Mahakama Kuu Kenya kuzuia madaktari wetu kuajiriwa kwao: Watanzania tumejifunza nini?

Africa /Kenya /Tanzania kuna mahakama? semeni tu hamtaki kazi kama kawaida ya watanzania ,hivi mnafikiri Kenya kuna engineers wangapi hawana kazi au wanaachishwa kazi na wanakuwa replaced by foreigners? unafikiri kama issue hii ingetokea Tanzania hao majirani zetu wasingekuja Tanzania kufanya kazi eti wasubiri Tanzania imalize mgogoro na madaktari nchini, uhuru amenegotiate nao hao over 3months unafikiri hakujua kama kuna madaktari 1400 Kenya hawana kazi? alipokuwa anafanya nao makubaliano hicho chama cha madaktari ndo kwanza ni wahusika wakuu katika makubaliano hayo walikuwa wapi kumueleza uhuru bhana kama hawa hawataki kazi basi ajiri hawa wasiokuwa na kazi ,sisi tunachofuata ni serikali imesema nini, tuchosikiliza ni raisi wao kasema ni basi hayo mengine ya court watajua wenyewe, wamezoea migomo isiyo na tija ,wanataka pesa nyingi bila kufanya kazi sasa chama cha mdaktari wa Kenya wanaona aibu na wanajisikia vibaya kuwaona watanzania kwenda kutoa huduma kwao.
Jua pia kuna ethical laws za fani ya udakitari! Kulingana na maelezo ya Wizara,wangepeleka ambao hawajapitia Internmship ya kufuzu udakitari. MAT ni registered organ inayoisaidia Wizara kuregulate medical ethics za kazi ya udakitari. Kama walivyosema, sifa ya kuwa na kuruhusiwa kufanya kazi ya udakitari ni kupitia internmship kwa muda kadhaa. Now look how such decision of sending inappropiate docs was contradictory!
 
Hivi karibuni Mamlaka za juu nchini ziliafiki ombi la Waziri wa Afya wa Kenya juu ya ajira ya madaktari wetu. Madaktari hawa wa Tanzania walikuwa waajiriwe Kenya kuziba pengo la Madaktari wenzao wa Kenya waliogoma. Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kilipinga hatua ya kuruhusu madaktari wetu kwenda Kenya kwa sababu kadhaa. Moja ya sababu ni usalama wao kuwa mdogo. Wadau mbalimbali nao walipinga kuwa wasiende kwani waliogoma walikuwa na haki za msingi wanazodai. Hata hivyo,uongozi wa juu wa Serikali yetu,uliziba masikio ,na kuendelea na maandalizi vijana wetu waende! Kwa kitendo cha jana Mahakama Kuu Kenya kuzuia wasiende,tumejifunza nini?
1. Ni walazimishaji mambo?
2. Uongozi wetu wa juu nchini,hauwaamini Watanzania waliotoa maoni yao kuwa wasiende?
3. Nani alaumiwe endapo mahakama isingezuia,na wakaenda,wakadhurika?

Tupeane ushauri ili,tusijeaibika tena mbeleni kama ilivyotokea!
Weee vipi kamanda!! Madaktar wenyewe wanataka kwenda kuchangamkia fursa. Au umejitolea utawalisha na familia zao. Tuache uzandiki. Penye fursa wacha watu wafanye maamuzi yao. Hutakiwi kuwaamulia. Ujinga mtupu ulioongea
 
Mahoteli nyingi za kitalii nchini kwetu mameneja wengi ni wakenya na siyo hiyo tu mpaka wasimamizi wa vitengo kazi ambayo watanzania wanauwezo mkubwa wa kuufanya watanzania wakienda kwao hawapati hizo fursa.ni jambo la ajabu wao wamejazana kwetu kila mahali ukieenda humkosi mkenya .sijui kwa huu mfumo kama munganiko wa nchi zaAfrika mashariki una tija maana ni wakenya wanapata ajira Tanzania lkn Watanzania tukienda Kenya ndo hivyo tunazuiliwa
 
Weee vipi kamanda!! Madaktar wenyewe wanataka kwenda kuchangamkia fursa. Au umejitolea utawalisha na familia zao. Tuache uzandiki. Penye fursa wacha watu wafanye maamuzi yao. Hutakiwi kuwaamulia. Ujinga mtupu ulioongea
Kwani tunaposema EAC ni ndugu,si ni pamoja na kusaidiana kutatua migogoro ili fursa za kazi ziongezeke? Sina maana wasiende! Ningependa zaidi tungetuma deligation ya kushauri maelewano,then vijana ndo waende! Usipende kuona una fursa kumpangisha nyumba jirani anayeunguliwa nyumba,nenda kasaidie kuzima moto!
 
