mabifu na vyombo vya dola ilhali walitakiwa watumie vyombo vya dola kama daraja la mafanikio
 
Wataendelea kufanyia marekebisho hadi itakidhi vigezo
 
Wameambiwa wamekosea vifungu tuu vya sheria waliyotakiwa wavitumie wakati wanapeleka malalamiko yao. Hivyo wameambiwa walitakiwa watumie kifungu gani badala ya kifungu gani... Hivyo wakili wao amesema watalifanyia kazi hilo then watapeleka tena. Kwani wameambiwa eidha wakate rufaa kama wanaona hawajatendewa haki, au wapeleke mashtaka upya wakishafanyia marekebisho ombi lao...
Sio kwamba ni mwisho, ila kama wataona inafaa wanaweza wakapeleka upya ombi lao likiwa na marekebisho...
Ukienda muungwana blog utaipata hii kiurefu....
 
Yatizo sio cdm
Tatizo kuna injini ya treni mbovu [Mbowe]
Kazi mnayo

Badilisheni usafiri hasa injini imechoka
 
Chadema wamejikosesha makusudi ili ku-buy time kuona polisi watafanya nini siku ya mkutano wa CCM. Chadema endeleeni kufanya delaying tack ticks ili double standard ya polisi na serikali ya Magufuli kwa ujumla wake dhidi ya UKAWA izidi kudhidhihirika zaidi.
 
Inakuwake CDM yenye wanasheria mahiri wamapeleka shauri lisilofuata sheria?
 
Ccm watafanya KIKAO ( tena ni ndani wakiwa wao wenyewe )
Chadema walifanya MKUTANO ambao unawakusanya watu mbalimbali nje, kukiwa na maspkia na wanaohutubia wakipaza sauti. Wanaweza wakawatoka hapo....
Ila pia unakuja unaunganisha na lile la Mahafari ya CHASSO kule dodoma...
Ila nashangaa mbona dom walitawanya wakati Dar waliiacha?
Hayo ni mawazo tuu na maswali ninayojiuliza nikiunganisha hili la ccm na chadema.....
Sie wengine ni waangalia movie tuu, si wakereketwa wa pande zozote kati ya hizi panda hasimu....
 
Endeleeni kujifariji
 
Inakuwake CDM yenye wanasheria mahiri wamapeleka shauri lisilofuata sheria?
Aaah sijuwi.... Huyo huyo mwanasheria makini unayemjuwa wewe karekebishwa na hajalalama, ila kasema watafanyia marekebisho kama walivyoelekezwa na jaji na watapeleka tena... Tena huyo mwasheria anaitwa mallya....
Wao walitumia kanuni ya tano kifungu kidogo cha tatu, badala ya kanuni ya tano kifungu kidogo cha pili ambacho ndicho kilichotakiwa kutumiwa katika kupeleka maombi yao...
Na hii inatokana na pingamizi lililowekwa na mawakili wa serikali ambao wao ndio waliokosoa kuwa hawa jamaa hawakufuata utaratibu uliotakiwa katika kufikisha ombi lao hilo, na kuitaka mahakama kutupilia mbali ombi hilo, na jaji akaona ni kweli na kuamua kutupilia mbali ombi hilo na kuwapa ushauri ni kifungu gani walipaswa kutumia...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…