Magufuli's government switching costs to citizens

nchonga aliyebaki

JF-Expert Member
Mar 21, 2017
574
833
LEO NTATOA SOMO KIDOGO:

TAFADHALI SOMA UJUMBE WOTE UELEWE

GOVERNMENT SWITCHING COST: Madhara au mateso yatokanayo na kubadili mfumo kutoka mfumo usio sahihi kwenda mfumo halali,

Katika nchi ya Tanzania kumekuwepo na watu kuish kwa ujanja ujanja bila kufuata taratibu husika,
Short cut zilizojaa rushwa zilikithiri mpaka watu wakazoea kuish maisha ya ujanja ujanja, bila kufuata taratibu husika,
Ndiyo maana malalamiko ya ugumu wa maisha hasa kwa wajanja wajanja yameshamili.

Sasa katika nia ya dhati ya kubadili kutoka mfumo ujanja kuja uhalali,

Lazima waguswe wakwepa kodi, wauza pembejeo kwa upendeleo, wahujumu uchumi, wahujum hela ya mikopo ya elimu ya juu,

Kwa tathmin ya haraka inaonesha kuanzia mwaka 2007-2016 asilimia 74 ya watanzania waliishi maisha ya ujanja ujanja wa kukwepa kodi, au utapeli, au kujipa malipo yasiyo halali,

Asilimia 30% ya wachumi tanzania yaan wakubwa walikwepa kodi sana na kutokana na ukwepaji kodi wa hao watu ulinufanisha 90% ya watanzania kwa kupata bidhaa kwa bei ya chini kwa kuwa haikulipa kodi,

40% ya maliasili za Tanzania zilipelekwa bila kurekodiwa mahali popote ama kupitia njia ya anga , majini au ardhi, kubana maeneo haya kumesababisha tu sikilizie madhara ya Ku switch (kuhama) kutoka mfumo wa ujanja kwenda mfumo halali,

48% ya hela ya kwenye mzunguko haikuwa halali hii ilitokana na kutolewa mikopo ya biashara kutoka taasisi za serikali kwenda watu wasiostahili wasio na sifa stahiki,
Mishahara hewa ambayo iliwaendea watu ambao hawana sifa ya kuipata na saa Nyingine walipokea malipo zaid ya kazi walofanya, ilifanya mzunguko wa hela kuwa sivyo hela ilionekana kuwepo lakin baada ya kubanwa wakaumia wasio na nia njema na Tanzania, na madhara yake ni makubwa sana,

70% ya waliokuwa wanapata ajira hawakuwa na sifa stahiki, kigezo kilichotumika ni rushwa ,kujuana, na kupendeleana tu , wakati watu wenye sifa stahiki wanabaki,

60% ya bajet ya nchi ilitegemeam misaada bila kujua madhara yake,

UJIO WA MAGUFULI
Ujio wa bwana mkubwa huyu umesababisha hela yote hiyo kukauka maana haikuwa halali, madhara haya yakawa makubwa maana hakuna hela mtaani ni kwasababu hatujazoea kupata kipato halali, ni upigaji tu hivyo inakuwa ngumu kwa sasa kuendana na mfumo huu, na ajira za ngono ,kujuana , kupendelea hakuna tena hii imedababisha watu kusema hata hakuna ajira,

MUDA WA MADHARA
Muda wa madhara haya utaendelea kuwepo mpaka mwaka 2018 may ndipo watanzania watakuwa wemezoea kujipatia kipato halali, ndipo watanzania watakuwa tiyari wamezoea kuwa ajira so kujuana ni vigezo,

Ndipo watanzania watakuwa washajua kuwa ni lazima wawe na vigezo na kuimarisha vigezo vya kupata pesa toka taasisi husika, maana taasisi zilisitisha kwa muda kwa kuhofia wale wauza madawa ya kulevya, au wanaojilipa malimbikizo yasiyo na tija na kujipatia mikopo kama watapata fursa tena,

MAISHA KUWA MATAMU

Maisha ya watanzania yatakuwa mazuri kuanzia July 2018, maana watazoea mfumo na watakuwa wamesharudi kwenye msitari husika,

Vijana wengi watakuwa wameshajua kuwa siyo jukumu la serikali kuwapa ajira wahitimu wote,watakuwa wameshapata njia mbadala,

Huduma za jamii zitaimarika zaidi kutokana na vipaumbele vya bwana mkubwa kujikita kwenye Huduma za jamii kwa ujumla kuliko MTU mmoja mmoja,

YAPI YANGEKUWA MADHARA KAMA MAGUFULI ASINGEBADILI MFUMO?
1. Tanzania ingefilisika kwa kudaiwa kila sehem maana tungeshindwa hata kulipa madeni wanayotusaidia kujazia bajeti,

