Magufuli awaaibisha wale waliokuwa wanasema hajui kiingereza

Aliyeleta huu uzi ndo mpuuzi. Kwanini atudanganye kwamba Magufuli kaongea Kingereza kwa ufasaha na ujasiri wakati video aliyoipost inaonesha vinginevyo?Hata hizo lugha nyingine kuna sehemu kakosea. Hakukua na maana ya kuanzisha uzi wa kipuuzi kama huu.Kiingereza ni lugha kama nyingine lakini tuache uzushi na uongo
 
Hahaha " everybody knows the definition of catalyst, it is the substance that speeds up the reaction.....". Do chemistry at work. Kila mtu na fani yake
......Without itself undergoing permanent chemical change.
 
Baadhi mambo ni kuyaacha kama yalivyo mtu akija jambo la hovyo si lazima kujibu
Hivi we mtoa mada na wewe umekaa kupoteza muda wako kwa jambo la ajabu. Rais amewahi kuwa mwalimu wa sekondari na ni Dk. vitu vingine kwa waelewa ilikuwa ni enzi ya kampeni.. Rais yuko vizuri sana.
 
MAGUFULI AWAAIBISHA WALE WALIOKUWA WANASEMA HAJUI KINGEREZA

Unapozungumza jina la Dr John Pombe Magufuli ni jina lilopata umaarufu sana duniani kote kuanzia mwishoni mwa mwaka jana baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo kwa sasa Dr. Magufuli (CCM) ndio Rais wa Tanzania awamu ya tano , Magufuli ni raisi mwenye busara, mvuto kwa jamii, weredi, jasiri,mwenye huruma na wanyonge,mzungumzaji mzuri(good speaker) na mtu mwenye uwezo mkubwa wa akili (IQ and EQ).

Katika kipindi cha kampeni mwaka jana kulitokea uzushi uliosambazwa na wapinzani juu ya mgombea wa CCM hususani UKAWA kwamba mgombea wa CCM Dr. Magufuli hajui kuongea Kingereza. Uzushi huu ulienezwa kwa kasi na kufanya baadhi ya watu kuamini kuwa ni kweli, lakini kumbe sio kweli ilikuwa ni kutaka kumchafua kisiasa. Rais Magufuli aliposhinda uchaguzi na kuwa rais alianza kuwadhihirishia kuwa anajua kuongea kingereza pale alipokuwa anakutana na wageni mbalimbali Ikulu na kuzungumza nao kwa lugha ya kingereza na wapinzani hao kukaa kimya kwa aibu.

Leo katika mkutano wa 17 wa EAC Raisi Magufuli akiwa mwenyekiti wa mkutano huo AMEWAAIBISHA KABISA WAPINZANI WAKE KWA KUONGOZA MKUTANO WOTE KWA LUGHA YA KINGEREZA na kuzungumza kingereza fasaha kabisa kwa ujasili na ubora wake ule ule kama akiwa anazungumza lugha adhimu ya Kiswahili. Pia haikuishia hapo Rais Magufuli akawadhihirishia wana EAC kuwa yeye ni bora katika lugha kwa kuzungumza lugha zote za EAC kuanzia KIGANDA, KINYARUANDA, KURUNDI, KIJALUO, na kushangiliwa kwa makofi makubwa na wajumbe wa mkutano huo kwa uwezo wake huo wa kuzungumza lugha mbalimbali kwa ubora ikiwemo pia KINGEREZA NA KISWAHILI kwa ubora wa hali ya juu.

Sasa ujinga wa kusema Magufuli hajui kingereza utakuwa ni unyumbu kwani lazima ujiulize, je, leo Magufuli kashikiwa mdomo sio yeye aliyekuwa anazungumza? Je, alivyoongea watu walikuwa hawamsikii au?? Je, anavyokuwa Ikulu na wageni nyie Nyumbu ndio mnakuwa mnamsemea?? Je , PhD yake ninyi nyumbu ndio mliomsaidia kusoma ?? Ukitaka kujua wewe ni Nyumbu sema tena Magufuli hajui ongea kingereza wakati EAC wote wamejionea wenyewe Jembe JPM akiunguruma Ngurudoto na kutumbua majipu ya EAC kwa kutumia kingereza, kwa kweli ukisema tena Magufuli hajui kingereza utakuwa nyumbu tu , maana utakuwa huna akili bali wewe una yako mengine au wewe ndio hujui kingereza.

Kweli Magufuli ni GIFTED LEADER tulienaye Tanzania , Tumuunge mkono na kumuombea kwa Mungu amlinde azidi kututumikia watanzania wote kwa ubora na weredi, leo kadhihirisha kuwa viongozi bora Afrika wataendelea kutoka Tanzania. HONGERA MAGUFULI KUONGOZA VIZURI MKUTANO EAC NA KUCHAGULIWA TENA KUONGOZA EAC KWA MWAKA MMOJA ZAIDI.

