Magufuli hafai kabisa kuwa Mwenyekiti CCM

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
20,353
38,580
Kama kuna tamaduni ambayo CCM wanatakiwa waikwepe kwa gharama yoyote ile ni ya kuwa na Mwenyekti ambaye pia ni Rais wa nchi. Mantiki ya kuwa hivyo ilianza wakati ule wa chama kushika hatamu ambapo kulikuwa hakuna vyama vingine vya siasa zaidi ya CCM. Lakini kwa sasa ambapo watu wameshaanza kuona kuna tofauti kati ya chama cha siasa na serikali ni vyema CCM ikatafakari kama wanahitaji kuendelea na tamaduni hiyo.

Siku hizi watu wanaotamka "viongozi wa chama na serikali" wamebakia wachache sana wakiongozwa na Nape. Magufuli mimi namkubali sana kwa uwezo wa kukariri namba lakini sidhani kama ana ladha ya uanasiasa.Hata wakati wa Kampeni waliovutiwa na Magufuli ni wale waliokuwa na kiu ya kuwakomoa wengine lakini siyo kwamba yeye mwenyewe ana mvuto wa kisiasa.

Chama cha siasa kinahitaji kuongozwa na mtu mwenye Karisma na Maono vitu viwili ambavyo Mwana CCM huyu Magufuli hana. Kikwete alikuwa na Karisma lakini kina Lowassa na kundi lake wakamsaidia kuweka maono. Kwa kutumia Karisma yake akawatumia wana mkakati Nape na Kinana kupambana na Lowassa lakini alipotaka chama kiwe na Maono alimtafuta Mangula toka kwenye mashamba yake ya Viazi kuja kuwa Makamu mwenyekiti wake.

Hakuna jambo mahsusi ambalo Magufuli amewahi kulifanya kwa miaka zaidi 20 aliyokuwa kwenye siasa linaloweza kumfanya kuwa na sifa ya kuongoza taasisi kubwa ya kisiasa kama CCM. Mtu asiye kuwa na Karisma wala maono kwenye taasisi ya kisiasa ni msiba mkubwa. Mkapa alikuwa na Maono lakini alimtumia Malecela aliyekuwa na Karisma kuendesha CCM wakati yeye akiendesha Serikali.
 
Naona una 'personal vendetta" na JPM. Kama huoni karisma wenzako tunaiona kwa wingi. Na kama huoni unasiasa wake, tulio wengi tunaona ni mwanasiasa aliyebobea. Ndiyo sababu akawa mbunge wa Chato kwa miaka 2 mfululizo
 
Hakuna ukweli ktk ulichokiandika,hivi ni maono gani yaliyowekwa na viongozi walioko madarakani na wale waliopita?CCM ilipoteza mwelekeo & dira kitambo sana na mtu anayeweza kuirudisha CCM ktk njia sahihi ni Dr Magufuli,CCM haipaswi kuimarishwa kwa siasa za fitina,propaganda, kutumia nguvu za dola au kufanya siasa kupitiliza hata ktk masuala muhimu ya kitaifa vitu ambavyo Kikwete na Mkapa waliviweza sana,bali CCM ili kuimarika kinahitaji kukubali kuishi ktk zama za siasa za nguvu za hoja.Ni mazingira ndiyo yanayopaswa kuiimarisha CCM,kama vile kuwa tayari kuachana na ufisadi,kufanya maamuzi yanayotanguliza maslahi ya wananchi mbele,wawe tayari kufanya safi zinazoweka maslahi ya nchi mbele na chama nyuma.Haya ndio mambo ambayo Dr Magufuli anayapigania ila najua kuna mchwa wengi tu ndani ya hicho chama hawataki kabisa kuona Dr Magufuli akipewa Uenyekiti kwani mirija yao ya upigaji ndani ya chama na serikalini itakatwa rasmi,na wao wana hoja kama ya kwako dhidi ya Magufuli.
 
Naona Leo umesahau kumeza vidonge vyako vya Wazimu. Ila nakukumbusha tu huyo unayemuongelea ni RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. Uwe na adabu kidogo.
 
Ila nakukumbusha tu huyo unayemuongelea ni RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO (WA) TANZANIA. Uwe na adabu kidogo.
Hapana hapa simuongelei Rais wa Jamhri ya Muungano Tanzania bali namuongelea Mwanachama wa CCM anayeitwa John Pombe Magufuli! Na hilo neno "wa" limehaibu sentesi yako.
 
Dalili za watu kumuogopa Magufuli ndio hizi na ndio hawa hawa waliosema Magufuli anafaa kutumikishwa kama Mtendaji na sio kuwa kama Rais na kuwatumikisha wengine watende. Ni vigumu mtu aliye nje ya CCM kuwa na maono ya njia wanazopaswa kupita CCM. Kama Lowassa ameweza kuwa kiongozi mkuu wa UKAWA na CDM(indirectly) Ugumu uko wapi kwa Magufuli.
 
Sasa wewe usitake kutupeleka kwenye mambo ya urais wa Magufuli. Hapa tunamzungumzia Magufuli Mwanachama wa CCM. Halafu labda iwe mtu anataka kujibaraguza au kujifaragua kumlinganisha Lowassa na Magufuli kisiasa. Lowassa kisiasa kwa Magufuli ni Mlima na Magufulil ni kichuguu!!
 
Ili nchi iende mbele viongozi aina ya JPM ndiyo wanatakiwa kuongoza vyama.
Wakati wa bla bla umepita tunataka maendeleo. Muda wa kuchekeana haupo.
Tangu lini umegundua kuwa nchi yetu iko nyuma kimaendeleo na unadhani ni nani kasababisha tuwe nyuma kimaendeleo?
 
Acha hizo, sasa leo CCM inakuwa juu ya serikali, tangu lini kama siyo kujiridhisha wenyewe kwa wenywewe. Kuna nchi hazina chama lakini hakuna nchi isiyokuwa na Rais. Watanzania kwa sasa tuko zaidi ya milioni 45, wana CCM jumla yao hawazidi milioni tano. CCM ni sawa na Chadema, Chauma, TLP, taja chochote unachokijua, tofauti ni kwamba CCM ni chama kikongwe na kinachoongoza serikali kutokana na uchaguzi ambao hakika mwaka jana kama si Magufuli saa hizi tungezungumza mengine ndiyo maana hata katika kampeni tuliambiwa chagua Magufuli, sikuona bango lililoandika chagua CCM. Narudia tena nchi inawerza kwenda bila chama cha siasa lakini haiwezi kwenda bila serikali. Rais anapigiwa mizinga 21, mwenyekiti wa chama anapigiwa mingapi. Rais ndiyo serikali na serikali ndiyo Rais. Hivi mwenyekiti wa chama kinachotawala Marekani anaitwa nani, mimi namjua Rais wa Marekani ananitwa Obama, wala hatuna sababu ya kumjua mwenyekiti wa chama kunachotawala China, Japan Uingereza, lakini marais tunawajua.
 
JPM kafaa kwa nafasi kubwa ya urais sembuse uenyekiti wa Chama. Mimi si mwanachama wa chama chochote cha siasa. Tuwashindanishe sasa JPM akabidhiwe CCM sasa na Lowasa akabidhiwe CDM halafu tukutane Oktoba 2020 kupima nani aliona wanachotaka wenye nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…