Madalali wa bongo mna matatizo gani lakini?

Mr mutuu

JF-Expert Member
Jan 27, 2023
2,848
14,302
Wiki hii nimekua nafatilia sana pages za madalali wa magari, Kuna gari ya ofisi nataka kununua kutokana na bajeti nimeamua nianze na used kwanza, sasa hao madalali yaani ni vichekesho tu

"Gari ya muhindi, dukani na nyumbani tu"

"Gari ya mdada"

"Gari ya baba mchugaji hii"

"Gari ya mrembo wa kiarabu"

"Chuma Haina kipengere(ni kama wote walishakubaliana kutotumia neno kipengele kabisa wote wanaandika kipengere)

Ukikuta gari zile za zamani namba A na B wanakuambia "chuma imekaza balaa, ni kuweka wese na kuondoka"

" Lete hela haraka tajiri ameshavurugwa akili"

Kuna magari hata hawaweki hata basic information kama yom,cc,odometer ,yaani ni kutia udamvi udamvi
 
Unaongea ukweli, na hii yote tuwavumilie tu maana elimu madalali hawana, hawana elimu ya biashara wala elimu ya shule. Ndio matokeo yake, mtu anauza gari anakuwa mbabe sana

Hana lugha ya biashara, hapo inabidi wewe mteja ndio uwe mpole na sio muuzaji hahahha

NAUZA BASI LA SHULE MILLION 39.8
NAMBA EF

NAUZA RAUM
MILLION 12.8
NAMBA DX

📱📲 GARI IPO DAR ES SALAAM USITUME SMS SIJUI KUCHATI ❌🚫👎
PIGA SIMU MUDA OTE NA POKEA ATA KAMA NIPOCHOONI NA KATA GOGO NA POKEA SIMU.
 
Ilipostiwa bajaji namba B, bei 1.8m, ipo Zakhem.

Kufika eneo la tukio, nikaambiwa imeuzwa, na ipo nyingine ambayo sikuridhika nayo.

Nikarudi. Dakika chache baadaye inapostiwa nyingine, nikaulizia bei nikaambiwa imeuzwa.

Sasa nikauliza, hii ya pili sikuikuta lakini inapostiwa na ninaambiwa imeuzwa tayari; inakuwaje?

Kuna mmoja alifunga safari toka Zenji hadi Kwa Msuguri kwenda kuiona bajaji. Anafika pale anakutana na kitu kingine kabisa.

Wengine ukiwauliza bei wanakupa namba ya simu.

Yote haya yanaharibu biashara yao na kuonekana matapeli tu.
 
Unaongea ukweli, na hii yote tuwavumilie tu maana elimu madalali hawana, hawana elimu ya biashara wala elimu ya shule. Ndio matokeo yake, mtu anauza gari anakuwa mbabe sana

Hana lugha ya biashara, hapo inabidi wewe mteja ndio uwe mpole na sio muuzaji hahahha

NAUZA BASI LA SHULE MILLION 39.8
NAMBA EF

NAUZA RAUM
MILLION 12.8
NAMBA DX

📱📲 GARI IPO DAR ES SALAAM USITUME SMS SIJUI KUCHATI ❌🚫👎
PIGA SIMU MUDA OTE NA POKEA ATA KAMA NIPOCHOONI NA KATA GOGO NA POKEA SIMU.
😂😂😂
 
Wiki hii nimekua nafatilia sana pages za madalali wa magari, Kuna gari ya ofisi nataka kununua kutokana na bajeti nimeamua nianze na used kwanza, sasa hao madalali yaani ni vichekesho tu

"Gari ya muhindi, dukani na nyumbani tu"

"Gari ya mdada"

"Gari ya baba mchugaji hii"

"Gari ya mrembo wa kiarabu"

"Chuma Haina kipengere(ni kama wote walishakubaliana kutotumia neno kipengele kabisa wote wanaandika kipengere)

Ukikuta gari zile za zamani namba A na B wanakuambia "chuma imekaza balaa, ni kuweka wese na kuondoka"

" Lete hela haraka tajiri ameshavurugwa akili"

Kuna magari hata hawaweki hata basic information kama yom,cc,odometer ,yaani ni kutia udamvi udamvi
Kudeal na madalali wa kibongo kunatakiwa kuwa na moyo aisee. Binafsi sidhani kama wanajitambua akili hawa watu, utakuta mtu unamwambia dalali nataka nyumba ya aina fulani na anakuambia ipo, mnaenda kuona hiyo nyumba unakuta siyo kisha anakuambia "hata hii poa tu" haina tofauti sana na ile uliyoitaka. Nakiri kusema kuwa Madalali wa kibongo hawana akili na hawajuwi kazi yao, ni wababaishaji mno.
 
Wiki hii nimekua nafatilia sana pages za madalali wa magari, Kuna gari ya ofisi nataka kununua kutokana na bajeti nimeamua nianze na used kwanza, sasa hao madalali yaani ni vichekesho tu

"Gari ya muhindi, dukani na nyumbani tu"

"Gari ya mdada"

"Gari ya baba mchugaji hii"

"Gari ya mrembo wa kiarabu"

"Chuma Haina kipengere(ni kama wote walishakubaliana kutotumia neno kipengele kabisa wote wanaandika kipengere)

Ukikuta gari zile za zamani namba A na B wanakuambia "chuma imekaza balaa, ni kuweka wese na kuondoka"

" Lete hela haraka tajiri ameshavurugwa akili"

Kuna magari hata hawaweki hata basic information kama yom,cc,odometer ,yaani ni kutia udamvi udamvi
Wabongo tuna matatizo sana. Tunapenda kuigana mpaka makosa. Nimependa sana hapo ulipoandika ''kipengere''. Kuna neno jingine linakosewa lakini huwa linatumika sana na matapeli ''tafadhari''.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom