MR VICTOR KAPESA

New Member
Mar 18, 2024
4
3
Kuhusu usafiri wa haraka nchini Tanzania, kuna jitihada za kuboresha miundombinu na huduma za usafiri, hasa katika miji mikubwa kama Dar es Salaam. Mradi wa mabasi yaendayo kasi ni moja ya mikakati inayolenga kupunguza msongamano wa trafiki na kuboresha usafiri mijini. Hata hivyo, bado kuna changamoto z kukamilisha miundombinu na kusimamia huduma ili kuhakikisha ufanisi wa usafiri huo.
Changomoto kubwa ipo kwenye kipengele cha usimamizi: Kuna changamoto katika usimamizi wa huduma za usafiri wa haraka, ikiwa ni pamoja na utoaji wa tiketi, ulinzi, na usalama wa abiria.( Unakuta abiria wamejaa mpaka wanakosa nafasi ya kugeuka kupumua) lakini bado wadau hawalioni ilo haya magari ya mwendo kasi yanajaa sana kweli hasahasa jioni watu wakiwa wanatoka kazini.
Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba idadi ya watu inaongezeka sasa tanzania ya sasahivi hasahasa mkoa wa Dar es salaaam kuna uhitaji mkubwa sana wa kuboresha na kupanua hizi barabara kwa sababu huwezi ukaongeza magari ya mwendo kasi zaidi utasababisha misongamano barabarani.
 

Attachments

  • 8d5226d809304fd4b176832e55eca4e2.mp4
    809.2 KB
Back
Top Bottom