Magufuli Unapoteza Legitimacy Haraka Mno

Acha basi porojo ndugu! Sasa ndo umeandika nini? Muhongo kakukosea nini? Kila siku mwaanzisha majungu! Acha watu wachape kazi. Hakuna mwizi atakayesalia! Hadi Papa la Mafisadi litafikiwa tu!
japokuwa na wwe umeandika pumba ila avatar yako imeniacha hoi...:D:D:D:D
 
Huyu m2 kwa mtazamo wangu kuna vitu atajifanya kuwa amevisahau kuvifanya kabisa. Mfano jipu la Rada, uuzwaji wa nyumba za serikali na mgodi wa Kiwira.
 
Mleta thread hauna akili.

Unataka watu wawajibishwe kwa uzushi?! Kuna mtu anaongoza kwa tuhuma za ufisadi nchi hii zaidi ya mamvi? Mbona mlizungusha mikono na kutaka kumpa nchi?
Tuhuma zipi ? Richmond ni ya Kikwete .
 
Ni kwa sababu unahangaika na dagaa tena kutumia nguvu nyingi huku huku ukiyaacha Nyangumi yakikukejeli. Ungekuwa kweli Musa wa kizazi hiki, anayewapeleka watanzania waliochoshwa na mfumo wa CCM katika nchi ya ahadi, Usingemuacha Prof. Muhongo Kwenye Baraza la mawaziri hasa ukitafakari kashfa zote zinazomuandama, kuanzia Escrow hadi Mafuta Bandarini.

Ungetaka tukuone mwokozi wa watanzania, Basi January Makamba angejiuzulu mapema sana kutokana na tuhuma za rushwa zinazomkabili. Kadhalika Waziri wa Mambo ya Ndani Charles Kitwanga angepisha Uchunguzi kutokana na kashfa nzito ya Lugumi.

Matokeo yake Unapoteza muelekeo kufukuzana mahakamani na kijana asiye na mbele wall yuma kwa kuwa amekuita Bwege. Unapoteza muelekeo kumfukuza Anna Malecela wakati CCM imejaa waua tembo na wafanya bisahara ya kulevya. Mbunge wa Rorya, Lameck Airo amewahi kusema kwamba, nguvu yako ni ya Soda, kweli Nguvu yako soda inakwisha
Hujafuatwa kuulizwa utoe ufafanuzi maana nchi hii kukomalia petty issues they are leading
 
Acha basi porojo ndugu! Sasa ndo umeandika nini? Muhongo kakukosea nini? Kila siku mwaanzisha majungu! Acha watu wachape kazi. Hakuna mwizi atakayesalia! Hadi Papa la Mafisadi litafikiwa tu!
Kujaribu kum-mislead waziri mkuu kwenye ziara yake ya kustukiza bandarini!
 
Back
Top Bottom