2. Tanzania ingekuwa mikononi mwa wagen zaid,kama kuwalipa fidia ya madeni wanayotupa kujazia bajeti, au kupitia misaada yenye mashart magumu, baadhi ya taasisi nyeti zingepaswa kuwekwa rehani,

3. Wizi au utapeli wa kimataifa miongoni mwa vijana wanaosoma na kupata elimu ya juu alafu nafasi zao zinachukuliwa na wasio na vigezo, maana hao ma IT na wana mitandao wangecheza na taasisi za fedha na miamala isiyo halali, na pia ingesababisha wenye akili mbadala.wengi mtaani,

4. Makundi ya vijana waliochoka maisha wangejitokeza na kuanza uarifu hadharani, na kusababisha uaribifu,

SIFA ZA WANAOMCHUKIA MAGUFULI

kama unamchukia Magufuli utakuwa katika kundi mojawapo hapa

1. Wakwepa kodi
2. Wahujumu uchumi
3. Wafanya biashara haramu,
4. Wajanja wajanja wasiopenda kufanya kazi,
5. Chuki binafsi tu
6. Wapinzani wanaotafta huruma ya wananchi , maana ni lazima wapinge,

Hayo ndo madhara ya SWITCHING,

TUVUMILIE NEEMA YAJA,

By
Raia Mpenda Haki
 
Umegusa pande zote na huo ndio ukweli.
Hii Darasa ungenunua airtime kwenye TV na Radio ili watanzania wapate ukweli
 
Acha kua kama haujaenda shule mabadiliko anayoyafanya raisi ni ya mtu mmoja kama anazo busara atengeneze mfumo imara kisheri kuzuia hio mianya maana siku atakayoondoka madarakani kila kitu kitarudi kama kilivyokua
 
Kivip
Acha kua kama haujaenda shule mabadiliko anayoyafanya raisi ni ya mtu mmoja kama anazo busara atengeneze mfumo imara kisheri kuzuia hio mianya maana siku atakayoondoka madarakani kila kitu kitarudi kama kilivyokua
 
Huu ni ukweli usiopingika.

Mtoa uzi natamani kukupa ofa kwa sababu ulichoeleza NI KWELI TUPU.

Hakuna kama Magufuli......God bless our President.

Wataelewa baadaee.
 
Porojo @ work. Hizo asilimia umezito National Bureau of Statistics au unaongea ukitokea kijiweni kwako kijitonyama kwa ally maua?
 
Kama suala lenyewe ni dogo hivyo mbona nguvu kubwa sana inatumika?, maana hao uliowasema wamezoea kuishi kiujanja ni sehemu ndogo saana ya raia wa Tanzania na Sidhani kama wanazidi 2mil, ambao ukiamua kudeal nao kwa dhati haiwezi hata kudhidi mwaka1..

Kinachowasumbua asilimia kubwa ya watanzania ni umasikini na huu ndio ukweli, na kwa asilimia kubwa umasikini huu wa watanzania umesabishwa na mamlaka za kiuongozi kushindwa kujenga mifumo itakayoikwamua nchi na wananchi wake kiuchumi.. Moja ya mifumo ambayo imeleta na inaleta shida kwa watanzania ambayo kimsingi ni kazi ya serikalI ni Elimu duni na isiyotosheleza mwishowe inazalisha wasomi hewa, kilimo cha hovyo kilichopitwa na wakati na kisichozingatia faida ( mifumo ya kilimo cha umwagiliaji), Afya - idadi ndogo ya wahudumu na vituo vya afya na ukosefu wa vita vya afya na wataalamu wa kutosha wa afya ambao wangewezesha uwepo wa watanzania wengi wenye afya ya kiakili....

Ili Tanzania iondokane na matatizo yake iliyokuwanayo suluhu ni kujenga mifumo itakayowezesha kuondoa umasikini kwa Tanzania na jamii yake, Mifumo itakayowezesha kupatikana kwa elimu bora miongoni mwa watanzania, mifumo itakayowezesha afya nzuri ya kiakili kwa watanzania, mifumo itakayowezesha ukulima bora na wa kisasa unaozingatia biashara, mifumo itakayowezesha ajira kwa watu wasahihi sehemu sahihi...
 
Weka za kwako tuone usipinge bila kuwa Na data, watu tuna data Na ni wasomi nguli , tunajua jinsi ya kufanya research, kwani we unategemea data za national statistics only?
Porojo @ work. Hizo asilimia umezito National Bureau of Statistics au unaongea ukitokea kijiweni kwako kijitonyama kwa ally maua?
 
Hebu shusha hizo data za waajiriwa asilimia kubwa hivyo kwamba hawana sifa. Na hizo nyinginezo. This is exaggeration at its best.
 
mtoa maada uko sawa kabisa. ila kuna kitu kimoja umesahau BASHITE.

swala la bashite linaondoa kabisa kama si kumaliza jitihada za Mheshimiwa na kuonekana ni unafki. maana kama ni rushwa bashite yumo na ushahid umewekwa. kama ni madili nae yumo na ushahid umewekwa, sasa sielew mkuu anashughulikiaje wengine wakati wa karibu anawaonea haya.

kimahesabu +*+*+*+*-=-
 
Ni sahihi kwamba nchi ilikuwa na mfumo usiofaa kiuchumi na kimaisha lakini kudai au kuamini kwamba yanayofanyika sasa hivi ni maandalizi ya mambo kuwa sawa ifikapo 2018 ni aina nyingine ya udhaifu wa fikra.
Umewahi kusikia economic strategy yoyote toka kwa Magufuli? Katika mazingira ya namna hii ambayo nchi kimsingi imekufa unawezaje kudhani itafufuka baada ya mwaka mmoja kutoka sasa? Kwa misingi ipi? Sekta binafsi ambayo ndiyo ingeleta kodi kwa wingi inauawa kila siku, idadi ya wasio na ajira ni kubwa kuliko katika kipindi chochote, serikali haina hela za shughuli za maendeleo ambazo ndizo zingechangia ku-stimulate ukuaji wa uchumi, serikali ambayo kwenye kila nchi ndiyo mteja mkuu kwenye uchumi imezuia hela halafu unataka kuaminisha watu kuwa haya ni maandalizi ya mafanikio baada ya mwaka mmoja?
Halafu acheni kuwasakama watu na kudai kuwa kila anayeumia alizoea kupiga madili wakati mpaka sasa kwa mujibu wa ripoti ya CAG madili bado yanapigwa tu.
Be wise and use your head if at all it has anything worth using inside it.
 
atengeneze mfumo imara kisheri kuzuia hio mianya maana siku atakayoondoka madarakani kila kitu kitarudi kama kilivyokua
Ni kweli kabisa mkuu,bila kufanya hivyo itakuwa ni sawa na kukitafuta kiuno cha nyoka.
 
MAgu is doing right kwenye baadhi ya mambo...but kuna machache sana halafu hayana ulazima kabisa ndo anabugi kwa mfano swala la vyeti feki ni right call but kumuacha bashite imeharibu mchakato wote. Swala la ndege ni zuri lakini kununua tatu kwa muda mfupi wakati sekta ya kilimo na afya zinasua sua, ni jambo zuri lililofanyika kwa wakati usio sahihi. Kuzuia siasa za majukwaani inampotezea credits, watu hatuli maandamano lakini jua yakitokea na nyie hamtakula. Waache wapinzani wafanye kazi yao yale mazuri yachukue yafanyie kazi mbona hutatumia nguvu kuleta watu kwenye matamasha?for now magufuli yuko right 80% but 20% anayobungi ndo inachafua yote mazuri anayofanya the only way ya kuwin back ni kurekebisha hayo madhaifu na sio kuyafunika.
 
Wenye nia nzuri ya mabadiliko ya kudumu hubadili mifumo, katiba na sheria. Maneno haya ataondoka miaka 10 si haba tutarudi tena kulekule tulikokimbia.
 
Katika kitu ambacho leo ningeambiwa nimshauri Rais ni kuhusu swala la mikopo ya Bank.
1. Kama BoT haiwezi kuwekeza kwa kutoa mikopo nafuu kwa benk bora waruhusu benk kukopa nje ili zikopeshe kwa riba ya chini
2.Uchumi utakua kama kodi zetu zitaendana na kipato cha mwananchi.Hivyo biashara zitakazo tokana na mikopo zitakua na kuleta positive effect kwenye uchumi wa Nchi.
3. Bora kuwa na kodi rahisi ukakusanya kwa wengi kuliko kodi nyingi kubwa zitakazo lipwa na wachache.
4. Mfanya biashara mdogo asaidiwe kukua na si kuchukua kodi hadi anafunga biashara.
 
Acha kua kama haujaenda shule mabadiliko anayoyafanya raisi ni ya mtu mmoja kama anazo busara atengeneze mfumo imara kisheri kuzuia hio mianya maana siku atakayoondoka madarakani kila kitu kitarudi kama kilivyokua
Usiseme hivyo
 
Hapa kuna vita ya kulipisa visasi iliyo jificha kwenye vita ya Ufisadi.

sioni nafuu hapa, huwezi sema kutakuwa na nafuu ilihali kwa sasa tunadaiwa pesa za kuvunja mikataba. Wawekezaji wanaogopa kuja kuwekeza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…