Magufuli kuingilia kati uchaguzi wa serikali ya wanafunzi UDOM ni sahihi?

Mtakaopinga agizo mtatafutwa kama sukari na mkipatikana mtafichwa kama sukari. Wasomi mnakuja kulialia mnakosa misimamo? Sasa mnasoma nini kama kujitambua hamjitambua ilihali sheria mnazijua? Mkulima alie nanyi mlie!
 
Kuna vitu navitafakari kwa sauti sivielewi!!!!? What is the motive behind this matter? What remedies is she looking for?
Anataka arudishwe chuo maana amepinduliwa na kufukuzwa bila sababu ya msi ngi, vipi ungekuwa wewe ungeendelea kubung'aabung'aa?
 
Hii haina uhusiano na BAVICHA Rose Maruchu ni mwanafunzi kama wanafunzi wengine amepeleka kesi mahakamani ili apate haki yake ya msingi kwani huyu Dada alikuwa Makamu wa Rais wa college baada ya aliyekuwa Rais wa college Victor Kabyemelwa kufukuzwa chuo bila sababu zinazoeleweka yeye alitakiwa ndiye akaimu madaraka hayo cha ajabu naye akatimuliwa na utawala ukasimika uongozi mpya wakishirikiana na Stella Manyanya na Mwigulu Nchemba, kosa lake lipo wapi Dada wa watu?
Wawaachie CCM watawale... Kitu pekee kitakachokupa furaha maishani ni kuachana na CCM wafanye wanavyotaka na wewe jali maisha yako tu.. Mimi nilishaamua kufanya hivyo maana hizi siasa za Tanzania ni upuuzi tu.. Wewe dada Rose piga kitabu achana na siasa, maliza degree yako uende ukapambane uraiani ambako hutapata kikwazo kitakachokuathiri... Ukitaka ujue siasa za vyuo ni ujinga muangalieni yule aliyekuwa Rais hapo Mwakibinga kwa kupewa kichwa na Bavicha na Zitto na kufukuzwa mara mbili chuo leo hii maisha yake yamekuwa ya ovyo tu na sio Chadema wala huko ACT alikokimbilia wamemsaidia kwa chochote..

Wewe Rose kama unanisoma hapa malizia degree yako rudi mtaani ndio uanze siasa za kiuanaharakati..
 
Kwa mtu asiyejua mambo yanayoendelea UDOM anaweza akalipuuza hili lakini kwa anayejua hili hatashangaa unafikiri kilichompelekea Esther Matiko kuuliza swali kwa waziri mkuu kuhusu siasa vyuoni ni kitu gani? Haya mambo tunayapuuzia lakini imefika hatua tumechoka kuendeshwa haiwezekani mpaka viongozi wa chuo nao wawe makada na makomredi wa chama chuo kinapaswa kijitenge na siasa kuu siyo mpaka Rais wa college apangwe kwenye vikao vya chama dola! Puuzeni leo lakini wasomi tunaowajenga baadaye ni hatari! Mimi imeniuma sana hii.

Nikizipata bunduki....
Kijana labda nikuulize tu, hivi hao wanasiasa wa chuo wanawasaidia nini cha maana hapo chuoni??
 
Kumbe unaelewa kabisa kuwa "..uongozi wa chuo wakishirikiana na tume ya uchaguzi katika college... WANAWATISHA...." Habari ya Rais kuingilia uchaguzi inatoka wapi? au ni Rais wa Wanafunzi?, Umetishwa ukatishika!
Hiyo habari imeletwa na tume ya chss wakishirikiana na utawala
 
UDOSO ni mradi wa watu kujipatia pesa. Hakuna kiongozi anaejali maskahi ya wanafunzi kwa ujumla isipokuwa tumbo lake. Viongozi wapo tena waliomba kuongoza wizara husika lakini cha ajabu unakuta wizara hiyo ndo inafanya madudu, kwa mfano wizara ya afya imeshindwa kuisimamia zahanati inayotoa huduma social sciences matokeo huduma zitolewazo pale ni mbovu mbovu isiyo na kifani, wafanyakazi wanatukana wagonjwa na kuwarundika mapokezi bila kupewa huduma. Wizara ya chakula nayo hovyo. Ile ya mazingira ndo usiseme; mazingira ya nje machafu kupindukia, vyoo ndo usiseme hadi wanafunzi wanaonekana kwenda kujisaidia vichakani kisa matundu mengi ya vyoo yameziba na kufanya mavi kutoka choo cha floor ya juu yavuje kushuka chini kwenye lower floor kitu ambacho ni hatari kwa mtu anayejisadia kwenye lower floor kwani wakati wowote mavi yanatua kichwani kama si mdomoni kwake.
Wanaojiita viongozi wamekalia kugawana pesa za udoso tu badala kutatua kero za wanafunzi. Na hii sababu ya pesa ndo inawafanya kupeleka mapingamizi mahakamani.
Hata mimi hainijii akilini kabisa... Mtu umeenda kusoma, ulishakuwa kiongozi na umebakiza miezi kadhaa kumaliza chuo lakini bado unang'ang'ania uongozi.. Kwani hapo uliufuata uongozi au Degree?? Mbaya zaidi hawa viongozi wa vyuoni hawafanyi chochote kile zaidi ya kuiba pesa ya serikali ya wanafunzi.. Nyie wabunge wa CCM na Ukawa kwa ujumla ndio mnaopeleka hizi siasa za kipuuzi huko vyuoni. Waacheni watoto wasome jamani..
 
