ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 58,966
- 69,638
Ana Kanisa kabisa huyu 🤣🤣Mchungaji wa mchongo
Analo kanisa na ndilo Neema analosali.Ana Kanisa kabisa huyu 🤣🤣
shetani anafurahi sana kuleta mada hii ili kuwapofusha macho wanadamu waamini kuwa kutoa fungu la kumi sio sahihi. hii ni nyenzo anaitumia kuwarudisha nyuma kutoa fungu la kumi. ukweli ni kwamba, duniani hasa katika makanisa yetu wapo wachungaji wanaotumiwa na Mungu na wapo waongo na matapeli pia, wamejichanganya kwa ajili ya kupata kitu. hilo halimaanishi kuwa wachungaji wote ni waongo au kutoa fungu la kumi ni kosa. hilo ni agizo la Mungu na wale tu waliokutana na Mungu wakalijua hili ndio wanajua ninachokisema. toeni fungu la kumi, ila toeni mahali sahihi, usitoe kila mahali tu kwasababu unaweza kujikuta umetoa hata kwa mashetani au maajenti wa shetani kama hao wauza mafuta na manabii wa uongo wa arusha na kwengine. toa mahali Mungu wa kweli anaabudiwa, hasa pale ambapo unalishwa chakula chako cha kiroho. ni agizo la Mungu na hata shetani akileta makandokando kulichafua, litabaki hivyo milele.My Take
Wachungaji wa Makanisa ya Voda fasta tafuteni kazi za kufanya badala ya kutapeli Waumini Kwa visingizio vya Zaka za bwana.
====
Mgogoro wa ama ni mkopo au sadaka ya fungu la kumi (zaka) baina ya Mchungaji John Mtuka wa Kimara na muumini wake, Neema Wawa umehitimishwa na Mahakama Kuu ikibainisha ni mkopo unaostahili kurejeshwa.
Muumini huyo alimfikisha mahakamani mchungaji huyo akimdai Sh15 milioni alizomkopesha, huku mchungaji huyo akidai fedha hizo hazikuwa mkopo, bali zilitolewa kama sadaka ya fungu la kumi kwenye kanisa wanaloabudu (halikutajwa), shauri ambalo limefika hadi mahakama kuu.
Hata hivyo, katika hukumu yake, Jaji John Nkwabi wa Mahakama Kuu ya Tanzania masjala ya Dar es Salaam, alisema fedha hizo, hazikuwa fungu la kumi wala sadaka ya ujenzi kama mchungaji alivyokuwa anaeleza, bali ulikuwa ni mkopo.
Hayo yamo katika hukumu ya Jaji Nkwabi iliyotolewa juzi kuhusu rufaa ya kesi iliyokuwa imekatwa na Mchungaji Mtuka, akipinga hukumu ya mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ya Agosti 2, 2022 iliyompa ushindi Neema Wawa.
Katika hukumu hiyo, Jaji Nkwabi alianza kwa kusema rufaa hiyo inashangaza kwa sababu wadaawa walikuwa na mahusiano ya mchungaji na muumini na muumini alikuwa akihudhuria kanisani ambako mchungaji aliweza hadi kufahamu ukwasi wake.
“Ilitokea pale uwezo wa kifedha wa mjibu rufaa (Neema) ulipokaa sawa, mrufani (mchungaji) alifahamu kupitia fungu la kumi alilokuwa akilitoa, suala ambalo kiukweli ndiyo mahitaji ya mafundisho ya dini,” alieleza Jaji.
“Wakati mchungaji anadai muumini wake alilipa Sh5 milioni kama fungu la kumi, muumini wake anasema alilipa tu Sh1 milioni kama fungu la 10. Kwa maoni yangu utata wa hii kesi ulianzia hapa, ukichanganya na madai ya michango ya ujenzi,” alisema.
Mwananchi
Kama wewe ndio yule mchungaji kalipe deni acha porojoshetani anafurahi sana kuleta mada hii ili kuwapofusha macho wanadamu waamini kuwa kutoa fungu la kumi sio sahihi. hii ni nyenzo anaitumia kuwarudisha nyuma kutoa fungu la kumi. ukweli ni kwamba, duniani hasa katika makanisa yetu wapo wachungaji wanaotumiwa na Mungu na wapo waongo na matapeli pia, wamejichanganya kwa ajili ya kupata kitu. hilo halimaanishi kuwa wachungaji wote ni waongo au kutoa fungu la kumi ni kosa. hilo ni agizo la Mungu na wale tu waliokutana na Mungu wakalijua hili ndio wanajua ninachokisema. toeni fungu la kumi, ila toeni mahali sahihi, usitoe kila mahali tu kwasababu unaweza kujikuta umetoa hata kwa mashetani au maajenti wa shetani kama hao wauza mafuta na manabii wa uongo wa arusha na kwengine. toa mahali Mungu wa kweli anaabudiwa, hasa pale ambapo unalishwa chakula chako cha kiroho. ni agizo la Mungu na hata shetani akileta makandokando kulichafua, litabaki hivyo milele.
mimi ni mwanasheria ndugu, wala sio mchungaji, ila huwa natoa fungu la kumi, kanisani kwetu. wala hukuwa na haja kupotez amuda kuandika hilo swali.Kama wewe ndio yule mchungaji kalipe deni acha porojo
Hapo mahali sahihi ambapo watu wote tunakubaliana kwamba hapa ndio sahihi ni wapi?toeni mahali sahihi