Jamaa zangu wengi waliliona hili wala hawakuhangaika nawaonea huruma waliotuma maombi maana walikuwa na matumaini ya kupata ajira baada ya kuona bongo hakuna dalili
 
Hivi rais anaomba msamaha! MTU Gani usiyetaka ushauri? Au kalogwa

Vyama vya wafanyakazi pamoja na taasisi zinazohusiana na wafanyakazi bado Hazina meno ya kutetea maslahi ya wateja wao. Viongozi wako kwa ajili ya mishahara na marupurupu.
 
Nilichojifunza ni kuwa Kenya baada ya kubadili katiba yao imewezesha nchi hiyo kuwa na mifumo na taasisi imara zinazoweza kusimamia haki na uwajibikaji bila ya kuingiliwa na mihimili mingine na hasa serikali. Tanzania ni lazima tufike mahali tukubali kuwa ili nchi yetu ipige hatua kubwa za maendeleo tunahitaji taasisi imara ambazo zitaweza kusimamia rasilimali kwa ufanisi katika kuwaletea maendelo wananchi. Hatuhitaji mtu mmoja awe ndiyo kila kitu kwa sababu kwanza hataweza nchi hii ni kubwa siyo kama vinchi vidogovidogo kama rwanda, burundi etc.

Mpango wa decentralization by devolution ulikuwa ni kitu muhimu ktk kuharakisha maendeleo katika local levels, sasa yeye badala yake ame-reverse amekuja na centralization ambapo serikali kuu sasa inataamia kila kitu.

Hivyo ushauri wangu, siyo vibaya tukiiga kenya kwa kuanza na katiba ya warioba. Kama Rais alivyosema siku anawaapisha kina mwakyembe na wenzake kuwa maisha yako so temporally hivyo ni muhimu kwake aache legacy kwa kutuwekea mifumo na taasisi imara badala ya yeye kujilimbikizia madaraka nadhani atakubalinana na mimi kuwa akiendelea na utaratibu anaoenda nao come 2020 hataweza kuwambia watanzania alichokifanya maana mpaka sasa amekalia kufukuza na kuteua watu as if watu ndiyo watakaomsaidia kumbe kinachotakiwa ni ku-strengthen the government systems and institutions.
 
Jua pia kuna ethical laws za fani ya udakitari! Kulingana na maelezo ya Wizara,wangepeleka ambao hawajapitia Internmship ya kufuzu udakitari. MAT ni registered organ inayoisaidia Wizara kuregulate medical ethics za kazi ya udakitari. Kama walivyosema, sifa ya kuwa na kuruhusiwa kufanya kazi ya udakitari ni kupitia internmship kwa muda kadhaa. Now look how such decision of sending inappropiate docs was contradictory!

Ndugu yangu Tanzania kuna madaktari wengi sana ambao wamemaliza attachment na wapo mitaani wakisubiri ajira, mtu akiwa amemaliza attachment ( internship ) maana yake ameshafuzu na tayari anasifa ya kufanya kazi popote , na hao wanaaokwenda kutoa huduma nchini Kenya ,lakini pia hata madaktari waliokuwa kwenye private sector ambao wanaweza packages ya Kenya iko vipi basi wao pia wanaruhusiwa, hivyo tunapeleka madaktari wazuri ambao ni well recognized by MAT. By the way hao wakenya unafikiri udakatari wao una jipya lipi hapa duniani? wote ni gale gale tu kama wetu, ni operation ipi ya kutisha imewahi fanywa Kenya na madaktari wazawa kama sio hizi hizi tu kama za bongo?. Hii ni EAC bhana, upande mmoja ukikwama unaangalia updande mweingine within EAC block mnapojipanga, au EAC block just for Kenyans kwenda nchi zingine kufanya kazi? alichofanya uhuru ni sahihi kabisa kwa kujua uhusiano wa kikanda hivyo kutoa nafasi kwa vijana wa kitanzania kufanya kazi maana mwanzoni walidai wataleta madaktari kutoka india or cuba nahisi baada ya analysis zao wakagundua gharama itakuwa kubwa ndo wakaja Tanzania.
 
