Rais Magufuli amekerwa na mahakimu ambao wanachelewesha kesi na kukosesha haki isitoke mapema.
Lakini Rais inaelekea hajaelezwa ukweli wote wa sekta hii na kibaya zaidi hakuwahi kufanya kazi katika sekta ya Kazi na Ajira na inawezekana hana picha kamili.
Kinachotokea kwa mahakimu ndiho kilkile kinachotokea kwenye kesi za ajira pale Tume ya Usuluhishi na Uamuzi yaani CMA.
CMA ilipoanza kesi za ajira zilikuwa hazimalizi hata miezi sita. Lakini ssa hivi CMA pameanza kupoteza matumaini kwani kesi sasa zinamaliza hata miaka miwili kwa sababu ambazo hazina mashiko kabisa.
Unashitukia kwamba malamikiwa hakuja na shahidi halafu eti kesi inaahirishwa, tena ikiahirishwa si chini ya mwezi. Watu wa CMA wanaoitwa "Mediator" au "arbitrator" haaoni shida yoyote kuahirisha, tena kuna siku tulishuhudia mtu unaingia tu unakuta anajitayarisha kuiahirisha, tena jamaa hana wasiwasi.
Hii imefanya CMA pawe na mrundikano wa kesi na ukienda pale kwenye saa nne asubuhi utakuta pamejazana sawa tu na Muhimbili ambako Magufuli anaenda kila mara.
Pale CMA kwenye jengo la "Simba Building" lililoko kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi, imefika mahala ukiambiwa kesi yako fika saa 04:00 asubuhi na ukafika kamili muda huo, ukifungua mlango unatarajia kumuona "arbitrator" anakusubiri kuanza kesi.
Lakini kwa wingi wa mrundikano wa kesi, badala ya kuingia moja kwa moja kwa sababu muda ni ule uliandikiwa kwenye summons, unakuta bado kuna watu ama wanafanya kesi (mediation au arbitration).
Sasa inapotokea hivyo, huku nje hamjui sasa msubiri kwa muda gani nampo wengi. Vurugu ni pale wanaotoka wale waliokuwemo, utadhani wewe wa saa 04:00 utaitwa kama tunavyoitwa wagonjwa hospitali. Si hivyo, eti kinachotokea ni mjanja kuwahi na kuingia na kukaa kwa mheshimiwa.
Ukiachilia mbali matatizo ya kupigwa joto wakati hakuna AC na hata wamuzi wenyewe kuvuja jasho, tabia hizi mbili za pale CMA ni kikwazo kikubwa, kwani kadiri unavyosota na kesi yako pale CMA basi mwajiri ndivyo anavyovimba kichwa na kuwakomesha waajiriwa wengine kwani wanaona jinsi unavyosota na CMA na hivyo wanaogopa.
Mwaka jana wakati wa Mei Mosi, Mgaya wa TUCTA alisema wazi tena magazetini kwamba CMA pananuka rushwa na uchunguzi ufanyike. Sasa sijui uchunguzi unafanyika kweli au la,au sasa hasira za wafanyakazi wa CMA zimegeuka katika sasa wacheleweshe kesi ingawa ni kweli mwishoni unaweza kuipata.
Siku moja hukumu ya jamaa japo alishinda ilichelewa eti kwa sababu CMA hawakuwa na orinter na ikaahirishwa kwa zaidi ya wiki. Siku nyingine hakukuwa na sababu anawaambia njoo kesho
Hivyo, Rais Magufuli afanye kama Muhimbili. Siku moja aende pale CMA, siyo lile jengo ma Headquarter, bali lile la pembeni yake liitwalo SIMBA, na akute watu wamejazana pale awauize sababu za kujazana na awaulize kwa nini kesi zao zimechelewa. Ukweli sababu ni kama nilivyoeleza na wengine mtaongezeamliokwishapata matatizo hayo.
Kama Rais kataarifiwa kwamba kuna mahakimu wameshindwa kufikisha kesi 200 kwa mwaka, kwani hata CMA kusiwe na kiwango kwamba "arbitrator" awe na kesi kadhaa kwa mwaka na asipofikisha atumbuliwe jiu kwa sababu anachelewesha haki.
Hivyo, CMA ni jipu linalostahili kutumbuliwa kama mtakavyoeleza wengie humu.
Mchangiaji.