Kwa mwonekano wa nje hii mahakama inaonekana kama kitanzi kwa mafisadi papa, kinyume chake kitakuwa kilio kwa watu wanyonge wasio na hatia, wasio na majina, wasio na uwezo wa kuhonga majaji.
Litakuwa kaburi kwa watu walioonekana na watakaoonekana kwenda kinyume na wateule, hawa ni pamoja na walio ndani ya CCM.
I bet, mbele ya mahakama hii kutakuwa na uonevu wa hali ya juu kwa wafanyabiashara kutaifishwa mali zao kwa vile tu huyu alinihujumu kwenye uchaguzi au huyu sio mwenzetu.
Uonevu kwa wanasiasa 'wa pande zote', uonevu kwa wanaharakati na watetezi wa haki za binadamu kwa kisingizio cha kutoa maneno ya uchochezi.
Uonevu kwa watumishi wa umma, wakurugenzi wa mashirika kwa kisingizio cha kufisadi miradi kwa dhana ileile ya yule si mwenzetu.
Mahakama hii lazima iangaliwe kwa jicho la tatu.
Mwenyewe kasema atawalinda wastaafu, kwanini basi usijiulize hii mahakama imeundwa kwa ajili ya akina nani?
Na je kama itathibitika mbele ya mahakama hii mtuhumiwa alitenda kosa kwa maelekezo ya mstaafu aliyeapa kulindwa unategemea haki kutendeka?
Wait and see.
Kuna ile habari ya "mtego wa panya kuingia waliomo na wasiokuwano"! Kama sheria hii imetungwa kwa nia ovu ikiwalenga watu fulani, wajue wazi kabisa kwamba sheria ni msumeno na itakapoanza kukata watajikuta wamo wengi zaidi ambao hawakuwalenga na hawakuwatarajia, na wachache sana kati ya waliowalenga! Ni swala la muda tu!