[HASHTAG]#LONG[/HASHTAG] LIVE TANZANIA

[HASHTAG]#LONG[/HASHTAG] LIVE EAC

[HASHTAG]#LONG[/HASHTAG] LIVE AFRICA

[HASHTAG]#HAPAKAZITU[/HASHTAG]


By Mkulima Omi K.


Kwa Hivyo hii ndio inglishi ya Magufuli..."We are not supposed to be moving in the same directions, we are supposed to move together..."
 
Wote katika uzi huu tuanze kuchangia kwa Kingereza. Tuone watabaki wangapi wenye hadhi ya kukosoa wengine kwa lugha hiyo.
Faiza sio nani anaweza kiasi gani!
Ni Magufuli kwa status yake na level yake ya elimu!
Upo sahihi unapotaka wachangiaji watumie kiingereza Ila sema hivi!
" KILA MTANZANIA MWENYE PhD ACHANGIE KWA KIINGEREZA" Labda kuna kitu tunaweza kugundua! Kama JPM amesoma STD 1 to PhD in Tanzania tunamkisia awe na miaka zaidi ya 15 ya training inayotumia kiingereza kama lugha ya kufundishia plus miaka kadhaa ya ualimu, hakika alipaswa awe comfortable na hiyo lugha ya kigeni!
Hebu wenye PhD mjipange tuwaone kwanza!
 
Hapa ndio utaona jinsi tunavyo pagawa.
Eti ENGLISH,
kamwe hatutaendelea kufikiri kujua English ndio , Uongozi bora, ndio itatutoa kwenye mawingu ya Umasikini wa wa ubongo!

Wa aibike, au kwa wale wanaongea lugha za ukoloni, shame on you! Kidhungu Kha
 
Tena Wewe KIINGEREZA Chako Ambacho Huwa Unakiandika Humu JF Huwa Ni Chepesi Sana Ambacho Hata Mwanangu Wa Kiume Samora Gentamycine au Dada Yake Mwanangu Wa Kike Isabella Gentamycine Wanakuzidi Tena Mbali Sana Hicho KIINGEREZA Chako. Nimalizie Tu Kukuuliza Hivi Kuna UHUSIANO GANI KATI YA KUJUA KIINGEREZA CHA KUZUNGUMZA NA UTENDAJI WAKO WA KAZI ILI NCHI IPIGE HATUA ZA KIMAENDELEO? Katika Principles Za LEADERSHIP Katika Management Hakuna Kipengele Cha Kuzungumza Kiingereza Bali Kuna Haya Yafuatayo:

L = LORD FEARING PERSON.
E = ENERGETIC.
A = ACCOUNTABILITY.
D = DEDICATED.
E = EDUCATED ( Na Hawajasema Kuwa Ni Lazima Uwe Wordssmith au Linguist Bali Wanasisitiza HAPA KAZI TU )
R = RELIGIOUS.
S = SACRIFICE.
H = HONEST.
I = INTELLIGENT.
P = PATIENCE.

Jivunieeni KSWAHILI Chenu Na Hiyo Lugha Ya KIINGEREZA Mnayoisifia Siyo HALALI Kwenu Na Achaneni Nayo!
WEWE nenda straight to the point sio unajaza server-au una la kufanya??
 
Jamani kama hajui si hajui kuna haja gani ya kuwa asira kwa wanaomtetea au kwa vile ni rais mbadhani anajua kila kitu, hivi nyie mnavyokisikia hicho kizungu cha kukariri mnadhani anaweza kuwa MC, au anaweza kutangaza mpira.vilevile kutojua kitu sio dhambi, na sio kila rais lazima ajue kiingereza, mbona watu wengi wakitoka mikoani wanaambiwa hawajui kiswahili vizuri, lakini ni vigumu kwa kijana aliyezaliwa mjini kuambiwa hivyo.
 
Wote katika uzi huu tuanze kuchangia kwa Kingereza. Tuone watabaki wangapi wenye hadhi ya kukosoa wengine kwa lugha hiyo.
Mama wa gerezani kajua kidhungu imekuwa taabu-sasa sio unatutisha-fungua thread ingine tu flow
 
Sii kweli rais, Magufuli Kiingereza, hakipandi, Kiingereza kinapanda sana, na ushahidi ni hata mechi ya jana ya Taifa Stars, aliangalia kupitia Super Sport, hivyo hoja kuwa Kiingereza hakipandi sio kweli
P
 
Back
Top Bottom