SERIKALI YA TZ IMEASHINDWA KUWA AJIRI MADAKTARI WETU NDIYO MAANA WAKAAMUAWAWAPELEKE HUKO KENYA...MADAKTARI WETU WAMEINGIZWA MKENGE TU.....NA ZIS GOVERMENT

OVA
 
Kenya wana uzalendo na wanatetea maslahi ya wakenya. Kule wanadai nyongeza ya mishahara na maslahi bora. Hata wakenya mawakili na majaji wanatambua umuhimu wa maslahi bora kwa dr mkenya

Sasa hapa unaajiriwa kampuni ya mwekezaji mkubwa mfano acacia lakini mswahili mwenzio HR Superintendent anaungana na wazungu kukupunja mshahara. Tazama kampuni kama unilever angalia Area sales manage mkenya na mtanzania wanavyolipwa ndio utajua wenzetu wanajielewa
 
Hivi karibuni Mamlaka za juu nchini ziliafiki ombi la Waziri wa Afya wa Kenya juu ya ajira ya madaktari wetu. Madaktari hawa wa Tanzania walikuwa waajiriwe Kenya kuziba pengo la Madaktari wenzao wa Kenya waliogoma. Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kilipinga hatua ya kuruhusu madaktari wetu kwenda Kenya kwa sababu kadhaa. Moja ya sababu ni usalama wao kuwa mdogo. Wadau mbalimbali nao walipinga kuwa wasiende kwani waliogoma walikuwa na haki za msingi wanazodai. Hata hivyo,uongozi wa juu wa Serikali yetu,uliziba masikio ,na kuendelea na maandalizi vijana wetu waende! Kwa kitendo cha jana Mahakama Kuu Kenya kuzuia wasiende,tumejifunza nini?
1. Ni walazimishaji mambo?
2. Uongozi wetu wa juu nchini,hauwaamini Watanzania waliotoa maoni yao kuwa wasiende?
3. Nani alaumiwe endapo mahakama isingezuia,na wakaenda,wakadhurika?

Tupeane ushauri ili,tusijeaibika tena mbeleni kama ilivyotokea!

Mi nimejifunza kuwa:
1) vijana wote waliotoa maisha yao kwenda kutumikia ndugu zetu wa Kenya waajiriwe na wizara yetu ya afya mara moja!
2) Timua nyang'au wote waliojipenyezapenyeza kwa ajira zetu na acha kabisa kuamini upuuzi yao mara ingine!
 
ww ndo mpuuz kabisa au unadhan kenya nao wanaendesha nchi yao kidikteta kama tz? ww umeskia mahakama ishakataa unadhani serekal inaweza kuwapuuza kama serekal ya magu inavyopuuza mahakama zetu?
Mpuuzi wewe na fikra zako. Serikali ya kenya ndio itakayotoa taarifa ya kusimamisha zoezi linaloendelea hapa Tanzania.
Mahakama haiwezi kutoa uamuzi bila kuwapo mtu aliyeenda kulalamika. Hivyo serikali ya kenya ndio itakuja kusema tumeshindwa kesi hivyo zoezi lisimame. Tanzania haina itakachopungukiwa kwani huu ni msaada na kama anayesaidiwa akisema asante inatosha basi. Tatizo nyie wakosa akili mmeona nalo la kufanyia ligi. Kweli ukiwa chadema lazima uwe tahira halisi au hata wa kuigiza
 
Nimejifunza kuwa taaluma ya udaktari huko Kenya imeingiliwa na siasa
Watu wapo radhi wananchi wafe kwa kukosa huduma za afya kwa kujali maslahi yao.
Madakari wa kenya waligoma miezi mitatu,wakarudi wakadai hawawezi kazi kuna upungufu wa madaktari,Serikali yao ikaona isiwe taabu,wakaomba madktari Tanzania.Madakyari wa Kenya kwa kuwa shida yao ilikuwa ni kuyumbisha serikali yao tuu,wakaanza figisu,ooh hakuna haja ya kuleta madaktari toka Tanzania
 
Back
Top Bottom