mtoa mada..usitumie mtandao vibaya!..Mh.Rais anahusika vipi?aisee unamuonea
 
Kwa mtu asiyejua mambo yanayoendelea UDOM anaweza akalipuuza hili lakini kwa anayejua hili hatashangaa unafikiri kilichompelekea Esther Matiko kuuliza swali kwa waziri mkuu kuhusu siasa vyuoni ni kitu gani? Haya mambo tunayapuuzia lakini imefika hatua tumechoka kuendeshwa haiwezekani mpaka viongozi wa chuo nao wawe makada na makomredi wa chama chuo kinapaswa kijitenge na siasa kuu siyo mpaka Rais wa college apangwe kwenye vikao vya chama dola! Puuzeni leo lakini wasomi tunaowajenga baadaye ni hatari! Mimi imeniuma sana hii.

Nikizipata bunduki....

sema yote, best weapon ni kususia uchaguzi..huko mahakamani, ni mahakama ya nani??
 
Nchi ilivyo Na matatizo mengi hvyo mna zan raisi .. Hana cha kufanya.... Mpaka aingilie uchaguzi wa mwaka mmoja tu .

Grow up Na mfanye kilicho wapeleka chuo...
 
Msimpuuze mleta uzi Siasa nyingi ata wanasiasa na wanamapinduzi wameanzia vyuoni na kuendeleza harakati zao baada ya masomo,kwa hili la kwenda mahakamani ni kutafuta haki sasa kama kuna taarifa nyinginezo kuhusu uchaguzi huo ni vizuri wanachuo wakatumia weledi wao lakini la muhimu zaidi wajikite zaidi kwenye taaluma.
 
Wawaachie CCM watawale... Kitu pekee kitakachokupa furaha maishani ni kuachana na CCM wafanye wanavyotaka na wewe jali maisha yako tu.. Mimi nilishaamua kufanya hivyo maana hizi siasa za Tanzania ni upuuzi tu.. Wewe dada Rose piga kitabu achana na siasa, maliza degree yako uende ukapambane uraiani ambako hutapata kikwazo kitakachokuathiri... Ukitaka ujue siasa za vyuo ni ujinga muangalieni yule aliyekuwa Rais hapo Mwakibinga kwa kupewa kichwa na Bavicha na Zitto na kufukuzwa mara mbili chuo leo hii maisha yake yamekuwa ya ovyo tu na sio Chadema wala huko ACT alikokimbilia wamemsaidia kwa chochote..

Wewe Rose kama unanisoma hapa malizia degree yako rudi mtaani ndio uanze siasa za kiuanaharakati..
ushauri mzr sana..mwakibinga alijitwika siasa sana bila kujali impact ktk masomo yake....alisababisha hata masatu aliyekuwa rais wakati mwakibinga ni pm akafukuzwa....sijui kama walisharudishwa chuoni au bado lakini achaneni na siasa chuoni....unaweza kugombea wakikuzulimu achana nao...soma kwanza upate degree siasa zpo tu
 
Hapo UDOM ni chuo kikuu au ni chuo cha ufundi?

Kama suala la aina hiyo mnashindwa kulikabiri maisha mtayaweza? Pengine wanaotania kuwa hicho ni chuo kikuu cha kata huenda wana mantiki.
 
Hili lina mashahidi wengi maana wajumbe wa Tume ya uchaguzi kwenye college ya CHSS ndiyo wanaosambaza hizi habari kuwa amri imetoka kwa Rais na kwamba ole wetu tupinge!
Hao wajumbe sisi hatuwajui sisi tunacho jua wewe ndio unasambaza habari kuwa Rais kaingilia huo uchaguzi wenu ambao hauna mbele wala nyuma!
Kwa hili bandiko ni kama una mtusi Rais! Kumbuka mchuma janga hula na wakwao ni vyema ukawaomba mods wafute huu ujinga wako lasivyo utashikwa na ni wewe na familia yako ndio mtazunguka mahakamani wewe ukiwa nyuma ya nondo!

Hivi mnapata wapi muda wa kufungua case za kijinga namna hii...mnasoma saa ngapi? Hii linaweza thibitisha kuwa wanafunzi wa Udom wanatumia muda mwingi kufanya siasa badala ya kusoma!
 
Wewe umesikia raisi amesema unakuja kusambaza ujumbe huku, ukiambiwa uthibitishe kama raisi ndo amesema utathibitisha? Kwanini usimuachie huyo aliyekuambia ndo aje asambaze huu ujumbe, kesi zingine tunajitakiaga tu kwa viherehere vyetu.Akili za kuambiwa changanya na zako.

Raisi ndio nani?
 
Sidhani kama mkuu wa nchi anaweza kuhangaikia uchaguzi wa chuo tena Udom, kwa akili ya kawaida tu na utashi halisi, rais ana mambo mengi sana yanayo mnyima usingizi kwa hiyo sidhani kama ana mda wa kufuatilia siasa za watoto wa chuo.

TUSIPENDE KUPOST MAMBO YASIYO YA MSINGI MITANDAONI, UKIITWA KUTHIBITISHA HILO UTAWEZA, UKIKAMATWA NYUMBU WANALALAMA UMEONEWA
 
Back
Top Bottom